Quantcast
Channel: g sengo
Viewing all articles
Browse latest Browse all 12433

MZEE WA MIAKA 60 AGONGWA NA DALADALA MBILI KATIKA ENEO LA MABATINI NA KUFA.

$
0
0
Pichani wananchi wakiuangalia mwili wa marehemu Mzee mmoja ambaye anatajwa kwa jina la Mihayo Ngofa aliyefariki dunia papo hapo juzi (jumamosi) majira ya saa 3 usiku baada ya kugongwa na magari mawili ya abiria (daladala) wakati akivuka barabara katika eneo la Kokoto Mabatini.
 Marehemu Mihayo Ngofa anaye kadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 65 hadi 70 aligongwa na daladala ya kwanza iliyokuwa ikitokea mjini kati kuelekea Igoma na kisha kugongwa na daladala nyingine ambapo zote zilikuwa zikipishana kwa wakati mmoja nyingine ikitokea Igoma kuelekea mjini kati. 

Mara baada ya tukio hilo daladala hizo hazikusimama ziliunganisha safari zake kwa mwendo wa kasi bila kufahamika zilipoishia.

Vielelezo vinaonyesha kuwa marehemu alikuwa akitoka sokoni kuinunulia mboga familia yake.

Tukio hili linatokea wakati Wakandarasi wa wa ujenzi wa daraja la kivuko kipya cha juu cha watembea kwa miguu kikiwa katika hatua zake za mwisho kukamilika na kuanza kutumika.
 PICHA NA ZEPHANIA MANDIA
WA G.SENGO BLOG.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 12433

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>