WINGU jeusi limeendelea kutanda baada ya moto mkubwa kuendelea kuwaka mitaa ya External karibu na kanisa la Mzee waupako.
Ili kupunguza msongamano polisi wamelazimika kutumia baruti kutawanya watu na inasemekana kuwa hadi sasa frem zaidi ya saba za biashara zimeharibiwa na moto huo.
Chanzo cha moto huo kinasemekana kuwa ni nguzo mbovu ya umeme iliyo karibu na eneo hilo ambayo imekuwa kero kwa wananchi baada ya kuripoti Tanesco mara kwa mara bila mafanikio.
Moto huo ulianza kuwaka eneo la makusanyiko ya machupa chakavu za plastiki.
Gari tatu za Zimamoto zimeonekana eneo la tukio ila maji yamekuwa kikwazo kwenye zoezi hilo.
CHANZO/TBN