Quantcast
Channel: g sengo
Viewing all articles
Browse latest Browse all 12428

MWILI WA LETICIA NYERERE KUWASILI MUDA WOWOTE.

$
0
0
Aliyewahi kuwa mbunge wa Viti Maalumu wa
Aliyewahi kuwa mbunge wa Viti Maalumu CHADEMA, Marehemu Leticia Nyerere 
CHANZO: GAZETI LA MWANANCHI 
By Suzan Mwillo, Mwananchi
Dar es Salaam. Utaratibu wa kuusafirisha mwili wa aliyewahi kuwa mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema, Leticia Nyerere kutoka Marekani kuja Tanzania unaendelea kufanywa na familia yake.
Kwa mujibu wa wanafamilia ya Mwalimu Julius Nyerere, mwili huo unatarajiwa kuwasili nchini baada ya utaratibu wote kukamilika huko Marekani.
Shemeji wa marehemu, Makongoro Nyerere jana alisema maziko ya Leticia yatafanyika Butiama mkoani Mara.
“Shughuli ya kusafirisha mwili kutoka nchi moja kwenda nyingine ina hatua ndefu. Siyo haraka kama tunavyodhani,” alisema Makongoro.
Awali, akizungumza na vyombo vya habari Dar es Salaam, msemaji wa familia hiyo, Joseph Butiku alisema utaratibu ukikamilika watatoa taarifa ya lini atazikwa.      

Viewing all articles
Browse latest Browse all 12428

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>