Quantcast
Channel: g sengo
Viewing all 12413 articles
Browse latest View live

BAADA YA KUJIZATITI MWANZA YALAMBA SHAVU KUANDAA MAONESHO YA UTALII.


MWANZO MWISHO WALIVYOACHIWA WAFUNGWA GEREZA LA BUTIMBA MWANZA KWA MSAMAHA WA RAIS MAGUFULI

BAADA YA SUNGUSUNGU KUSISIMUA MAADHIMISHO YA UHURU 2019 RAIS MAGUFULI AWAZAWADIWA NG'OMBE 10

HIFADHI YA TAIFA KUPEWA KIPAUMBELE,SHUGHULI NYINGINE KUSITISHWA.

$
0
0
Kamishna wa hifadhi tanapa dactar ALLAN  KIJAZI  amesema kuwa wadau mbalimbali hapa nchini wanatakiwa kuona namna  bora wanaweza  kusimamia hifadhi  mpya ya TAIFA  YA NYERERE kwani ni  hifadhi muhimu KITAIFA ambayo ilikuwa ni sehemu ya pori la akiba lililipo chini ya mamlaka ya  usimamizi wa wanyama pori TAWA ambapo ilitangazwa rasmi na raisi  DK, JOHN  POMBE MAGUFURI baada ya bunge la jamuhuli ya muungano wa TANZANIA  kuridhia azimio kupandishwa hadhi hifadhi hiyo.

RAIS MAGUFULI ATANGAZA KUACHIWA KWA NDEGE YA TANZANIA ILIYOKAMATWA CANADA

$
0
0

Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400 iliyokuwa imakamatwa nchini Canada imeachiwa na wananchi watatangaziwa siku ya kuwasili ili waipokee jijini Mwanza.
 
Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa amesema hayo wakati anafungua Semina ya Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Inayofanyika Jijini Mwanza.

“Kwa taarifa tu, Ndege yetu iliyokuwa imeshikiliwa Canada imeachiwa, mtatangaziwa siku ya kuipokea na itapokelewa hapa Mwanza,” amesema.


WAISLAMU MKOA WA MWANZA WAUNGANA NA SHEIKH MKUU VITA DHIDI YA MUZIKI MOTO

$
0
0

BAADA ya Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi kutangaza kupiga marufuku dufu na kaswida maarufu kama ”mziki moto” akizitaja kuwa, zinaaibisha na kuchafua sura ya Uislamu huku zikitoka nje ya utamaduni na maadili ya dini tukufu ya Kiislamu.Mkoani Mwanza Sheikh wa Mkoa huo, Hassan Kabeke naye ameapa kupambana na hilo ili kuhakikisha maadili ya Uislamu yanalindwa.

JEH WAJUA KITENGE KILICHOVALIWA MWANZA 9 DISEMBA 2019 NDICHO KILICHOVALIWA SHEREHE ZA UHURU 1961?

