Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries leo imetoa zawadi ya Limo Bajaji kwa Bw. Mfaume Hassan Lwembe (43) ambaye ni dereva taxi na mkazi wa Mbagala katika kampeni yake inayoendelea ya “Tutoke na Serengeti”. Hii imetangazwa leo katika droo inayofanyika kila wiki makao makuu ya SBL yaliyopo Chang’ombe jijini Dar es Salaam chini ya usimamizi wa PWC na bodi ya michezo ya bahati nasibu Tanzania.
“Ninafuraha sana kusikia habari hizi, Asante sana Serengeti” alisema Bw. Mfaume mara baada ya kupewa taarifa za kuibuka mshindi wa Limo Bajaj kwenye promosheni ya Tutoke na Serengeti. Aliendelea kusema kwamba...“Hatimaye sasa nimepata kitu ambacho kitanisaidia kuinua hali ya maisha yangu”.
Alipoulizwa njinsi alivyoshiriki kwenye promosheni hiyo, Mfaume alieleza kwamba … “Baada ya kazi, huwa napendelea kupumzika sehemu na rafiki zangu huku tukipata vinywaji. Tangu promosheni hii ianze, nimekuwa nikinunua Serengeti Premium Lager na mara kwa mara nimekuwa nikituma namba zilizo chini ya kizibo kwenda 15317 kwa njia ya ujumbe mfupi. Ninamshukuru Mungu siku ya leo juhudi zangu zimezaa matunda leo”.
Mfaume aliipongeza SBL kwa kuwa kampuni ya kwanza kuanzisha promosheni ya aina hii hapa nchini, na kuuthibitishia umma kuwa promosheni hii ni halali kabisa na hakuna uchakachuaji katika kumpata mshindi.
Akiongea na vyombo vya habari, Meneja chapa bia ya Serengeti Premium Lager Bwana. Eli Huruma Ngowi alisema “kutokana na uhitaji na muitikio mzuri kutoka kwa wateja wetu kwenye kampeni hii”, SBL imeongeza mwezi mmoja wa promosheni ili kutoa fursa kwa wateja wengi zaidi kujishindia zawadi mbalimbali zilizoorodheshwa hapo awali….Kwa mantiki hiyo basi kampeni hii itafika kikomo mwisho wa mwezi Februari tofauti na ilivyotarajiwa mwanzo kuwa ingeisha mwezi Januari.
Eli Huruma aliendelea kusema kwamba “Hadi sasa zaidi ya shilingi milioni 700 tayari zimeshatumika katika kuwazawadia washindi mbalimbali ambapo kati yao watu (5) wameshinda Limo Bajaj na (2) wameshinda ziara ya kutembelea hifadhi ya taifa ya Serengeti national park huku wateja wengi zaidi wamejishindia fedha taslim Tsh 100,000 zinazotelewa kila wiki baada ya droo.
“SBL pamoja na BPESA wanajivunia kwamba promosheni hii imebadilisha maisha ya watu wengi kwa kiasi kikubwa ” alimalizia Eli Huruma.
Kwa upande mwingine, taarifa kutoka ofisi za BPESA, wataalam wa teknolojia ambao katika promosheni hii wanahusika na usambazaji wa fedha kwa njia ya simu kwa washindi kutoka pande mbalimbali hapa nchini, wamethibitisha kuwa watamkabidhi Bw. Mfaume Bajaj yake wiki ijayo.
Ili kushiriki kwenye promosheni hii, mteja anatakiwa awe na umri wa zaidi ya miaka 18, anunue Serengeti Premium Lager na kuangalia chini ya kizibo ambapo atakuta namba ambazo anatakiwa kuzituma kwenda katika mamba 15317. Kadiri mteja anavyoshiriki, ndivyo anavyojiweka katika nafasi ya kushinda.