Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa pili wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, ambaye ni Mtanzania, Said Omary Said, wakati wa hafla ya hitimisho la mashindano hayo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, leo Julai 20, 2014. Wa pili kushoto ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi. |