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA KITUO CHA AFYA UKARA

$
0
0


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Suluhu Hassan, akiweka Shada la Maua kwenye Mnara wa kumbukumbu  Eneo waklipoozikwa Wahanga wa Ajali ya Kivuko cha MV Nyerere Kisiwani  Ukara Wilayani Ukerewe  Disemba 14,2019 wakati malipotembekea Eneo hilo.
Picha ya Wananchi wa Ukara Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Suluhu Hassan, akikata utepe kuweka Jiwe la Uzinduzi wa Majengo mapya ya Kituo cha Afya  Bwisya Ukara Ukerewe  Disemba 14,2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Suluhu Hassan, akimpa pole Mtoto Femia Sabato (3)mkazi wa Bwisya Ukara aliyelazwa katika  Kituo cha Afya  Bwisya Ukara kwa matibabu mara baada  kuzinduzi wa Majengo mapya ya Kituo cha Afya  Bwisya Ukara Wilayani Ukerewe  Disemba 14,2019. kushoto ni Bibi wa Mtoto huyo Silimagi Manyeji.
Picha ya Wananchi wa Ukara Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza.  
Msanii wa Kikundi cha Sanaa cha Ngoma ya Matoigaa Charoo cha Ukara Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza Goabth Bwere akionesha Umahiri  wake katika uwanja wa Bwisye Ukara wakati wa Hafla ya  kuweka Jiwe la Uzinduzi wa Majengo mapya ya Kituo cha Afya  Bwisya Ukara Ukerewe Disemba 14,2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Suluhu Hassan, akihutubia Wananchi wa wa Bwisye Ukara Wilayani Ukerewe baada ya kuweka Jiwe la Uzinduzi wa Majengo mapya ya Kituo cha Afya  Bwisya Ukara Ukerewe Disemba 14,2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela alipowasili Uwanja wa ndege wa Mwanza  akitokea Kisiwani ukara wilayani Ukerewe  Baada ya kuweka Jiwe la Uzinduzi wa Majengo mapya ya Kituo cha Afya  Bwisya Ukara Ukerewe Disemba 14,2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Suluhu Hassan, katikati akiwa katika picha ya pamoja na Msanii wa Kikundi cha Sanaa cha Ngoma ya Matoigaa Charoo cha Ukara Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza Goabth Bwere katika uwanja wa Bwisye Baada ya Makamu wa Rais  kuweka Jiwe la Uzinduzi wa Majengo mapya ya Kituo cha Afya  Bwisya Ukara Ukerewe Disemba 14,2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Suluhu Hassan, katikati akiwa katika picha ya pamoja na Msanii wa Kikundi cha Sanaa cha Ngoma ya Matoigaa Charoo cha Ukara Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza Goabth Bwere katika uwanja wa Bwisye Baada ya Makamu wa Rais  kuweka Jiwe la Uzinduzi wa Majengo mapya ya Kituo cha Afya  Bwisya Ukara Ukerewe Disemba 14,2019.
Picha ya Wananchi wa Ukara Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza.

MBUNGE TWEVE NA KOMBA WAIPA HESHIMA TANZANIA

$
0
0
Mbunge Rose Tweve akishangiliwa na wabunge wenzake 
Mbunge Rose Tweve  na Yosepher Komba kulia wakijiandaa kwa kuanza riadha 
Mbunge Rose Tweve kulia akiwakimbiza wakenya 
Wabunge wanaume wanamichezo toka Tanzania wakimshangilia mbunge Tweve
 Wabunge wanawake Rose Tweve na Yosepher Komba wameendelea kuing'aza nyota ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuibuka na medali za dhahabu katika mbio za mita Mia moja (100m) na mita elfu moja na Mia tano (1500m).

Wakati Rose Tweve kutoka Mkoa wa Iringa akiwaburuza wabunge wa nchi za Kenya, Uganda, Burundi na wale wa Bunge la Afrika Mashariki EALA,  Yosepher Komba kutoka Viti Maalum Mkoa wa Tanga aliwagaragaza wapinzani wake katika mbio za mita 1500.

Wabunge Hao Vijana sasa mwaka wa Pili mfululizo wanaendelea kuipeperusha vema Bendera ya Tanzania katika mchezo wa riadha Naendelea wanatarajia kuendelea tena hapo jumapili katika mbio za kupokezana Vijiji.

Kwa upande mwengine mwanamama Anatropia Teonest alimaliza nafasi ya Pili katika mbio za mita 400, huku wanaume kupokezana Vijiji Tanzania ilishika nafasi ya tatu.

Michezo hiyo inaendelea Kesho katika mchezo wa Wavu wanaume na wanawake wakati Bunge la Tanzania watajitupa uwanjani kuvaana na Bunge la Afrika Mashariki

