Quantcast
Channel: g sengo
Viewing all 12408 articles
Browse latest View live

Article 2


WATANO KATI YA WALIOTOKA JELA KWA MSAMAHA WA RAIS WAUAWA NA WANANCHI.

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon
CHANZO/MWANANCHI
Dar es Salaam. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema watu watano waliotoka gerezani kwa msamaha wa Rais John Magufuli wameuawa na wananchi baada ya kurejea katika matendo maovu.

Sirro aliyewataka wanaoachiwa huru kwa msamaha wa rais kutorejea katika matendo hayo, ametoa kauli hiyo   leo Alhamisi Mei 24, 2018 mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akitoa taarifa ya ujenzi wa vituo vya polisi vya kisasa vya Mburahati, Kiluvya-Gogoni na Mbweni vilivyozinduliwa leo.

“Nia ya Rais Magufuli kuwapa msamaha ilikuwa njema lakini kuna baadhi ya watu wameitumia vibaya fursa hiyo na hadi sasa watu watano wamekwishauawa na wananchi,” amesema.

“Ukitoka gerezani kwa msamaha, maana yake umerekebisha mwenendo wako na wananchi wanatarajia uwe hivyo, lakini kama ukifanya vinginevyo Serikali isilaumiwe.”

Akizungumzia utendaji wa jeshi hilo, Sirro amesema tangu ashike madaraka hayo polisi wamewapeleka askari 1,267 kwenye mafunzo ya medani za kivita na wako imara.

Pia tumepeleka askari wa upelelezi zaidi ya 1,000 kwenye mafunzo ya ujuzi na ustadi wa kupeleleza kesi mbalimbali. Baada ya kuwapa mafunzo haya, tunataka kesi za kawaida upelelezi wake uwe umekamilika ndani ya miezi sita” amesema na kubainisha kuwa kesi kubwa upelelezi wake uwe umekamilika ndani ya miezi 12.

Pia, amemshukuru Rais Magufuli kwa kuwapatia Sh10 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za askari, kutoa kibali cha ajira kwa askari wapya 1,500 na kuwaruhusu wawapandishe vyeo askari wenye kustahili kuanzia cheo cha koplo hadi naibu kamishna wa polisi (DCP).



WAMILIKI WA VIWANDA VYA KUCHENJUA DHAHABU MKOANI MWANZA WAINGIWA HOFU YA KUFUNGA VIWANDA VYAO MARA BAADA YA KUINASA KAULI YA MKUU WA MKOA WA GEITA.

$
0
0

GSENGOtV
WAKATI Serikali ya Awamu ya tano ikikusudia kuanzisha soko la Kimataifa la madini jijini Mwanza ambapo tayari imeshatenga eneo kwaajili ya kuweka soko hilo ambalo licha ya kukuza sekta hiyo bali kudhibiti utoroshwaji wa madini nchini, upande wa pili, Mkuu wa mkoa wa Geita Robert Gabriel analalamikiwa na Umoja wa wamiliki wa viwanda vya uchenjuaji na wanunuzi wa dhahabu Mkoani Mwanza kwa kupiga marufuku wafanyabiashara wa madini kutoka mkoani kwake kusafirisha malighafi inayotumika kubebea dhahabu inayojulikana kama CARBON kwenda jijini Mwanza.

MIZENGO PINDA NA MAKONGORO NYERERE WAULA UTEUZI WA JPM.

$
0
0

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, amewateua Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee Mizengo Kayanza Peter Pinda na Makongoro Nyerere kuwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC).










UPANUZI WA KITENGO CHA DHARULA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO WAPIGWA JEKI YA SHILINGI MILIONI 240 NA BENKI CRBD

$
0
0

GSENGOtV
Changamoto ya rasilimali fedha kwa baadhi ya vituo vya huduma za afya nchini imekuwa kikwazo katika uboreshaji wa huduma hizo kiasi cha kuifanya sekta hiyo kutofikia malengo yanayotarajiwa.
 Kwa kuliona hilo Benki ya CRDB nchini hii leo Tarehe 25 Mei 2018 imekabidhi hundi ya shilingi milioni 240, kwa ajili ya upanuzi wa idara ya wagonjwa mahututi ya hospitali ya rufaa ya Bugando (BMC) Jijini Mwanza, ili kukabiliana na tatizo la msongamano wa wagonjwa unaoikabili Hospitali hiyo. 
 Mkurugenzi mkuu wa Hospitali ya rufaa ya Bugando Dk. Abel Makubi, ameiomba serikali kutangaza ajira mpya za madaktari, ili kupunguza uhaba wa madaktari bingwa katika idara hiyo.
 Akizungumzia matumizi ya fedha hizo kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB nchini Dk. Charles Kimei, kaimu mkurugenzi wa benki hiyo Esther Kileo, amesema msaada huo umetolewa, ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wagonjwa.
 Kutokana na umuhimu wa upanuzi wa Idara hiyo, Askofu mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Mwanza Jude Thadeus Ruwaich, ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi ya Hospitali hiyo, amesema msaada huo unahitajika, ili kutatua msongamano unaoikabili Hospitali hiyo.





 Kaimu mkurugenzi wa benki ya CRDB Esther Kileo akimpa mkono Askofu mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Mwanza Jude Thadeus Ruwaich mara wakati wa upigaji picha ya pamoja ya makabidhiano.
  CRDB katika picha ya pamoja na viongozi.
 Picha ya pamoja na wadau kitengo cha dharula.
 Baada ya makabidhiano hayo katika hatua nyingine, Benki hiyo imelikabidhi Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza Pikipiki tatu aina ya Boxer, zenye thamani ya shilingi milioni kumi ikiwa ni pamoja na gharama za usajili, ili kuboresha shughuli za ulinzi na usalama kwa mkoa wa Mwanza.
  Maelezo toka kwa mwenyeji kwa wageni.
 Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi akiwasilisha salamu za shukurani toka kwa IGP Simon Sirro kwa  Kaimu mkurugenzi Benki ya CRDB nchini baada ya kupokea pikipiki 3 kama sehemu ya kuliwezesha jeshi hili kuhudumia wananchi.
  Karibuni wageni.

 Picha ya pamoja.

MAKATIBU TAWALA WA MIKOA WAAGIZWA TAKWIMU ZA WAZEE IFIKAPO 30 JUNI 2018.

$
0
0

 Mhe. Seleman Jafo, akizungumza wakati wa Hafla ya kuwapatia Vitambulisho Wazee wa Jiji la Dodoma.


Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma akitoa salam za jiji muda mfupi kabla ya zoezi la ugawaji wa Vitambulisho kwa wazee halifanyika.

Mmoja ya Wazee akipokea kitambulisho mara baada yakuzinduliwa kwa zoezi lakuwapatia vitambulisho wazee Jiji la Dodoma.

Picha ya pamoja kati ya Mhe. Waziri Viongozi wa Halmashauri na wazee waliopatiwa vitambulisho.

 Mhe. Diwani wa Kata ya Mkonze akishukuru kwaniaba ya wananchi wa Mkonze.




Makatibu Tawala wa Mikoa Waagizwa  Takwimu za Wazee ifikapo 30 Juni, 2018

Na. Atley Kuni-OR TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Mb), amewaagiza Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara kuwasilisha taarifa za takwimu za wazee ifikapo      30, Juni 2018.

Waziri Jafo, alitoa kauli hiyo mapema leo alipokuwa akizindua  zoezi la kuwapatia  vitambulisho maalum wazee wapatao 1,118 wa Jiji la Dodoma kutoka kata za Mkonze, Mnadani, Uhuru, Madukani, Makole na Majengo. Vitambulisho hivyo, pamoja na mambo mengine vitawawezesha wazee hao kupata huduma za afya bure na kwa wakati.

“Ifikapo tarehe 15 Juni, 2018 kila kata iwe imetambua wazee na ifikapo tarehe 22 Juni, 2018 kila Halmashauri iwe imeunganisha taarifa za wazee kutoka katika kata zake zote” alisema Waziri. Aidha Waziri Jafo aliagiza kuwa, “ifikapo Juni, 26, 2018 kila Mkoa uwe umeunganisha taarifa zote na kuzituma kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI”.

Aliwaonyawale wote watakaoshindwa kutimiza agizo hilo kuchukuliwa hatua kulingana na miongozo, kwasababu watakuwa wameshindwa kutekeleza wajibu wao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Ndugu Godwin Kunambi akizungumza katika hafla hiyo alisema shabaha ni kuwafikia wazee wote kwenye Jiji hilo, na kubainisha kwamba, vitambulisho wanavyo vitoa kwa wazee hao vitatumika pia kuwapa kipaumbele wazee sehemu zote za kutolea huduma hususan ofisi za serikali.

“Mhe. Waziri tunataka vitambulisho hivi tunavyo wapatia wazee wetu leo viwasaidie pia kupata huduma kwa haraka na kwa wakati pindi wanapofika kwenye ofisi zingine za Serikali” alisema Kunambi.

Mbali na kutolea ufafanuzi wa matumizi ya vitambulisho hivyo, Mkurugenzi Kunambi alisema juu ya Jiji hilo lilivyo jipanga katika suala zima la makusanyo ya mapato ya ndani, ambayo ndio yamekuwa chachu ya kuboresha huduma za afya kwa makundi maalum hususan wazee.

“Mhe. Waziri, Jiji limepanga kukusanya Bil. 68 katika mwaka wa fedha ujao ikilinganishwa na mwaka huu wa fedha ambapo tulijiwekea lengo la kukusanya Bil. 20 nahadi kufikia mwezi Februari tulikuwa tumekusanya Bil. 14”. Kunambi ameongeza kuwa, katika mwaka ujao wa fedha wametenga kiasi cha Mil. 58 kwaajili yakuwezesha huduma za wazee kwenye Jiji hilo.

Naye Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Deo Ndejembi, ametumia fursa hiyo kuwaonya baadhi ya watendaji wanao waambia wazee kwamba hakuna dawa.

“Kumekuwepo na malalamiko mengi siku za nyuma kutoka kwa wazee kuwa, baadhi ya watendaji wa afya wanawanyanyapaa wazee na kuwaambia hakuna dawa wafikapo vituoni, sasa Mhe Waziri, mimi niliseme kwa uwazi kabisa hatuta mvumilia mtu yeyote atakaye onekana ni kikwazo kwa wazee hawa kadi zimetoka wazee wahudumiwe, sio mnajiwekea vijiduka karibu na vituo halafu mnawaambia waende waka nunue” alionya Ndejembi

Awali akitoa taarifa ya uandaji wa vitambulisho Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma, Dkt. Mohamed Nyembea, alisema utekelezaji wa zoezi hilo ulianza kwa hatua za awali kwa kuwatambua wazee katika Kata 41 za Jiji la Dodoma, ambapo jumla ya wazee 15,885 kutoka kata 33 miongoni mwa 41 wamekwisha tambuliwa  na miongoni mwao wanawake ni 9,132 na wanaume ni 6,753 ambapo ni sawa na asilimia 80.5 ya  kata zote 41 za Jiji la hilo.

Utoaji wa vitambulisho kwa wazee ni utekelezaji wa sera ya Taifa ya wazee ya mwaka 2003 ambapo inazungumzia mambo muhimu ya wazee ikiwepo kutenga dirisha maalum katika vituo vya kutolea huduma za afya.  

KABLA YA FAINALI YA LEO USIKU HEBU TUJIKUMBUSHE

USIKU WA LEO NI LIVERPOOL AU REAL MADRID UEFA CHAMPIONS LEAGUE.

$
0
0
FAINALI ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2018 inafanyika leo Olimpiki NSK mjini Kiev, Ukraine ikizikutanisha Liverpool ya England na Real Madrid ya Hispania kuanzia Saa 21:45 usiku.

Hiyo itakuwa fainali ya 63 ya michuano hiyo inayoandaliwa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), na msimu wa 26 tangu ipewe jina jipya la Ligi ya Mabingwa Ulaya kutoka lile la zamani la Klabu Bingwa Ulaya.

Mshindi wa mchezo wa leo atakutana na mshindi wa fainali ya UEFA Europa 2018 katika Super Cup ya UEFA. Pia watafuzu kuanzia hatua ya Nusu Fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA mwaka 2018 FIFA kama wawakilishi wa UEFA Mabingwa watetezi, Real Madrid walitinga fainali ya 16 ya rekodi baada ya ushindi wa 4–3 jumla dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani wakiwatupa mashindanoni kwa mara ya pili mfululizo. 

Na hii ni fainali ya tatu mfululizo ya Real Madrid na fainali ya nne kwenye mashindano matano huku ikipewa nafasi ya kushinda taji la 13 la rekodi, baada ya awali kushinda katika miaka ya 1956, 1957, 1958, 1959, 1960, 1966, 1998, 2000, 2002, 2014, 2016 na 2017; na kufungwa katika fainali za 1962, 1964 na 1981. 

