Quantcast
Channel: g sengo
Viewing all articles
Browse latest Browse all 12422

WANNE WAUAWA MKOANI MWANZA KWA TUHUMA ZA WIZI WA NG'OMBE

$
0
0

WATUwanne wameuawa mkoani Mwanza kwa tuhuma za wizi wa ng’ombe Katika eneo la Igwambiti kata ya Buhongwa Wilaya ya Nyamagana.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Valentino Mlowola amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya  saa 11 alfajiri ambapo wananchi walipata taarifa ya kuwepo kwa  wizi wa ng’ombe katika kitongoji cha Mtende.
 Aidha, kamanda Mlowola amewataja waliofariki kuwa ni pamoja na  Ezekiel Lucas (27), Kusekwa Lucas (25), Masumbuko Kisinza (30) na Mafisi Mwita (26) ambao walishambuliwa na wananchi kwa  silaha za jadi kinyume cha sheria.
Hata hivyo, amesema tayari Jeshi la Polisi linawashikilia watu watatu kwa kukutwa  na silaha mbalimbali ambazo zimesadikiwa kutumika katika tukio hilo ,huku  uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea. BOFYA PLAY HAPO JUU KUMSIKILIZA KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 12422

Trending Articles