PICHA ZA MAPOLOMOKO YA LIYOSABABISHWA NA MLIPUKO WA ARDHI NA MUA YA UPEPO MKALI RORYA

$
0
0
MBUNGE wa Jimbo la Wilaya ya Rorya Mkoa wa Mara, Lameck Airo (CCM) akipewa maelezo na Emmanuel Odworu mmoja wa athirika wa mapolomoko yaliyosababishwa mlipuko na mvua ya upepo mkali katika Kitongoji cha Sang'ombe Kijiji cha Tatwe Kata ya Goribe Wilaya ya Rorya Mkoa wa Mara.
MBUNGE wa Jimbo la Wilaya ya Rorya Mkoa wa Mara, Lameck Airo (CCM) akipewa maelezo na wananchi wathiriwa na mapolomoko ya urefu wa km 2 yaliyosababishwa mlipuko na mvua ya upepo mkali iliyoharibu ekari 20 za mashamba ya mazao mchanganyiko katika Kitongoji cha Sang'ombe Kijiji cha Tatwe Kata ya Goribe Wilaya ya Rorya Mkoa wa Mara.
MBUNGE wa Jimbo la Wilaya ya Rorya Mkoa wa Mara, Lameck Airo (CCM) akipewa maelezo na Emmanuel Odworu mmoja wa athirika wa mapolomoko yaliyosababishwa mlipuko na mvua ya upepo mkali katika Kitongoji cha Sang'ombe Kijiji cha Tatwe Kata ya Goribe Wilaya ya Rorya Mkoa wa Mara.
Sehemu ya mashamba yaliyoharibiwa ekari 20 kusombwa vibaya na mapolomoko ya mawe na aedhi zaidi ya km 2 yaliyosababishwa na mlipuko na mvua ya upepo mkali katika Kitongoji cha Sang'ombe Kijiji cha Tatwe Kata ya Goribe Wilaya ya Rorya Mkoa wa Mara. 
MBUNGE wa Jimbo la Wilaya ya Rorya Mkoa wa Mara, Lameck Airo (CCM) akipewa maelezo na wananchi wathiriwa na mapolomoko ya urefu wa km 2 yaliyosababishwa mlipuko na mvua ya upepo mkali iliyoharibu ekari 20 za mashamba ya mazao mchanganyiko katika Kitongoji cha Sang'ombe Kijiji cha Tatwe Kata ya Goribe Wilaya ya Rorya Mkoa wa Mara.
MBUNGE wa Jimbo la Wilaya ya Rorya Mkoa wa Mara, Lameck Airo (CCM) akikabidhi kiasi cha Sh milioni 2.3 Kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Tatwe Julius Ochwachi ili kusaidia waathiriwa wa Kaya kumi kufatia mapolomoko ya mawe na aedhi zaidi ya km 2 yaliyosababishwa na mlipuko na mvua ya upepo mkali katika Kitongoji cha Sang'ombe Kijiji cha Tatwe Kata ya Goribe Wilaya ya Rorya Mkoa wa Mara. 
 Sehemu ya mashamba yaliyoharibiwa ekari 20 kusombwa vibaya na mapolomoko ya mawe na aedhi zaidi ya km 2 yaliyosababishwa na mlipuko na mvua ya upepo mkali katika Kitongoji cha Sang'ombe Kijiji cha Tatwe Kata ya Goribe Wilaya ya Rorya Mkoa wa Mara
PICHA ZOTE NA PETER FABIAN.

Na MWANDISHI WETU RORYA MKOA WA MARA.


MVUA ya upepo mkali yasababisha mlipuko na mapolomoko ya mawe na mmomonyoko mkubwa wa ardhi yaliyotokea Kitongoji cha Sang'ombe Kijiji cha Tatwe Kata ya Goribe Wilayani Rorya Mkubwa wa Mara yaliyosababishwa na mvua kubwa ya iliyoambatana na upepo mkali umesababisha watu 93 kuathiriwa huku kaya kumi zikiathirika zaidi.

Mbunge wa Jimbo la Rorya Lameck Airo (CCM) alitembelea eneo hilo akiambatana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rorya, Charles Ochele na viongozi wengine wa Kata na Vijiji jirani kufika katika eneo la tukio kujionea uhalibifu mkubwa wa ardhi uliopelekea mto na bonde kubwa huku za zaidi ekari 20 za mazao ya wananchi kusombwa na maji na kuharibiwa na mamia ya mawe yaliyoporomoka yenye urefu wa km 2 kutoka eneo la tukio hadi mto Chirya.

Airo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Tatwe alitoa pole kwa wananchi na kusikitisha na tukio hilo ambalo limeacha maswali mengi na kuwashitua wananchi zaidi 93 kuharibiwa mazao katika mashamba yao yenye urefu wa ekari 20 huku kaya kumi zikipata athari kubwa ikiwemo kupata nyufa kutoka na mlipuko huo.

