PICHA NA SAUTI ZAJA HIVI PUNDE.
Watu wanne wameripotiwa kufariki dunia katika matukio manne tofauti mkoani Mwanza vikiwemo vifo vilivyo sababishwa na ajali za barabarani.
Watu wanne wameripotiwa kufariki dunia katika matukio manne tofauti mkoani Mwanza vikiwemo vifo vilivyo sababishwa na ajali za barabarani.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Mwanza Valentino Mlowola amesema Katika tukio la kwanza mtu aliyejulikana kwa jina la Japhery Reluwe mwenye umri kati ya miaka 25-30 mkazi wa Tanesco amefariki dunia baada ya kugongwa na gari aina ya balloon katika barabara ya Kenyata –Maliasili.
Katika tukio jingine mtu mmoja ambaye hajafahamika jina lake anaesadikiwa kuwa na umri wa kati ya (20-30) aliuawa kwa kupigwa na kisha kuchomwa moto na kundi la wahalifu katika eneo la kiloleli kata ya nyamanoro wilayani Ilemela mkoani Mwanza.
Aidha mapema LeoMtu mmoja ambaye pia hakufahamika jina lake amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa katika ajali mbaya iliyohusisha lori aina ya Scania lenye namba za usajili T 442 BSH mali ya kampuni ya Nyanza Botling Company Ltd (Cocacola) ya jijini Mwanza na pikipiki aina ya Sanya yenye namba za usajili T 115 CKP mali ya Aristides Fidelis .
Ajali hiyo ambayo imetokea katika eneo la taa za kuongozea magari barabara ya Nyerere na hatimaye gari hilo kuungua moto, imesababisha kifo cha abiria aliyekuwa katika pikipiki ambaye hajafahamika jina lake na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando.