↧
MKURUGENZI WA MAJI MUSOMA ATUMBULIWA.
↧
DIAMOND PLATNUMZ : RWANDA NI NYUMBANI KWETU PIA ( Exclusive Interview ) RTV
Naseeb Abdul Juma, popularly known by his stage name Diamond Platnumz, is a Tanzanian bongo flava recording artist and dancer from Tanzania.
↧
↧
NAIBU WAZIRI WA MADINI MHE BITEKO AWATAKA WACHIMBAJI WADOGO KUTAMBUA UMUHIMU WA KULIPA KODI
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza jambo wakati wa mkutano na wachimbaji wa madini ya Jasi na Chumvi Mkoani Mtwara, Leo 19 Januari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Wachimbaji wa madini ya Jasi na Chumvi Mkoani Mtwara wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati wa Mkutano wa pamoja na wachimbaji hao kwenye ofisi za Madini Kanda ya kusini, Leo 19 Januari 2018.
Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo Kanda ya kusini Ndg Peter Ludovick akieleza kero za wachimbaji mbele ya Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati wa mkutano na wachimbaji wadogo, Leo 19 Januyari 2018.
Na Mathias Canal, Mtwara
Wizara ya Madini imesisitiza wachimbaji wadogo na wakubwa nchini kutambua umuhimu wa ulipaji kodi kwa kila wanachozalisha kwani itasaidia kuongeza pato la Taifa kwa kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi ikiwemo ukarabati wa miundombinu, Ujenzi na uimarishaji Wa sekta ya afya, elimu, Sekta ya umeme na sekta ya maji.
Akizungumza Mkoani Mtwara wakati wa mkutano na wachimbaji wa madini ya Jasi na Chumvi Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko amesema kuwa jamii bado haina elimu ya kutosha juu ya ulipaji kodi hivyo ofisi za madini nchini zinapaswa kuongeza msukumo Wa utoaji elimu juu ya ulipaji kodi na utunzaji wa kumbukumbuku za shughuli za uvunaji Madini kwa kila mahali kwenye leseni.
Mhe Biteko alisema kuwa wachimbaji wadogo kote nchini wanapaswa kutambua kuwa hawatakiwi kusalia kukwepa kodi badala yake wanapaswa kutoka kwenye uchuuzi na hatimaye kuhamia kwenye ufanyabiashara na kuhifadhi taarifa zote kwa mujibu wa kanuni kwa kipindi cha miaka 5.
Alisema kuwa mtu yeyote anapoitwa mfanyabiashara anatambulika katika jamii na serikali kwa ujumla wake hivyo kigezo kikubwa na muhimu kwa mfanyabiashara ni kulipa kodi kwa mujibu Wa kanuni, sheria na taratibu.
Akizungumza kwa msisitizo Mhe Biteko alisema kuwa watanzania wamempata Mhe Dkt John Pombe Magufuli kuongoza Taifa akiwa Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania katika kipindi cha miaka mitano hivyo wanapaswa kuunga mkono juhudi za utendaji wake kwa kulipa kodi kwa manufaa ya jamii nzima.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Wa Madini ameupongeza uongozi Wa Ofisi ya Madini Kanda ya Mtwara kwa ushirikiano mzuri na wachimbaji jambo ambalo limeimarisha utendaji wao pasina malalamiko dhidi ya serikali.
Kwa upande wake Mwenyekiti Wa Chama Cha wachimbaji Mkoa Wa Mtwara Ndg Festo Balegele akizungumza wakati Wa mkutano huo alimsihi Naibu Waziri wa Madini kutilia mkazo uongezaji thamani wa chumvi inayozalishwa nchini kwa kuikausha (Drying) na kuisaga (Grinding) sambamba na kuongeza Madini joto kwani itapelekea serikali kuokoa fedha nyingi za kigeni zinazotumiwa na serikali kuagiza chumvi nje ya nchi.
Alisema kuwa kila mwaka jumla ya tani 350 za chumvi huagizwa nje ya nchi ambapo ikiwasili nchini inauzwa kwa shilingi 500 kwa gramu 500 sawa na shilingi 50,000 kwa kilo 50 kiasi ambacho ni kikubwa Mara tano ya gharama za chumvi inayozalishwa nchini kwani inauzwa kwa shilingi 5000 kwa kilo 50.
Alisema kuwa chumvi inayoagizwa nje ya nchi ni kiasi cha Tani 350,000 kila mwaka huku akisisitiza kuwa serikali ingetilia mkazo na kuboresha miundombinu nchini ingerahisisha upatikanaji wa chumvi nyingi nchini ambayo inauzwa kwa kiasi kidogo chenye uwezo wa kukidhi mahitaji ya watanzania.
↧
KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA DAWASA/DAWASCO KWA KAZI NZURI YA KUSIMAMIA MIRADI YA MAJI
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, RUVU
KAMATI ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo, imeipongeza Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) na Kampuni ya Maji Safi na Maji Taka, (DAWASCO), kwa kazi nzuri ya usimamizi wa miradi ya uboreshaji wa huduma za ugawaji na usambazaji maji katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Akizungumza kwenye majumuisho ya ziara ya kamati hiyo baada ya kutembelea miradi inayotekelezwa na kusimamiwa na DAWASA na DAWASCO Dar es Salaami na mkoa wa Pwani leo Januari 20, 2018, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe.Emmanuel Papian, alisema. Kazi iliyofanyika ni kubwa na Kamati imeona jinsi gani fedha za serikali zimetumika.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo alisema, miradi mingi inatekelezwa kwa fedha za mkopo kutoka India, lakini Kamati imebaini kuwa kila kitu kinafanywa na makampuni ya kutoka India, jambo ambalo sio sahihi sana.
“Inawezekana kuna mahali ambapo tumezidiwa, au kujichanganya, na kama ni kwenye component ya huo mkopo iliandikwa, kuna jambo la kuangalia na kujadili.” Alisema Mhe. Papian.
Aidha Mhe. Papian alisema Kamati inashauri kuwa watendaji wa ndani (Wakandarasi) wanapomaliza hii miradi basi vijana wa Kitanzania lazima wawe wameshajua na kufundishwa na wajifunze kila kitu ili waweze kuendesha miradi hii kikamilifu.
Ziara ya Kamati hiyo ilianzia makao makuu ya DAWASA, ambapo Kamati ilipokea taarifa ya utendaji ya DAWASA na DAWASCO, na kasha walipata fursa ya kutembeela baadhi ya miradi hiyo ambayo ni ujenzi wa matenki makubwa ya kuhifadhia maji ya Changanyikeni, Salasala, vituo vya kusukuma maji vya Makongo na Salasala.
Kamati pia ilitembelea eneo la utandazaji mabomba ya kusambaza maji huko Mpiji Machimbo na kumalizia ziara yao kwa kutembelea mitambo ya maji ya Ruvu chini na Ruvu Juu.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwangi’ngo alisema, Mradi wa uboreshaji wa huduma za ugawaji na usambazaji maji katika baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani unaendelea kwa kasi katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam na katika Miji ya Bagamoyo na Kibaha na tayari umefikia asilimia 72.2 kukamilika.
“Mradi huu unatekelezwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka, (DAWASA), ulianza rasmi Machi mwaka 2016 na unatarajiwa kukamilika Februari 28, 2018.” Alisema.
Akifafanua zaidi kuhusu kazi zinazofanyika kwa sasa, Mhandisi Mwang’ingo alitaja kuwa ni pamoja na ujenzi wa matenki tisa (9) ya kuhifadhi na kusambaza maji yenye ukubwa wa kuhifadhi kati ya lita za ujazo milioni 3.0 hadi milioni 6.0 ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vituo vine vya kusukuma maji na ununuzi na ufungaji wa pampu kubwa za kusukuma maji 16.
Kazi nyingine ni pamoja na ununuzi wa transfoma na ufungaji njia za umeme wa msongo mkubwa, ununuzi na ulazaji mabomba yatakayokuwa na urefu wa jumla ya kilomita zipatazo 477.
“Maeneo yatakayofaidika na mradi huu ni pamoja na Salasala, Bunju, Wazo, Makongo, Changanyikeni, Bagamoyo, Mpiji, Zinga, Kiromo, Kitopeni, Ukuni, Buma, Mataya na ukanda maalum wa WPZA ambayo ni maeneo yanayohudumiwa na mtambo wa Ruvu Juu.” Alifafanua.
Aidha maeneo mengine yatakayofaidika na mradi huu ni pamoja na Mbezi Louis, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Msakuzi, Makabe, Malamba Mawili na Msigani na maeneo hayo yote yanapata huduma ya maji kutoka mtambo wa Ruvu Juu uliozindulkiwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli Juni 21, 2017.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya DAWASA, Bw.;aston T. Msongole, alisema ni nia ya DAWASA kuhakikisha maeneo yote ambayo hayajafikiwa na huduma ya maji hususan baadhi ya maeneo ya wilaya mpya ya Kigamboni, ni kuhakikisha huduma hiyo inawafikia.