"Tukio hili limetokea majira ya saa 11:00 jioni Desemba 12 na limeacha janga na hali ya wasiwasi baada ya kupolomoka wa shehena kubwa ya mawe na mmomonyoka mkubwa wa ardhi amapo eneo hilo limekuwa na mto mkubwa ambao unatililisha maji hadi mto Chirya haya ni maajabu lakini tushukuru hayakulenga makazi ya wananchi tungeshuhudia mamia kupoteza maisha," alisema.

Airo aliwaeleza wananchi hao kusikitishwa na tangu kutokea kwa tukio hilo ambapo Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Saimon Chacha na Kamati ya Ulinzi na Usalama na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kushindwa kufika katika eneo la tukio na kujionea athari kubwa ya mapolomoko na uharibifu wa ardhi na mazao ya wananchi kusombwa na kufunikwa na mchanga jamb ambalo amesikitishwa na kuwaomba wananchi kuwa watulivu kwa kipindi hiki ambacho tukisubilia utaratibu wa serikali baada ya kufika kujionea eneo hilo.

"Nimepokea taarifa za tukio hili kwa mshituko na nilimtaalifu Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ochele na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara Samwel Kiboye ambapo hapa nimekuja na viongozi hawa wa Wilaya wa Chama na tunatoa pole ya Sh milioni 2.3 kwa Kaya tatu zilizoathiriwa na kujihifadhi kwa na jirani huku kaya saba ambazo jumla yake kuzifanya kuwa Kaya kumi kuanza kupata huduma za chakula na malazi wakati tukisubiri wataalamu wa Halmashauri kufanya tathimini ya athari ya tukio hili,

Akikabidhi kiasi cha fedha hizo kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Tatwe, Julius Ochwachi, Mbunge Airo alifafanua kuwa yeye binafsi ametoa kiasi cha Sh milioni moja, Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo, Ochele ametoa Sh 300,000/- na Mdau wa maendeleo kutoka Wilaya hiyo aliyefahamika kwa jina Orwero aliyechangia Sh milioni moja pia.

Wakizungumzia katika eneo la tukio hilo baadhi ya wathirika wa tukio hilo, Kevin Chacha, Emmanuel Odworu, Rosemary Joseph walieleza kwa nyakati tofauti kuwa siku hiyo ilianza mvua majira ya saa 5:00 asubuhi ikanyesha kisha ikakata badae majira saa 11:00 jioni ikarejea mvua kubwa na kisha kusikika mliyo wa mlipuko mkubwa na kusikika kishindo cha mapolomoko ya maji, mawe na mchanga huku mvua ikiambatana na upepo mkali.

" Mvua hii iliwahi kutokea miaka 1996 lakini haikuwa na madhala kama hii leo tumeshuhudia maafa na mazao kusombwa na mawe na mchanga na tumeshuhudia nyumba mbili zikianguka na ng'ommbe wawili wakisombwa ni jambo ambalo limetuweka katika wasiwasi mkubwa na kuhofia maisha yetu hivyo tunaomba wataalam waje kufanya utafiti kutambua kilichotokea ama kilichosababisha, Alisema Rosemary Joseph

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rorya, Ochele alisema kwamba tukio hilo limewapa funzo na kuwa Wilaya hiyo ina viongozi wa Serikali wa aina gani kwa kushindwa kufika kujionea athari na uharibifu kwa wakati jambo ambalo watalikemea na kulisema kwa wahusika na kama Chama hawakufurahishwa na hali hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Tatwe, Julius Ochwachi aliwashukuru Mbunge Airo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Ochele kwa kufika na kutembelea eneo la tukio huku wakiguswa na kutoa msaada kwa waathirika kumi waliopoteza nyumba na mifugo yao huku wananchi wengine 83 wakiwa wameshuhudiwa wakipoteza mazao ya mahindi, mtama, ulezi, mihogo, viazi vitamu, mpunga na maharage katika maeneo mashamba yao zaidi ya ekari 20 huku mapolomoko hayo yakiwa na urefu wa km 2 kutoka eneo la tukio hadi mto Chirya.

ALICHOKIFANYA BARAKA MAGUFULI MBELE YA RAIS MAGUFULI IMEBAKI HISTORIA

$
0
0


Ni yule mkali wa kuigiza sauti ya Mhe. Rais .....safari hii kakutana naye uso kwa uso kwenye uzinduzi wa ndege mpya uliofanyika Airport jijini Mwanza

KITUO CHA AFYA BWISYA UKEREWE SASA KUFIKIRIWA KUWA HOSPITALI.

