$ 0 0 JESHI la Polisi Mkoani Iringa, linawashikilia Vijana wawili wakazi wa Kijiji cha Mazombe, Mkoani humo, kwa tuhuma za kukutwa na ‘kidole cha binadamu’ kutokana na Imani za kishirikina.Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani humo, Wankyo Nyigesa, amesema kuwa tukio hilo limetokea Februari 1,mwaka huu majira ya saa (11:15) asubuhi ambapo raia wema walio waona Vijana hao walifanikiwa kutoa taarifa mapema kwa Jeshi hilo na baadae kutiwa mbaroni,Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Gibson Kasenegala (29) na Benson Mlasu (23) wote wakazi wa kijiji hicho, kitendo ambacho kimewatia hofu wakazi wa eneo hilo.Hata hivyo alisema wakiwa pamoja walikuwa wakimiliki kidole hicho ambacho hakijulikani kuwa ni cha nani, kutokana na Imani za kishirikina kwamba kinaweza kuwasaidia kupata mali.“Tumewatia mbaroni na Uchunguzi wetu bado unaendelea ili tujue nani alikatwa Kidole, au kama kuna mtu aliuawa kisha kidole chake kikachukuliwa,” alisema Nyigesa.Alisema watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani, baada ya uchunguzi wa tukio hilo kukamilika na kuwataka Wananchi wa Mkoa huo na maeneo mengine kuachana na Imani za kishirikiana ambazo zinaathiri nguvu kazi ya familia zilizo nyingi.CHANZO: PRINCE MEDIA TZ.