Wilfred Warioba, alisema ili kurahisisha mawasiliano ya tume hiyo na wananchi, Tume imeamua kuanzisha teknolojia hiyo ya kutuma malalamiko moja kwa moja kupitia mitandao ya simu zao kwa njia ya ujumbe mfupi yaani ‘sms’.
Aliongeza kuwa tume ya haki za binadamu na utawala bora ni chombo huru ambacho kiko kwa ajili ya kutetea wananchi wote na hakitozi gharama yoyote ya kuwasilisha malalamiko.
Mtaalamu huyo aliongeza kuwa tume inapokea malalamiko ya aina yoyote ile bila kujali yameletwa na nani ili mradi yawe na ukweli ndani yake, kinachotakiwa ni mhusika kuandika malalamiko yake kwenye sehemu ya kuandika ujumbe mfupi kwenye simu yake ya mkononi na kisha kuutuma kwenye namba 0754 460 256.
Ujumbe huo ukishapokelewa mhusika (mlalamikaji) atapigiwa simu na kuulizwa baadhi ya mambo ili kujua kiini cha malalamiko yake kwa lengo la kujiridhisha ikiwa ni pamoja na kufahamu anaitwa nani, yuko wapi na mambo mengine yatakayoturahisishia kushughulikia malalamiko yake kwa wepesi zaidi, aliongeza.
Aidha Warioba alisema mwananchi yeyote atakayeleta malalamiko yake kwa ‘sms’ anatakiwa kutumia majina yake halisi na kutaja mahali alipo na si kusema uongo lengo likiwa kurahisisha kazi ya kushughulikia malalamiko yake.
Alifafanua kuwa tume hii haina upendeleo wowote wa kijinsia katika kushughulikia malalamiko ya wananchi yanayopokelewa huku akibainisha kuwa wananchi walio wengi bado hawajajua wajibu wao kwani wanayo matatizo mengi ila wanayanyamazia tu ndio maana tumewatembelea ili waseme waziwazi.
Tume ya uwasilishaji wa malalamiko kwa njia ya 'SMS' imeanzishwa mnamo mwezi Julai 2001 hapa nchini ikiwa imelenga kulinda na kutetea maslahi ya wananchi ambapo imejiwekea utaratibu wa kupokea na kushughulikia malalamiko mbalimbali ya wananchi kuanzia ngazi ya serikali kuu mpaka ngazi ya vijiji. ‘Mpaka sasa tume hiyo ina ofisi katika kanda 4 tu ambazo ni Lindi, Mwanza, DSM na Zanziba, lengo letu ni kuelimisha umma ili wafahamu wajibu wao ni nini, haki zao ni zipi, wanawezaje kuzipata na kwa utaratibu gani’, aliongeza Shayo.
Aliongeza kuwa tume ya haki za binadamu na utawala bora ni chombo huru ambacho kiko kwa ajili ya kutetea wananchi wote na hakitozi gharama yoyote ya kuwasilisha malalamiko.
Mtaalamu huyo aliongeza kuwa tume inapokea malalamiko ya aina yoyote ile bila kujali yameletwa na nani ili mradi yawe na ukweli ndani yake, kinachotakiwa ni mhusika kuandika malalamiko yake kwenye sehemu ya kuandika ujumbe mfupi kwenye simu yake ya mkononi na kisha kuutuma kwenye namba 0754 460 256.
Ujumbe huo ukishapokelewa mhusika (mlalamikaji) atapigiwa simu na kuulizwa baadhi ya mambo ili kujua kiini cha malalamiko yake kwa lengo la kujiridhisha ikiwa ni pamoja na kufahamu anaitwa nani, yuko wapi na mambo mengine yatakayoturahisishia kushughulikia malalamiko yake kwa wepesi zaidi, aliongeza.
Aidha Warioba alisema mwananchi yeyote atakayeleta malalamiko yake kwa ‘sms’ anatakiwa kutumia majina yake halisi na kutaja mahali alipo na si kusema uongo lengo likiwa kurahisisha kazi ya kushughulikia malalamiko yake.
Alifafanua kuwa tume hii haina upendeleo wowote wa kijinsia katika kushughulikia malalamiko ya wananchi yanayopokelewa huku akibainisha kuwa wananchi walio wengi bado hawajajua wajibu wao kwani wanayo matatizo mengi ila wanayanyamazia tu ndio maana tumewatembelea ili waseme waziwazi.
![]() |
Ndani ya semina na washiriki toka asasi mbalimbali za kiraia. |
![]() |
Kwa umakiiiini hii ni sehemu ya washiriki wa semina hiyo. |
![]() |
Washiriki. |
![]() |
Semina ikiendelea. |
![]() |
Picha ya pamoja wadau wa Tume na wadau wa asasi mbalimbali za kiraia jijini Mwanza. |