Katibu tawala jiji la Arusha Ado Mapunda (RAS) akipiga mpira kuashiria ufunguzi rasmi wa mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars jijini Arusha jana. |
Katibu tawala jiji la Arusha Ado Mapunda (RAS) akiongea na wachezaji katika ufunguzi wa mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars jijini Arusha jana. |
Katibu tawala Jiji la Arusha Ado Mapunda (RAS) akikagua timu katika ufunguzi wa mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars jijini Arusha jana. |
KATIBU tawala afungua Airtel Rising Stars Arusha Katibu tawala mkoa wa Arusha Ado Mapunda jana alizindua mashindano ya kuibua vipaji vya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars jijini Arusha na kuwataka vijana wanaoshiriki mashindano hayo kujituma na kucheza kwa bidii ili kutimiza ndoto zao za kuwa wachezaji nyota.
Hafla ya ufunguzi ilihudhuliwa na viongozi wa shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) mkoa wa Arusha, mdhamini wa mashindano Airtel Tanzania na wadau wengine wa soka. Ufunguzi huo uliufanyika katika uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
“Tumepewa nafasi ya kuwa washiriki katika mashindano haya ya Airtel Rising Stars 2015.
Hivyo inatupasa tudhihirishe kuwa mkoa wetu una vipaji na tunaweza kuchangia katika maendeleo ya soka kwa kutoa wachezaji kwenye timu za vijana za taifa”, alisema Mapunda Arusha inashirikisha timu ya wasichana ambapo timu kombaini kutoka mkoa huo itasafiri kuelekea Dar-es-Salaam mwezi ujao kushiriki mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa.
Timu nyingine kwa upande wa wasichana ni Ilala, Temeke, Kinondoni, Mbeya na Mwanza. “Naamini vijana hawa wanaoibuliwa katika Airtel Rising Stars kila mwaka wanahitajika sana katika kuongoza nchi yetu kufika mbali katika Mafanikio”, alisema Mapunda na kuwapongeza Airtel katika kuwekeza katika maendeleo ya Mpira.
Programu hii ya soka la vijana ilianzishwa nchini Tanzania na sehemu nyingine barani Afrika mnamo mwaka 2011 na ime0nyesha kwa vitendo na imekua chombo muhimu katika maendeleo ya soka hasa katika soka la wasichana. Timu ya Taifa ya wasichana inaundwa na wachezaji kutoka Airtel Rising Stars. Alisema katika soka wachezaji wanaweza kujitengezea vyanzo vya ajira.
“ Soka imewapa ajira mamilioni ya wachezaji na viongozi ulimwenguni na wameweza kuishi maisha ya kifahari kutokana na mishahara wanayopata”, alisema na kuwataka wasichana kuwa na malengo ya mbali.
Akiongea katika ufunguzi huo Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde aliwashukuru viongozi wa shirikisho la mpira wa miguu TFFA) na chama cha soka mkoa wa Arusha kwa muda wao na ushirikiano wao katika mashindano. “ Pia natoa shukrani zangu za dhati kwa mgini rasmi kuja kuungana nasi katika uzinduzi huu.
Matinde amewataka wasichana kufanya vizuri na wayatumia mashindano ya Airtel Rising Stars kufanikisha ndoto zao kupitia soka.
Mechi ya ufunguzi iliwakutanisha Chriss FC na Future Stars ambapo mechi ilikwenda sare ya bila kufungana.