$
0
0

Hii ni ziara ya kwanza ya kufanywa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kisiwa cha Ukara Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza. Ambapo awali baada ya Makamu wa Rais kuhani eneo la makaburi ilimolala miili ya baadhi marehemu kati ya mamia waliofariki kwenye ajali ya Meli ya MV Nyerere iliyotokea Septemba 19 mwaka 2018, na kuweka shada la maua pia aliweka Jiwe la Uzinduzi wa Majengo mapya ya Kituo cha Afya Bwisya Ukara.

KAMISHNA WA OPERESHENI NA MAFUNZO YA JESHI LA POLISI, CP LIBERATUS SABAS, AMEFUNGA MAFUNZO YA ASKARI WA KIKOSI MAALUM CHA ULINZI MPAKA WA TANZANIA NA MSUMBIJI PAMOJA NA ULINZI WA AMANI KIMATAIFA KILELEPORI NA WEST KILIMANJARO.

$
0
0

 Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi, CP Liberatus Sabas akisalimiana na wakufunzi wa askari wa Kikosi Maalum kitakachosimamia Ulinzi wa Amani katika Mpaka wa Tanzania na Msumbiji huko mkoani Mtwara katika Mto Ruvuma ambapo kumekuwa kukitokea mauaji ya mara kwa mara kwa raia wema yaliosababishwa na wahalifu kutoka Nchini jirani ya Msumbiji. (Picha na Jeshi la Polisi)
 Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi, CP Liberatus Sabas akiongea na askari  wanaohitimu mafunzo ya usimamizi wa Ulinzi katika Mpaka wa Tanzania na Msumbiji yaliofanyika katika pori la West Kilimanjaro mkoani Kilimanjaro.(Picha na Jeshi la Polisi)
 Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi, CP Liberatus Sabas akimkabidhi cheti cha ukufunzi bora Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP William Mwampagale wakati akifunga mafunzo ya askari wa Ulinzi wa Amani Kimataifa Kilelepori mkoani Kilimanjaro.(Picha na Jeshi la Polisi)
 Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi, CP Liberatus Sabas wa tatu kutoka kushoto kwa waliokaa akiwa katika picha ya pamoja Maafisa wa Jeshi la Polisi, wakufunzi wa ndani pamoja na wakufunzi wa umoja wa kimataifa baada ya kufunga mafunzo Kilelepori mkoani kilimanjaro. (Picha na Jeshi la Polisi)
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la polisi, CP Liberatus Sabas akisalimiana na wakufunzi wa Askari wa Kikosi Maalum kinachotarajiwa kujiunga na vikosi vingine vya Ulinzi wa Amani Kimataifa kwaajili ya kusimamia amani katika nchi au mataifa yenye migogoro. (Picha na Jeshi la Polisi)

EH BAN Eeee... MWANZA KUSHEREHEKEA CHRISTMAS HAPA.

$
0
0

Kama ikatokea uko ndani ya Jiji la Mwanza Christmas hii ya 2019 basi hili ndilo eneo la kujimwaga na kujiachia ukila 'KITU BILI KWA JIWE MOJA'

MAGUFULI AIBUA SHANGWE KRISMAS/ WAFANYAKAZI WAMTAKA WAZIRI MPINA KUFUNGA NATI UVUVI HARAMU

$
0
0

WAFANYAKAZI wa kiwanda cha kuchakata mabondo cha HONGLIN INTERNATIONAL TRADE DEVELOPMENT cha jijini Mwanza wamepaza sauti zao na kuishukuru Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli kwa namna ilivyopambana na Uvuvi Haramu na kuwezesha kupatikana malighafi za kutosha zilizowezesha kupatikana kwa ajira ya uhakika viwandani.

Wameitaka Serikali kuendelea kufunga nati ili kuwabana wavuvi haramu ili rasilimali za uvuvi ziongezeke mara dufu na kuwezesha viwanda zaidi kwani sasa ajira zimeongezeka kutokana na ongezeko la samaki.

