NA ALBERT G. SENGO: MWANZA
Timu ya soka ya Tanzania Taifa Stars tayari imewasili jijini Mwanza kwa mchezo wake wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya Malawi.
Stars imetinga jijini humo ikiwa na wachezaji 18 tu ambapo wengine sita toka Yanga Africans wamebaki jijini Dar es salaam wakisubiri kumalizia mchezo wa kiporo wa Ligi kuu soka Tanzania Bara dhidi ya JKT Ruvu utakao chezwa Jumatano.
Deogratius Munish, Nadir Haroub, Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Hassan Dilunga na Simon Msuva watajiunga na wenzao walioko jijini Mwanza siku ya Alhamisi. (TAARIFA KWA NJIA YA SAUTI KUWAJIA HIVI PUNDE)