Liverpool wameingia fainali ya nane, na ya kwanza tangu mwaka 2007, ambayo walishinda kwa jumla ya mabao 7–6 dhidi ya Roma ya Italia. 

Wameshinda taji hilo mara tano katika miaka ya 1977, 1978, 1981, 1984 na 2005, na wamefungwa mara mbili kwenye fainali 1985 na 2007. 

Mwandishi mmoja aliyehudhuria mazoezi ya Real Madrid jana aligongwa usoni na mpira uliopigwa na Cristiano Ronaldo na kuchanika kidogo jirani ya jicho.

Real walikuwa wanafanya mazoezi Uwanja wa Olimpiki mjini Kiev kuelekea fainali leo na ndipo Ronaldo alipompiga na mpira mwandishi huyo. Lakini Ronaldo alimuomba msamaha kwa ishara ya mkono mwandisi huyo aliyepatiwa huduma ya kwanza uwanjani hapo.

Beki ghali aliyesajiliwa Liverpool kwa dau la Pauni Milioni 75 amesema kwamba Real Madrid hawajawahi kukutana na timu kama yao kabla.

Amesema; nani anajali? Alipoulizwa kama Wekundu hao walistahiloi kufika gainali ya Ligi ya Mabinghwa Ulaya.

Mashabiki wa Liverpool walishambuliwa na wababe mjini Kiev juzi, kabla ya Polisi kuthibitisha watu wawili walikamatwa.

Picha za kutisha zimeonyesha watu wakishambuliana kwa kwa magongo, meza na viti. Polisi wa Merseyside wamesema wana taarifa za tukio hilo na wana Maofisa wao mjini Kiev.

Gwiji wa England, David Beckham amemtaka mchezaji mwenzake wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane sasa kocha wa klanbu hiyo kushinda fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool: 'Tafadhali wafunge Liverpool'
Beckham ni mpenzi wa Manchester United ambao ni wapinzani wa Liverpool. 

Beckham aliondoka Old Trafford kuhamia Los Blancos kwa dau la Pauni Milioni 25 mwaka 2003.

MATUKIO KATIKA PICHA 'NI REAL MADRID MABINGWA TENA UEFA 2018'

$
0
0
Uso kwa uso msindi ni mmoja tu. 
 Kikosi  cha Real Madrid leo kilikuwa; Navas, Carvajal/Nacho, Varane, Sergio Ramos, Marcelo, Modric, Casemiro, Kroos, Isco/Bal, Benzema/Asensio nA Ronaldo
 Liverpool starting XI: Karius, Alexander-Arnold, Lovren, Van Dijk, Robertson, Milner/Can, Henderson, Wijnaldum, Salah/Lallana, Firmino ma Mane.
 Fainali UEFA Champions League 2018
 Kiev 2018
Marcelo v Salah 
Kabla ya kutolewa kutokana na rafu mbaya aliyochezewa na Ramos, Mo Salah alikuwa mwiba dimbani 
 Mashabiki Liverpool
Mashabiki Real Madrid 
Liverpool ilipata pigo mapema tu katika mchezo wa leo, baada ya mshambuliaji wake nyota, Mmisri Mohammed Salah kutolewa nje dakika ya 30 kufuatia kuumia baada ya kugongana na beki na Nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos. 
Hawezi endelea tena na mchezo. 
 Hakuna jinsi.
 Kipa Karius akawazawadia bao la kuongoza Real Madrid baada ya Karim Benzema kumpiga mpira bila uangalifu mbele ya Mfaransa huyo ukamgonga na kuingia nyavuni dakika ya 51. 

Mshambuliaji Msenegali, Sadio Mane akaisawazishia Liverpool dakika nne baadaye, kabla ya Gareth Bale kutokea benchi na kufunga mabao mawili dakika za 64 na 83. 
 Ni goli.
 Farao.

  Karius aliwasili Liverpool akitokea Mainz mwaka 2016 na alikuwa na mwanzo mgumu kabla ya kuzinduka na kuwa kipa chaguo la kwanza mbele ya kocha Jurgen Klopp akimpindua kipa Simon Mignolet. Lakini makosa ya leo ya Karius hayatasahaulika milele. 
  Karius amechangia anguko la Liverpool.
 Benzema akisherehekea.
 Tick tak.
 Goal.....
 It is......
TIMU ya Real Madrid imefanikiwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya tatu mfululizo baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Liverpool usiku wa Jumamosi Uwanja wa Olimpiki mjini Kiev, Ukraine. 
PICHA/AFP

MATOKEO UEFA YAMUUWA SHABIKI HUYU

KINANA, MBUYU KWENYE MSITU WA SIASA

$
0
0
Image may contain: 2 people, people smiling, people standing

Na Emmanuel J. Shilatu

Kanali Mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Abdulrahman Omar Kinana anatajwa kuwa katika orodha ya safu za viongozi mibuyu na migude kwenye misitu minene ya siasa yenye kuhimili tufani za kila aina pia Mwanasiasa anayependa kuheshimu utamaduni, utaratibu na mwenye kuishi kwa misingi ya nidhamu .

Kinana anatajwa kama zao miongoni mwa kunga zitokanazo na mazao katika medani za siasa, utawala, uongozi na aliyeshiba ujuzi toshelezi wa masuala ya diplomasia ya siasa pia anayejua mahusiano yatokanayo na historia, harakati za ukombozi na umoja wa Afrika.

Sauti yake aghalabu huwa na mvumo wa mawimbi ya busara, fikara njema na hekima zenye wito pele aamuapo kusema, kukosoa, kutetea, kukumbusha, kushauri au kuonya kutokana na tabia yake ya kufanya yote hayo kwa hali ya kujiamini akiwa na nguvu ya hoja.

Ukimya wa Mwanasiasa huyo siku zote ni kama mfano wa Simba hodari awindae nyikani au mbugani akiwa hana pupa wala kiherehere. Huyafanya yote kwa utulivu na umakini mkubwa ambao baadae haumletei majuto, athari wala taathira.

Ni Mwanasiasa wa aina yake aliyewahi kuhitajiwa na Marais (Wenyeviti) watatu awe katibu mkuu wa CCM akakataa huku akitoa madai mazito yenye msingi, nguvu ya hoja na maana.

Amewahi kutakiwa na Rais Ali Hassan Mwinyi awe Katibu Mkuu wa CCM akakataa huku akitoa hoja. Akasema alikuwa na mchakato wa kazi nyeti na muhimu akishirikiana na wenzake kufanya mabadiliko ya mfumo mpya wa Jeshi utakaokwenda sanjari na mahitaji ya wakati; hivyo asingekuwa tayari kuiacha kabla kazi hiyo kukamilika.

Akatakiwa tena na Rais Benjamin Mkapa ashike nafasi hiyo akasita kukubali huku akitoa hoja za msingi na zenye mashiko yasio na shaka wala utata.

Kinana mara ya kwanza alitakiwa na Mwenyekiti Mstaafu Kikwete akakataa kubeba jukumu hilo kwa sababu kadhaa alizoona ni ngumu kwake kukitumikia chama kwa wakati huo. Hata hivyo mbinu za ushawishi zikafanyika akaafiki kuwa Katibu Mkuu.

Bila shaka Kinana aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wakati CCM ikiwa katika mgawanyiko mkubwa uliohatarisha uhai na mustakabali wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Kwa busara zake, pengine na ziada ya maarifa au mbinu za kijeshi, uzoefu wa kisiasa, uongozi na utawala, Chama Cha Mapinduzi na viongozi wake ghafla wakashikamana tena na kuzika yaliopita.

Amewahi kusema mbele ya Mzee Mkapa kwa wakati ule amejiona mbele yake bado ipo hazina ya Viongozi wajuzi wa muda mrefu ndani ya chama, vingunge wenye weledi na maarifa ya kisiasa kuliko yake hivyo muda wa yeye kushika wadhifa si wakati huo.

Akaachwa na kuendelea kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM akiwa Meneja wa kampeni za wagombea urais Mzee Mkapa na Dk. Jakaya Kikwete.

Katika safu ya Vijana wa TANU Youth League na baadae UVCCM waliolelewa kwenye mikono ya Wanasiasa kama kina Mwalimu Julius Nyerere, Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi, Sheikh Thabit Kombo Jecha, Mzee Rashid Kawawa, Mzee Saadan Abdul Kandoro na Mzee Rajab Diwani, Kinana anaweza kusimama kati yao.

Ameshiriki pamoja nao katika mbio za siasa, akichuma uzoefu huku mbele yake kukiwa na Wanasiasa kama Mzee Pius Msekwa, Marehemu Kingunge Ngombare Mwiru, Mzee John Malecela, Hayati Daudi Mwakawago, Hayati Moses Nnuye, Balozi Chrispher Liundi, Ali Ameir Mohamed na wengine kadhaa.

Vijana wanasiasia wa rika lake na wanaopishana kwa umri kiasi kidogo ni kina Dk Kikwete , Dk Mohamed Seif Khatib, Dk Salmin Amour, Yusuf Makamba, Jaka Mwambi, John Chiligati, Marehenu Ukiwaona Ditope Mzuzuri na wengine wengi .

Kanali Mstaafu Kinana kama atajigamba amezaliwa na kulelewa ndani ya TANU/ASP na maisha yake yote amekulia CCM na serikali zake, hoja hiyo itajuzu na kuyakinika.

Kwa ufupi ni Mwanasiasa asiyebahatisha katika utambuzi wa mizungu ya siasa, mbinu za utendaji, uelewa na upimaji kwenye viwango vya usemaji, ushauri au anapofanya shambulizi la kisiasa dhidi ya hasimu wake.

Niliposikia tetesi za kujiuzulu kwake kwa siku nzima ya jana nilikuwa nikitafakari bila kupata majibu ya haraka na kuona haikuwa wakati sahihi na muafaka sana kwa kiongozi huyo wa CCM kuachia ngazi na kujiweka kando.

Hata hivyo CCM ni chama kikongwe chenye hazina kubwa ya Wanasiasa hodari hivyo lolote linaweza kuwa ila muhimu ni kutega mingo na kusubiri wakati kwa kutega vyema masikio yetu.

*Shilatu E.J*

KIKAO CHA HALMASHAURI KUU CHATEUA MAJINA MAWILI.

$
0
0


Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) kinachoendelea kufanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa chama hicho, Dkt. John Pombe Magufuli kimepitisha majina mawili ya wajumbe wapya wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na NEC.

Wajumbe hao ni Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu nne Mizengo Peter Pinda pamoja na Makongoro Nyerere.

Kikao hicho pia kimepiga kura ya kuwapata wajumbe sita kwa kuzingatia jinsia, watatu kutoka Tanzania Bara na watatu kutoka Tanzania Zanzibar ambao watakuwa wajumbe wa Kamati Kuu, Jumla ya majina 18, tisa kutoka kila upande yalipendekezwa kuwania nafasi hizo.

Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne Mh. Mizengo Pinda na Makongoro Nyerere waliteuliwa na  Rais Dkt. Magufuli  hivi karibuni kabla siku ya leo Mei 28, 2018 kupitishwa rasmi.

LORIS KARIUS ATISHIWA MAISHA.

$
0
0

Polisi wa eneo la Merseyside, Uingereza wamesema wanafahamu kuhusu vitisho vya maisha ambavyo vimetolewa dhidi ya mlinda lango wa Liverpool Loris Karius baada ya kuchezwa kwa fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumamosi.

Maafisa wamesema vitisho vyovyote vinavyotolewa kupitia mitandao ya kijamii vinafaa kuchunguzwa kwani ni hatari kwa usalama kwa usalama kwani mashabiki wanamihemko na hasira ya kukosa ubingwa.

Karius, 24, na familia yake wamekuwa wakipokea vitisho baada ya makosa mawili kutoka kwake kuwasaidia Real Madrid kupata ushindi wa 3-1.

"Tunachukulia ujumbe huu wa vitisho kwenye mitandao ya kijamii kwa uzito sana. Visa hivi vitachunguzwa," polisi wamesema.

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp, ambaye bado hajashinda kikombe tangu ajiunge na Liverpool 2015 amesema anamuonea huruma sana karius.



SERIKALI YAANDAA UTARATIBU WA KUWATAMBUA WAZEE NCHINI.

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jaffo, akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Dodoma, akielekeza Mikoa kukusanya takwimu sahihi za Wazee (Picha na Atley Kuni- OR TAMISEMI)


Serikali yaandaa utaratibu wa Kuwatambua  Wazee nchini


Na. Atley Kuni na Mathew Kwembe, OR TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewaagiza Wakuu wa Mikoa kusimamia zoezi la kuwatambua wazee wote nchini katika mikoa yao na wahakikishe kuwa ifikapo tarehe 30 Juni, 2018 Mikoa yao inawasilisha Ofisi ya Rais TAMISEMI orodha ya wazee katika mikoa yao.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma leo, Mhe. Jafo alisema kuwa tayari amekwishatoa maagizo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI kuhakikisha kuwa zoezi hilo linashirikisha ngazi zote za Mamlaka ya Serikali za Mitaa.