Waziri wa mifugu na uvuvi, Luhaga Mpina amewahakikishia kuwa Serikali iko imara na itaendelea kulinda rasilimali hizo ili ziweze kutumika kwa manufaa ya Watanzania wote.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA

$
0
0

KATIKA KUELEKEA SIKUKUU ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA.

 JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA  KWA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VINGINE VYA ULINZI  NA USALAMA LIMEJIPANGA VYEMA  KUHAKIKISHA SIKUKUU ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA ZINASHEHEREKEWA KWA AMANI NA UTULIVU. HIVYO TUWATOE HOFU WANANCHI NA WAGENI WATAKAOTEMBELEA MKOA WETU KWAMBA ULINZI UMEIMARISHWA  WA WAO NA MALI ZAO.

AIDHA TUTAHAKIKISHA NYUMBA ZOTE ZA IBADA, KUMBI ZA STAREHE NA MAENEO MENGINE  ULINZI UNAIMARISHWA VYA KUTOSHA KWANI ASKARI WATAKUWA KATIKA DORIA ZA MIGUU, PIKIPIKI, MBWA NA MAGARI KATIKA MAENEO YOTE YA JIJI NA  MKOA WA MWANZA, HIVYO WANANCHI WASIWE NA HOFU YOYOTE  PINDI WATAKAPOKUWA KWENYE IBADA AU BURUDANI MBALIMBALI. PIA TUWATAKE WANANCHI WANAPOKWENDA KATIKA MIKESHA YA SIKUKUU HIZI WASIACHE  NYUMBA ZAO BILA UANGALIZI  AU KIZIACHA WAZI KWANI KUNAWEZA KUSHAWISHI WEZI.

PIA TUWAKUMBUSHE WAZAZI NA WALEZI KUWA PAMOJA NA KUSHEREKEA SIKUKUU HIZI WASISAHAU MAJUKUMU YAO YA KUWA MAKINI NA WATOTO WAO KWA KUTOWAACHA PEKE YAO BARABARANI NA KATIKA SEHEMU ZA MICHEZO MFANO MAENEO YA BEACH/MIALO, DISKO TOTO NA KWENYE BEMBEA. PIA NI MARUFUKU KWA MAREVA  WA VYOMBO VYA MOTO KUENDESHA WAKIWA WAMELEWA AU MWENDO KASI, ENDAPO IKIBAINIKA HATUA STAHIKI  ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAO. HATA HIVYO KWA WALE WENYE TABIA YA KUCHOMA MATAIRI BARABARANI WAACHE KWANI NI KOSA KISHERIA.

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWATAKIA WANANCHI WOTE WA MKOA WA MWANZA NA WATANZANIA KWA UJUMLA SIKUKUU NJEMA YA KRISMASI NA MWAKA MPYA. LAKINI PIA KUSHEHEREKEA SIKUKUU HIZO KWA AMANI NA UTULIVU.

IMETOLEWA NA;
Muliro J. MULIRO- ACP
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.
24 DESEMBA, 2019.

Ben Pol - Sikukuu (Official Music Video)

$
0
0

Ben Pol perfoming Sikukuu (Christmas) which was originally performed by George Kinyonga & Orchestra Jobiso. Enjoy! Video Directed by : Adam Juma (Tanzania)

VIDEO MPYA TOKA KWA MZUNGU KICHAA.

$
0
0
Baada ya kimya cha muda mrefu, Mzungu Kichaa amerudi na singo mpya.  You Got Me ni wimbo ya mapenzi inayogusia hitaji la kupendwa kwa kila mwanadamu.

Mashairi na upigaji stadi wa gitaa na bass kutoka kwa Mzungu kichaa vimebeba wimbo. You Got Me ni nyimbo ya kwanza kutoka kwenye album mpya ya Mzungu Kichaa inayoitwa “Huyu nani” itakayotoka mapema mwaka 2020.