“Tayari tumechimba visima virefu vyenye uwezo wa kutoa maji mengi ya kumaliza tatizo la ukosefu wa maji kwenye maeneo hayo lakini tatizo ni uhaba wa fedha za kutengeneza mfumo wa kuyasambaza maji hayo kwa walaji” Alisema Bw.Msongole.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo, Mhe. Daniel; Nsanzugwanko, (katikati) akizunguzma jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwangi’ngo, (kushoto) na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo, Mhe. Emmanuel Papian, walipotembelea mtambo wa maji wa Ruvu Juu, Mlandizi mkoani Pwani.
Kaimu Mwewnyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo, Mhe. Emmanuel Papian, (Kushoto) na mjumbe wa Kamati hiyo, Mhe. Daniel Nsanzugwanko, (katikati), wakimsikilzia Mhandisi P.G. Rajani wa kampuni ya WAPCOS limited ya India, wakati wa ziara ya Kamati hiyo kwenye eneo la ujenzi wa mtambo wa kusukuma maji wa Salasala.
Taswira ya maendeleo ya ujenzi wa tenki kubwa la kuhifadhi na kusambaza maji la Salasala ukiwa umefikia hatua ya ufunikaji kabla ya kumwaga zege.
Mafundi wakisuka non do tayari kwa kumwaga zege kwenye tenki la Salasala.
Modester Mushi (kushoto), ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa ufundi DAWASA akiwa na Afisa Habari na UHusiano wa Jamii Mwandamizi wa Mamlaka hiyo, Bi.Mecky Mdaku wakati wa ziara hiyo ya Kamati ya Bunge huko Salasala.
![]()
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe.Emmanuel Papian, (kushoto), akizungumza jambo na Meneja Uhusiano wa Jamii, DAWASA, Bi. Neli Msuya. |
Kamati ikipokea taarifa ya utendaji ya DAWASA/DAWASCO mwanzoni mwa ziara hiyo.
![]()
Meneja Uhusiano wa Jamii, DAWASA, Bi. Neli Msuya, akigawa taarifa ya DAWASA kwa wajumbe wa Kamati. |
Baadhi ya wajumbe wa Kamati, wakisikiliza taarifa hiyo.
Mjumbe wa Kamati, Mhe,Kuntyi Yusuph Majala, akizunhgumza wakati wa Kamati ikipkea taarifa.
Mhandisi Mwangi’ngo, akitoa taarifa ya utendaji ya DAWASA.
Picha ya pamoja ya Kamati na watendaji wa DAWASA/DAWASCO na wajenzi.
Sehemu ya mtambo wa maji Ruvu Chini.
Sehemu ya mtambo wa maji Ruvu Chini.
↧
BREAKING NEWS: ACT WAZALENDO WAMETANGAZA KUJITOA KWENYE MARUDIO YA UCHAGUZI.
↧
↧
TAMASHA LA BUSARA KUENZI SANAA NA UTAMADUNI WA MWAFRIKA.
Na Mwandishi Wetu.
Watanzania wametakiwa kuenzi sanaa na utamaduni waliona kwa ajili ya kizazi kijacho ili kukijendea uzalendo wa kupenda nchi yao.
Hayo yamesema na Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud wakati akielezea ujio wa Tamasha la 15 linalotarajiwa kufanyika Ngome Kongwe, Unguja - Zanzibar kwa kushirikisha wanamuziki na vikundi mbali mbali vya sanaa kutoka pande zote za bara la Afrika na Ulaya.
“Katika Tamasha hili, ni sehemu ambapo watu wenye weledi wa sanaa mbalimbali hukutana, kuanzia kwa wakurugenzi wa matamasha mpaka kwa wazalishaji wa muziki, mameneja wa wanamuziki, wasambazaji wa muziki, wote hawa huja hapa Zanzibar mwezi Februari kuja kushuhudia utamu wa midundo ya muziki wa Ukanda wa Afrika Mashariki,” anasema Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud.
Anaongeza kuwa, “Hili siyo tu tukio ambalo watumbuizaji wa Tamasha pekee huhudhuria, bali hata baadhi ya wanamuziki ambao hawapo katika orodha ya kutumbuiza huja kwa minajili ya kujifunza kutoka kwa wale wanaofanya maonesho mbalimbali, na pia hupata fursa ya kufahamiana na wadau muhimu wa tasnia yao na kutengeneza mahusiano ya kikazi kwa miezi ijayo, hata zaidi ya hapo baada ya tamasha kuisha.”
Likisifika kuwa miongoni mwa matamasha yanayoheshimika, Sauti za Busara likiwa na kauli mbiu ya “Kuunganishwa na Muziki” kwa mwaka huu, linawakutanisha pamoja zaidi ya wanamuziki 460 katika visiwa vya Zanzibar.