Alisema ifikapo tarehe 15 juni 2018 anatarajia kuona kuwa zoezi hilo liwe limekamilika katika ngazi ya kata ambapo Mtendaji wa Kata atapaswa kuliwasilisha katika ngazi ya halmashauri kabla ya kufika ngazi ya Mkoa.

Pia alisema kuwa ifikapo tarehe 20 Juni, 2018 anatarajia kuwa zoezi hilo liwe limekamilika katika ngazi ya halmashauri ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri atapaswa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji katika ngazi ya mkoa tarehe 26 juni, 2018.

Waziri Jafo alieleza kuwa ifikapo tarehe 30 Juni, 2018 anatarajia kuwa ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa iwasilishe taarifa hiyo katika Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Akifafanua zaidi kuhusu umuhimu wa zoezi hilo Mhe.Jafo alisema kuwa serikali imeamua kuchukua hatua hiyo ya kuwatambua wazee wote nchini ili wasiendelee kupata manyanyaso kwa kukosa utambuzi rasmi.

Aliongeza kuwa wazee ni tunu ya taifa na hivyo hawana budi kuenziwa kwa serikali kuhakikisha kuwa wanatambuliwa na kupatiwa vitambulisho vitakavyowawezesha kupata huduma muhimu kama vile afya.

Kwa mujibu wa Waziri Jafo wazee wanaolengwa ni wale wa kuanzia miaka 60 ambapo inakadiriwa kuwa asilimia 75 ya wazee wote nchini wapo maeneo ya vijijini.

RC DKT. KEBWE ATAKA WANAFUNZI WOTE WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KUPATIWA CHAKULA MASHULENI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akifungua majengo ya shule ya Chagongwe wakati wa ziaya yake ya kukagua miradi ya maendeleo. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG-Gairo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akiwa na mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe  (wa pili kushoto) wakipiga picha ya ukumbusho mara baada ya kumaliza ufunguzi wa majengo ya shule ya sekondari Chagongwe.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Chagongwe waliojitokeza kumpokea wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya ya Gairo na vitongoji vyake.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akimsikiliza mmoja ya wazee waliojitolea eneo la shamba lake kwa ajili ya kujenga sekondari ya Chagongwe ambapo alitoa eneo la heka 25.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akipewa zawadi ya mbuzi na Diwani wa Kata ya Chagongwe mara baada ya kuwa amemaliza kuwahutubia wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akiwa na mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe (mwenye kilemba) wakionyeshwa eneo la shule ya Nongwe lililovamiwa na wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akikagua hosteli ya wanafunzi wa shule ya sekondari Nongwe.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akikagua vyoo vya hosteli ya wanafunzi wa shule ya sekondari Nongwe.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akiwa na mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe (mwenye kilemba) wakishiriki ngoma wakati wa mapokezi yao katika shule ya sekondari Nongwe.
Mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe (mwenye kilemba) akiwasalimia wananchi wa Kijiji Cha Nongwe waliohudhuria katika mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro mara baada ya kuwasili kijijini kukagua miradi ya maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akiwahutubia wananchi wa Kijijini Nongwe waliohudhuria katika mkutano wa hadhara.
Burudani ya ngoma ikiendelea.
Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe wakati wa ziara ya kukagua maendeleo katika wilaya ya Gairo. Hapa alikuwa akielekea Kata ya Kata ya Chagongwe.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe)  akiwa na mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe (mwenye kilemba) wakikagua ubovu wa barabara ya Chagongwe ambayo kwasasa imeharibika kutokana na mvua inayoendelea kunyesha maeneo mbali mbali.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akiwa na mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe wakikagua Daraja la Barabara ya Chagongwe-Kumbulu yenye urefu wa Km 34 lililojengwa na Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA).
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akiwa na mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe  (wa pili kulia) wakiongozwa na Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA), Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Mhandisi Simon Masala  (aliyenyoosha mkono) kukagua daraja la Chagongwe lililojengwa na TARURA.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akiwa na mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe  (wa katikati) wakipewa maelezo machache na Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA), Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Mhandisi Simon Masala  (aliyenyoosha mkono) kukagua daraja la Chagongwe lililojengwa na TARURA.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akiwa na mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe  (wa pili kulia) wakipewa maelezo machache na Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA), Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Mhandisi Simon Masala  (aliyenyoosha mkono) wakati wakikagua daraja la Chagongwe lililojengwa na TARURA. Pembeni ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Gairo, Agnes Mkandya (aliyejifunika shuka).
Msafara ukiondoka Darajani.
Mmoja ya wazazi akitoa elimu ya jinsia kwa wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari Chagongwe.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG-Gairo.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ameuagiza uongozi wa wilaya ya Gairo na mkoa wetu kwa ujumla kuhakikisha wanafunzi wa shule msingi mpaka sekondani wanapatiwa chakula mashuleni.

Kauli hiyo ameitoa wishoni mwa wiki iliyopita wakati akiwa katika Ufunguzi wa madarasa ya shule ya sekondari Chagongwe katika ziara yake kwa siku ya tatu Wilayani Gairo kukagua miradi ya maendeleo.

Ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Gairo kujiwekea mpango kazi ili kuwawezesha watoto wote kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari wanapatiwa chakula cha mchana na kuwawezesha waweze kufanya vizuri katika masomo yao.

"Watoto wa shule za Morogoro kutokula chakula mashuleni ni aibu, sitaki kabisa kusikia hili suala watoto kunyimwa chakula, naomba Mwenyekiti wa Halmashauri ya Gairo, upitishe azimio kwenye baraza na shule ambayo hawatatoa chakula shuleni wachukuliwe hatua uongozi wa eneo hilo," amesema Dkt. Kebwe.

"Mkoa wetu unaongozwa kwa uzalishaji wa chakula cha kutosha sasa inakuwaje watoto wetu tuwanyime chakula, tutakosa matokeo mazuri," amesema.



Aidha amesema kuwa mtoto anatakiwa kula chakula mara mbili ya mtu mzima, unapomnyima chakula hata ukuaji wake unakuwa hafifu... "Ubongo unatakiwa kupata chakula gram 6 za grucose<"

Amesema kuwa kukosekana kwa chakula shuleni kumekuwa kukichangia matokeo mabaya kwa wanafunzi bila kujali ni shule ya msingi au sekondari.

