NA. ALBERT G.SENGO: MWANZA
Bado vitendo vya baadhi ya timu za Polisi kutumia ubabe kupata matokeo kwenye mchezo hapa nchini hususani Ligi soka daraja la kwanza Tanzania Bara vimeendelea kutawala na kuwa sugu.
Hilo limeonekana kwenye mchezo uliofanyika leo (jumapili) baina ya Toto Africans na Polisi Dodoma uliovunjika katika dakika ya 70, Toto wakiongoza kwa bao 1-0, ikiwa ni mara baada ya baadhi ya wachezaji wa Polisi Dom na viongozi benchi la ufundi kumdunda refa na kamisaa wa mchezo huo. (SIKILIZA TAARIFA YA SPORTS XTRA HUKU UKISUBIRI PICHA AMBAZO ZITAWAJIA HIVI PUNDE)