We don’t have time (hatuna muda) / To take it slow (kuwa watulivu) / Cos the future (sababu kesho yetu) / We will never know (hatuijui)
Be open (uwe muwazi) / Be free (uwe huru) / Take a chance (itumie nafasi hii) /Jump on to the other side with me (ruka upande wa pili pamoja nami)

Khalid Kumbuka aka KK, ni kaka mdogo wa Adili mmoja wa waasisi wa kundi la kwanza la Hipihop Tanzania Kwanza Unit, ambaye alifariki katika ajali mbaya ya gari Dar es salaam mwaka 1992. Mzungu kichaa alipokuja Tanzania katikati ya miaka ya 90 mama yao Margarethe Kumbuka ndiye alimfundisha Kiswahili katika shule ya sekondari Dar es Salaam. Baada ya kuhamia London kusoma Chuo kikuu na mama Margarethe alihamishiwa chuo hicho hicho kufundisha Kiswahili na wote wakafanya masters pamoja. Baadae Mzungu kichaa alipogundua kipaji cha Khalid Kumbuka kwenye uandishi na kutumbuiza, ilikuwa rahisi kumualika studio na kufanya kazi pamoja.

Magitaa mawili yamechanganywa kwenye kiitikio na kutoa hisia ya kipee kutokana na upigaji wa gitaa wa Mzungu kichaa. Aina ya sauti ambayo amekuwa akiitengeneza tangu siku za awali kwenye Bongo Flava ambapo mtiririko wake wa gitaa ulisikika kwenye She Gatta Gwan wa Mangwaire na Mambo ya Pwani ya Solo Thang. Kwenye You Got Me, P Funk Majani alimjaribu Mzungu Kichaa kupiga gitaa la Bass na kuongezea ubunifu wake kwenye kuzalisha maadhi ya Trap hi-hat na kiki nzuri na snare. Pasipo shaka hii ni kazi bora iliyotokana na uzoefu wa muda mrefu.

CREDITS
Track: You Got Me
Featuring: KK, Grace Matata
Produced by: Mzungu Kichaa and P Funk Majani
Recorded at: Caravan Records and Bongo Records
Mixed by: P Funk Majani
Mastered by: Jacob Brondlund
Record Label: Caravan Records
Video Director: Jessica Maria Olsen
Video Editor: Carlo Kamin
Video Grading: Justin Campos

KAMA UNATAKA KUFUGA NYATI MAJI 'MILANGO IKO WAZI NJOO UCHUKUWE MBEGU SERIKALINI'

$
0
0


Shamba la Mifugo la Mabuki lililopo wilayani Misungwi mkoani Mwanza lilianzishwa mnamo mwaka 1966 baada ya Uhuru wa Tanganyika kwa ajili ya kuzalisha F1, hii ilikuja baada ya kugundua kuwa wafugaji wachache waliopewa ng’ombe wa kisasa kutoka Ulaya, wengi wao walishindwa kuwamudu wakafa ndipo wataalamu wa Mifugo waliokuwepo enzi hizo wakaona ni vyema kuzalisha ng’ombe wa maziwa wanaoweza kuhimili mazingira ya nyanda za nchi zenye joto ikiwemo Tanzania.

Shuhudia ziara ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina akizuru Shamba hilo la Mabuki kama sehemu ya mwendelezo wa Agenda ya Kitaifa ya Utafiti wa Mifugo, Uvuvi na Ukuzaji viumbe kwenye maji 2020 – 2025 ambapo pia amepata fursa ya kuwaona Nyati Maji wanaofugwa kituoni hapo, mbegu iliyoingizwa nchini enzi za utawala wa Rais wa Kwanza nchini Hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere.Kwa wale wanaotaka kufuga Nyati hao, kitambo sana Serikali ilishafungua milango.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina.
Pia shamba la Mifugo la mabuki linafuga Mbuzi wa maziwa (hawapo pichani) aina ya Toggenburg wenye uwezo wa kutoa kati ya lita moja na nusu kwa mkamuo mmoja yaani lita 3 kwa siku, kiwango kinachozidi uwezo wa ngombe wa kienyeji anayekamuliwa lita 1 kwa mkamuo na lita 2 kwa siku.


Ng'ombe hasa madume yananunuliwa kwa wingi sana na wafugaji kwaajili ya mbegu.

 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina akipata maelekezo toka kwa Meneja Msaidizi wa Shamba la mifugo la Mabuki ambaye pia ni Afisa Mifugo Daraja la Kwanza Pascal Godwin Bahemu (mwenye kofia).
Shamba la Mifugo la Mabuki lililopo wilayani Misungwi mkoani Mwanza, lina ukubwa wa Hekta 9,773, ambapo mpaka hivi sasa shamba linauwezo wa kuzalisha ng'ombe 580 kwa mwaka yaani wastani wa 320 majike na 260 madume.