"Tatizo hili tulilizungumza wakati tunafanya tathimini ya mkoa juu ya kushuka kwa elimu na jambo lililojitokeza ni wakafunzi kutopewa chakula kunachangia matokea mabaya<" amesema.

Alisisitiza kuwa Halmashauri zote zisimamie suala la chakula shuleni ni lazima na wala siyo hiari naomba uongozi usimamie kwa msisistizo mkubwa, kuanzia walimu wakuu, wakuu wa shule atakula nao sahani moja na akiona ni waheshimiwa madiwani ndiyo hawahamasishi atabanana nao mpaka kieleweke.

"Mwaka juzi tulikuwa tunashika mkia nafasi ya 23 katika upande wa matokeo ya elimu, ila tokea tulipoanza kubanana vizuri matokeo yameonekana mpaka sasa tupo nafasi ya 11 kitaifa ni jambo linaloleta faraja sana, Kidato cha sita tunaongoza maana tupo nafasi ya pili kitaifa, sekondari tumesogea mpaka namba 14 kitaifa" amesema.

Ameongeza kuwa tamko lake hilo lisije kutafsiriwa vibaya kuwa tunawatoza michango ya hela, michango haipo kwa waraka namba 6 umefafanua elimu bila malipo, tatizo lenu wengine wanasema  elimu bure, hakuna elimu ya bure ni elimu bila malipo kwa mzazi ila serikali ndiyo inagharamia.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe amemshukuru Mkuu hiyo kwa kutenga muda wake na kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo na kumhaidi kufanyia kazi changamoto na maelekezo yote aliyoyatoa.

"Mkuu wa Mkoa tunakushukuru sana kwa kuweza kufika eneo letu na kuona changamoto tulizo nazo tunahidi kuzifanyia kazi na tunakuomba ufikishe salamu zetu pia kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kuikumbuka wilaya yetu kwa kutupa hela za maendeleo,"

Mhe. Siriel amewaomba vingozi wa wilaya ya Gairo kuendeleza upendo na mshikamano walionao ili kuendelea kuwatumikia wananchi vyema.


JAMII YATAMBUA UMUHIMU WA MWANAMKE KUMILIKI ARDHI.

$
0
0
Wananchi wa Kijiji cha Mawala, Wilaya ya Kilolo Iringa, wakisaidia kutekeleza baadhi ya shughuli za mpango wa matumzi ya ardhi ya kijiji chao.
Bahati Mwinyimvua mwananchi toka kijiji cha Melela Wilaya ya Mvomero Morogoro. Akichangia hoja kuhusiana na umiliki wa ardhi kwa wanawake
Ng’eng’enu Mambega katibu wa kamati ya maamuzi kijiji cha Mela, wilaya ya Mvomero Morogoro akibainisha jinsi elimu ya umiliki wa ardhi kwa wanawake ulivyosaidia kuwabadili kifikra na kuwapa wenza wao maeneo wayamiliki. 
Angolile Rayson Afisa mradi toka Shirika la PELUM Tanzania akichangia mada kuhusiana na mpango wa matumzi ya ardhi.



Jamii kwa sasa imeanza kutambua na kuthamini haki za mwanamke kwenye masuala ya umiliki wa ardhi na hivyo kumpa nafasi zaidi kisheria kupata, kumiliki, kutumia na kugawa ardhi kama ambavyo imekuwa ikifanyika kwa wanaume. 

Kuwepo kwa mabadiliko haya chanya kwa baadhi ya jamii imetokana na kusambaa kwa elimu ambayo imekuwa ikitolewa na Shirika la PELUM Tanzania kupitia mradi wa Ushiriki wa wananchi katika kusimamia sekta ya kilimo unaofadhiliwa na watu wa marekani. 

Angolile Rayson ambaye ni Afisa Mradi amesema vijiji vyote 30 vya mradi ambavyo 27 kati yake toka wilaya sita za Morogoro, Mvomero, Kilolo, Mufundi, Bahi na Kongwa vimefanyiwa mpango wa matumizi ya ardhi, wananachi wake walikuwa wakiendeleza mila na tamaduni potofu za kuona kuwa mwanamke si sehemu ya familia hivyo hapaswi kumiliki ardhi kwani ataolewa na kwenda kuendeleza ukoo mwingine. 

Lakini baada ya kufanya mafunzo kwenye vijiji hivyo juu ya haki za mwanamke kumiliki ardhi, jamii imebadilika na sasa mwanamke si tu amekuwa akimilikishwa ardhi peke yake bali pia ana maamuzi nayo kisheria kuitumia kwa shughuli zozote za kiuchumi, kukodisha na hata akiamua kuiuza. 

“Tunashukuru baada ya kutoa elimu juu ya haki za mwanamke kumiliki ardhi wakati wa kutekeleza mpango wa matumizi ya ardhi, wanaume wengi wamewapa wenza wao maeneo wamiliki kwa majina yao wenyewe na wengine wamemiliki umiliki wa pamoja yaani mke na mume na zaidi ya yote hata watoto wa kike kwenye baadhi ya familia wamepewa maeneo na wazazi wao wamiliki. Shirika kupitia Hamlashauri za wilaya husika tumewapimia maeneo yao na kwa sasa wanasubiri hatimiliki za kimila ili wawe na umiliki halali jambo ambalo sisi kama Shirika tumeona ni sehemu kubwa ya mafanikio.” Alifafanua Angolile 

Wakielezea wakati wa kufanyika tathimini ya mradi wananchi wa kijiji cha Ikuka Wilaya ya Kilolo, Iringa walibainisha kuwa katika kijiji chao hapakuwa na mazingira mazuri hasa upande wa wanawake na watoto wa kike wanapoomba kupewa ama kurithishwa ardhi kilichokuwa kinafuata ni muhusika kufariki katika mazingira tatanishi hali iliyowafanya wahusishe suala hilo na imani za kiushirikina 

Kutokana na hali hiyo, wanawake iliwapasa kutokuzungumzia neno ardhi midomoni mwao. Ila baada ya kupata elimu, kwa sasa wanawake wamepimiwa vipande vya ardhi walivyopewa na wenza wao ikiwemo wengine kuwa na umiliki wa pamoja wa mume na mke. 

“Tunashukuru Shirika la PELUM Tanzania kwa kutupa mafunzo ya haki za ardhi ambayo yamekuwa msaada na hasa kwa wanawake kwani kupitia elimu hii tumefahamu haki zetu kama wanawake kuwa na sisi tunapaswa kumiliki ardhi na kuwa na maamuzi nayo kisheria. Kwenye kijiji chetu kwa sasa wapo wanawake wamepima ardhi zao mmoja mmoja na wengine wanatarajia kuwa na umiliki wa mume na mke kama mimi na sasa tunasubiri ugawaji wa hatimiliki.”Bahati Mwinyimvua Mwananchi kijiji cha Melela Wilaya ya Mvomero, Morogoro. 

Ng’eng’enu Mambega yeye ni katibu kamati ya maamuzi kijiji cha Mela, wilaya ya Mvomero Morogoro anasema baada ya kupata elimu ya masuala ya ardhi kwa sasa si tu wamewapa maeneo wenza wao wayamiliki ambao yameshapimwa kupitia mradi ila pia wanawashirikisha mambo mbalimbali wenza wao na kuwaruhusu kufanya maamuzi jambo ambalo halikuwa likifanyika kweye tamaduni za kimasai. 

“ Zamani tulikuwa tunawathamini na kuwarithisha watoto wa kiume ardhi hata kama mzee kafariki kijana ndio anakuwa mwenye sauti lakini kwa sasa mambo yamebadiliki mama naye ana haki zake kwenye eneo la mume wake na vijana wa kike pia tumewapa maeneo wayamiliki wenyewe.” Alifafanua Mambega 

Kwa upande wake Zaveria Mdendemi toka kijiji cha Makungu, Wilaya ya Mufindi Iringa anasema, kutokana na mila potofu kuwa mwanaume ama mtoto wa kiume pekee ndio anapaswa kumiliki ardhi, jambo lilimletea mgogoro na mtoto wake wa kwanza wa kiume ambaye alitaka kumpokonywa mali zote ikiwemo ardhi aliyoachiwa na marehemu mume wake lakini kupitia elimu aliyoipata, alimpeleka kwa mwenyekiti wa kijiji akaeleimishwa na hatimaye akamuachia mama yake mali zote akisubiri maamuzi ya mama juu ya mali hizo. 

“Nashukuru mradi huu kutoa kipamumbe kwa wajane kupimiwa maeneo yao, kwani mila na desturi ambazo tumezikuta mwanamke amekuwa akinyimwa nafasi kumiliki mali yoyote na hasa sisi wajane pindi mume anapofariki tumekuwa tukifukuzwa kwenye nyumba tulizojenga na wenza wetu na kupokonywa mali zote wakati mwingine hadi watoto ama uachiwe watoto bila mali yoyote. Lakini kwa sasa elimu imewezesha jamii kutambua thamani ya mwanamke kumiliki ardhi na hivyo tumefanikiwa kupimiwa maeneo yaliyobaki mikononi mwetu”. Rosemary Ulanga mwananchi kijiji cha Ibugule, wilya ya Bahi Dododma. 

Kupitia upimaji huo wa ardhi kwenye vijiji 27, Shirika la PELUM Tanzania linatarajia kutoa hatimiliki za kimila zipatazo 4000 kwa makundi ya wazee, wajane, wagane, watu wenye ulemavu na wa kipato cha chini

SERIKALI INAMTIHANI MWINGINE HUU:- YATAKIWA KUSAMBAZA BURE PEDI MASHULENI.

$
0
0
Wanafunzi mkoani Mwanza wakiwa kwenye maandamano ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Hedhi Duniani 2018. Maandamano ya wanafunzi yalianzia eneo la Mission na kupokelewa katika uwanja wa Furahisha. Mkurugenzi wa shirika la Tanzania Youth With New Hope in Life Organization (TAYONEHO), Dr.Imani Tinda akizungumza kwenye maadhimisho hayo. Mgeni rasmi, Muuguzi Mkuu mkoani Mwanza Agness Hassan akizungumza kwenye maadhimisho hayo kwa niaba ya Mganga Mkuu mkoani Mwanza. Maadhimisho ya Siku ya Hedhi Duniani 2018 yamefanyika kitaifa mkoani Dodoma, kama ilivyokuwa mwaka jana wakati yanaanza kuadhimishwa hapa nchini. Meneja wa shirika la Plan International mkoani Mwanza, Baraka Mgohamwende akiwasilisha salamu zake kwenye maadhimisho hayo. Upendo Abisai ambaye ni mwakilishi wa mradi wa Youth For Change unaotekelezwa na shirika la Plan International, akitoa salamu zake kwenye maadhimisho hayo. Elizabeth Mbokela (katikati), ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi Nyegezi akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi wa kike mkoani Mwanza. 
Pia shirika la Plan International limetumia maadhimisho hayo kutoa pedi kwa wanafunzi wa kike ili kuwasaidia kujisitiri wakati wa hedhi. Wanafunzi kutoka shule mbalimbali mkoani Mwanza wakiwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Hedhi Duniani, ngazi ya mkoa. Wanafunzi kutoka shule za msingi mkoani Mwanza wakiwa kwenye maadhimisho hayo yaliyofanyika katika uwanja wa Furahisha. Wanafunzi wakionyesha igizo namna ukosefu wa elimu kuhusu hedhi unavyoweza kuwanyima mabinti uhuru wa kujiamini na kushindwa kuhudhuria masomo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa shirika la TAYONEHO FDr.Imani Tinda, Muuguzi mkuu mkoani Mwanza Agness Hassan pamoja na Meneja Mradi (Boresha Elimu) kutoka shirika la TAYONEHO James Edward wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye maadhimisho hayo.Tazama video hapa chini. 
  ISOME PIA HABARI HII Mwanza kuadhimisha Siku ya Hedhi Duniani 2018