TAFITI ZA AWALI.Kwa tafiti za URT za Mwaka 2015, Tanzania inashika nafasi ya pili kwa wingi wa mifugo barani Afrika ikiwa na ng'ombe milioni 25, mbuzi milioni 16.7, kondoo milioni 8, nguruwe milioni 2.4, na kuku milioni 36. Kati ya ng'ombe milioni 25 ng'ombe wa asili ni 98%. Hivyo, ni 2% tu ya ng'ombe wote Tanzania wanaofugwa kwa mfumo wa ufugaji wa kisasa. Tafiti hizo zinaonesha kuwa ufugaji wa asili unachangia 7.4% ya pato la Taifa na ongezeko la ukuaji la 2.2% kila mwaka. Ufugaji wa asili umethibitika kiuchumi kuwa na ufanisi mkubwa katika matumizi ya ardhi na uhifadhi wa mazingira. Ufugaji wa asili unategemewa na idadi kubwa ya Watanzania kwa kuendesha maisha yao; iwe kwa chakula, mavazi, na maendeleo kwa mapana yake. Mchango wake katika uchumi rasmi na usio rasmi (informal and formal economies) ni dhahiri hasa kupitia kodi na tozo mbalimbali katika masoko ya mifugo, usafirishaji wa mifugo, ukaguzi wa mifugo, na upatikanaji wa malighafi kwa matumizi ya viwanda mbalimbali.

WANAFUNZI WATALII KISIWA CHA SAANANE.

$
0
0
Mwongoza watalii qa Hifadhi ya Saanane Michael Pascal kuwapa maelezo wanafunzi na walimu wa Kilimani Sekondari walipotembelea hifadhi hiyo. 
Walimu wa Shule ya Kilimani  Sekondari  wakiwa wamevalia maboya kujiokolea kabla ya kupanda boti kuekelea Hifadhi ya Saanane jana.


 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kilimani wakiwa wameruka juu ya mwamba eneo la Jumping Stone katika Hifadhi ya Saanane jana.
 Mkurugenzi wa kampuni ya URSINO Ltd Mnandi Mrutu Mnandi  (kulia) pamoja na Mkuu wa Shule ya Sekondari Kilimani wakionyesha umakini wa kuruka juu kwenye mwamba wa Jumping Stone katika Hifadhi ya Saanane. 
 Mwongoza watalii katika Hifadhi ya Saanane Michael Pascal akiwapa maelezo Wanafunzi na walimu wa Kilimani Sekondari ikiwemo Mkurugenzi wa kampuni ya URSINO Ltd Mnandi Mrutu Mnandi, kushoto mwenye kofia walipotembelea hifadhi hiyo jana.
 Mkurugenzi wa kampuni ya URSINO Ltd Mnandi Mrutu Mnandi (mwenye kofia) akizungumza jambo wakati wa ziara ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kilimani kutembelea Hifadhi ya Saanane jana .Mnandi ndiyo aliyefadhili ziara hiyo.
Mkurugenzi wa kampuni ya URSINO Ltd,Mnandi Mrutu Mnandi wa nne kutoka kulia akishiriki pamoja na wanafunzi wa Shule ya Kilimani Sekondari, kuruka juu ya mwamba (Jumping Stone) katika Hifadhi ya Saanane. Wa tatu kutoka kulia ni Mkuu wa Shule hiyo Gerana Majaliwa.
 Mkurugenzi wa kampuni ya URSINO Ltd, Mnandi Mrutu Mnandi aliyeketi kuahoto,Mkuu wa Shule ya Sekondari Kilimani Gerana Majaliwa  (kulia) walimu pamoja na wanafunzi wa shule hiyo wakimsikiliza mwongoza watalii qa Hifadhi ya Saanane, Michael Pascal ,aliyesimama.
Boti za Hifadhi ya Saanane zikiwa zimewabeba wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kilimani kwenda kutembelea Hifadhi ya Saanane jana  kwa ufadhili wa Mkurugenzi wa kampuni ya URSINO Ltd Mnandi Mrutu Mnandi.  Picha zote na Baltazar Mashaka 
Viewing all 12413 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>