Tanzania leo imeungana na mataifa mengine kuadhimisha Siku ya Hedhi Duniani ambapo kwa mkoa wa Mwanza maadhimisho hayo yamefanyika katika uwanja wa Furahisha.
Akisoma risala ya wanafunzi wa kike mkoani Mwanza, Elizabeth Mbokela ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi Nyegezi amesema ni vyema serikali ikatenga bajeti kwa ajili ya kutoa bure taulo (pedi) kwa wanafunzi wa kike hatua itakayowasaidia kuondokana na changamoto ya kukosa masomo kutokana na hedhi.
Dr.Imani Tinda ambaye ni Mkurugenzi wa shirika la TAYONEHO lililoratibu maadhimisho hayo kwa kushirikiana na Plan Internationa,  amesema wanafunzi wa kike wamekuwa wakipoteza vipindi vya masomo kutokana na suala la hedhi ambapo kawaida mwanafunzi anapaswa kuhudhuria darasani siku 194 sawa na vipindi 1,740 lakini kutokana na hedhi wanafunzi wa kike huudhuria siku 84 sawa na vipindi 756.
Akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu Mkoa Mwanza, Muuguzi Mkuu mkoani Mwanza Agness Hassan ametoa rai kwa kamati za shule kuhakikisha zinashiriki ipasavyo kuboresha mazingira ya wanafunzi wa kike hususani kutenga chumba maalumu kwa ajili ya kujisitiri wakati wa hedhi.
Maadhimisho ya Siku ya Hedhi Duniani hufanyika kila mwaka Mei 28 ambapo mwaka huu ni mara ya pili Tanzania kuadhimisha maadhimisho hayo tangu kuasisiwa na Umoja wa Mataifa UN mwaka 2014.
Mwaka huu kitaifa kaulimbiu ni “kila siku inaweza kuwa siku siku nzuri hata kama ni siku ya hedhi” huku kimataifa ikiwa ni “hakuna tena mipaka” kauli zote zikilenga kuhamasisha jamii kutakuwa kwamba hedhi ni suala la kawaida lisilopaswa kuleta vikwazo vya aina yoyote kwa wasichana na wanawake.

MBAO 1-1 RUVU MCHEZO WA MWISHO LIGI KUU VODACOM TZ BARA

$
0
0


GSENGOtV
Mbao FC imetoka sare ya 1-1 na Ruvu Shooting Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza. (Cheki video kwa muhtasari ikiwemo goli la kusawazisha la Mbao Fc)

MATOKEO MENGINE.
SIMBA SC imefanikiwa kumaliza msimu kwa kupoteza mechi moja tu, baada ya sare ya 1-1 na wenyeji Maji Maji FC Uwanja wa Maji Maji mjini Songea. 

Hiyo inakuwa sare ya tisa ya msimu, mechi nyingine Simba SC ikishinda 20 na kufungwa moja tu na Kagera Sugar mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli wiki iliyopita Uwanja wa Taifa. 


Maji Maji FC leo walitangulia kwa bao la mshambuliaji Marcel Boniventusa Kaheza kabla ya kiungo kutoka Rwanda, Haruna Niyonzima kusawazisha kwa penalti.


Niyonzima aliyesajiliwa msimu huu kutoka kwa mahasimu wa jadi, Yanga alipoteza nafasi ya kuifungia bao la ushindi Simba baada ya mkwaju wake wa penalti kupanguliwa na kipa Hashim Mussa kipindi cha pili.


Ndanda FC imeshinda 3-1 dhidi ya Stand United Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara na kunusurika kushuka daraja.

Kagera Sugar imepata ushindi wa 2-1 mbele ya wenyeji, Lipuli FC ya Iringa Uwanja wa Samora, Tanzania Prisons imeilaza 1-0 Singida United Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, Mtibwa Sugar imetoka sare ya 0-0 na Mbeya City Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro, Mwadui FC imewapiga wenyeji, Njombe Mji FC 2-0 Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe.


Kwa matokeo hayo, Simba SC inamaliza msimu na pointi 69 baada ya mechi zake 30, wakati Azam FC yenye pointi 55 za mechi 29 wapo nafasi ya pili mbele ya mabingwa wa msimu uliopita, Yanga SC wenye pointi 52 za mechi 29.

Mechi kati ya Yanga na Azam FC inatarajiwa kufanyika kuanzia Saa 2:00 usiku wa leo Uwanja wa Taifa na ndiyo itakuwa ya kuamua mshindi wa pili wa msimu huu. Azam wanataka sare tu kumaliza nafasi ya pili, lakini Yanga wanahitaji ushindi ili kumaliza nyuma ya Simba wakibebwa na wastani wao mzuri wa mabao na pia kwa sababu walishinda mechi ya kwanza Chamazi.   


Maji Maji na Njombe Mji FC ziimeshuka Daraja kutokana na tayari African Lyon, KMC, JKT Tanzania za Dar es Salaam, Coastal Union ya Tanga, Alliance Schools ya Mwanza na Biashara United ya Mara zimekwishapanda kuelekea ligi ya msimu ujao, itakayokuwa na timu 20 ambayo ni ongezeko la timu nne.

BUIBUI-MTU APEWA URAIA UFARANSA KWA KUMUOKOA MTOTO ASIANGUKE GHOROFANI

$
0
0
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ametoa amri ya kupewa uraia Mamoudou Gassama mhamiaji kutoka Mali ambaye ameonesha ushujaa mkubwa wa kukwea kwa umahiri wa kipekee dari za nyumba za jengo kubwa la ghorofa na kumuokoa mtoto aliyekuwa anakaribia kuanguka.
Mwanamme huyo kutoka Mali anaendelea kupongezwa kote nchini Ufaransa kwa ushujaa wake huo na ameshapewa uraia kwa amri ya Rais Emmanuel Macron.

Macron ametangaza kuwa, Mamoudou Gassama mhamiaji anayeishi nchini Ufaransa kinyume cha sheria, kuanzia sasa atakuwa raia wa kawaida wa Ufaransa na atajiunga na kikosi cha Zima Moto.
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa akizungumza na Mamoudou Gassama

Kundi kubwa la watu waliokuwa wamekusanyika kusubiri kuona hatima ya mtoto huyo aliyekuwa ananing'inia ghorofani na kuweko uwezekano wa kuanguka wakati wowote, walichukua filamu za video zinazomuonesha Gassama akikwea ghorofa za jingo hilo kama buibui hadi alipomfikia mtoto huyo na kumuokoa na kifo.

Majirani waliokuwa wanajaribu kumfikia mtoto huyo walishindwa kumuokoa. Baada wa Gassama kumfikia mtoto huyo na kumuokoa, kundi la watu lililokuwa limekusanyika chini ya jingo hilo lilipiga mayowe makubwa ya furaha na kumpongeza 'buibui-mtu' huyo.

LIVE - WABUNGE WAKIAGA MWILI WA ALIYEKUWA MBUNGE WA BUYUNGU, MWL KASUKU BILAGO

$
0
0


GSENGOtV
Shughuli hii ya kutoa heshima za mwili inafanyika muda huu katika viwanja vya Bunge, Dodoma. Mara baada ya shughuli hii, mwili huo utasafirishwa kwenda Kigoma kwa maziko. Marehemu Kasuku Bilago alifariki dunia Jumamosi Mei 26, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Viewing all 12408 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>