Likiwa ni tamasha ambalo limeshuhudia ukuaji mkubwa katika uadhimishwaji wake na mwaka huu ukiwa wa 15, Tamasha hili linavutia wataalamu wa habari na muziki kutoka katika kila pembe ya Afrika, Ulaya na mahali pengine, ambapo hutoa jukwaa la kipekee kwa wanamuziki wa Afrika Mashariki kuutanganza muziki wao duniani.
“Kila mwaka, kila mwanamuziki anayepata fursa ya kutumbuiza katika jukwaa la Sauti za Busara, hualikwa kuzunguka katika miji mbalimbali duniani na kufanya maonesho kwenye matamasha yanayofanyika katika nchi hizo. Wanamuziki ambao hupata fursa ya kualikwa aghalabu, ni wale ambao wamethibitika katika maonesho yao kuwa wabunifu, wenye kuzungumza ujumbe fulani, na wanaocheza muziki wenye utambulisho fulani,” anasema Yusuf, akiwataja Msafiri Zawose, Jagwa Music, Leo Mkanyia, Tausi Women’s Taarab na Maulidi ya Homu ya Mtendeni kama mifano ya vikundi vya Kitanzania ambavyo tayari vimekwishaitwa katika safari za kimataifa baada ya kuonekana katika Tamasha la Sauti za Busara.
Kulingana na maelezo ya Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud, Tamasha la Sauti za Busara ni fursa adhimu ambayo wanamuziki kutoka Tanzania hawatakiwi kukosa, kwa kuwa fursa kama hizi ni chache na ngumu kuzipata ndani ya Afrika.
“Watu wa rangi tofauti huungana kwa pamoja kusheherekea muziki wa Kiafrika. Matarajio na msisimko ni mkubwa, hoteli zinazopatikana Stone Town huwa zinajaa katika wiki ya tamasha zikiwahudumia watu wanaotoka katika kila kona ya Tanzania, Afrika na Ulaya,” anasema Yusuf.
Kwa makadirio ya haraka, tamasha linachangia kiasi cha Dola za Marekani 7 milioni katika uchumi kila mwaka, kikiwa ni kipindi cha mavuno kwa biashara nyingi zinazofanyika kwenye kila pembe ya Zanzibar na sehemu zingine, na kulifanya Tamasha la Sauti za Busara kuwa zaidi ya ‘Tamasha la Muziki’.
Hata hivyo, licha ya kuwa na mafanikio hayo yote, lakini changamoto kubwa inayolikumba tamasha hili ni ufadhili, na ndiyo sababu hata tamasha la mwaka 2016 lilifutwa na kusababisha hasara kubwa sana kwa biashara nyingi visiwani Zanzibar.
“Tunaendelea kutegemea fedha za wafadhili kutoka katika balozi mbalimbali, ambapo balozi za Norway na Uswisi zikiwa miongoni mwa wafadhili wakubwa, zikisaidia mafunzo na jitihada za ujengaji uwezo,” anasema Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud.
Tamasha la Sauti za Busara 2018 linafadhiliwa na Ubalozi wa Norway, Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania na Zambia, Africalia, Mozeti, Zanlink, Memories of Zanzibar, Zenj FM, Chuchu FM, Tifu TV, Music In Africa, Ikala Zanzibar Stone Town Lodge, Emerson Zanzibar, Coastal Aviation, 2Tech Security, Ubalozi wa Ujerumani, Golden Tulip Dar City Centre.
↧
SCORPION AHUKUMIWA MIAKA SABA JELA.
↧
RC LUHUMBI ATANGAZA KIAMA KWA WAZAZI NA WALEZI AMBAO AWAJAWAANDIKISHA SHULE WATOTO WAO
Baadhi ya wakuu wa idara pamoja na waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wakati alipokuwa akizungumza na kuelezea mikakati iliyopo mkoani humo. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akiwashukuru wananchi ambao wamekuwa wakijitoa kuunga juhudi za serikali za kuhakikisha kila eneo linatatuliwa changamoto zake. |
Na,Joel Maduka,Geita
Serikali mkoani Geita imetangaza oparesheni ya kuwafuatilia wazazi na walezi ambao watoto wao walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza na kwamba hadi sasa bado awajawapelekwa shuleni na pindi watakapobainika watafikishwa kwenye vyombo vya sheria .
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa mkoa wa Geita Robert Gabriel wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa kwa seekondari hali sio nzuri ya wanafunzi ambao wametakiwa kuingia kidato cha kwanza kwani hadi sasa asilimia 46 ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza hawajaripoti shuleni.
Luhumbi ameongezea kwamba suala la elimu ni haki ya mtoto na hayupo tayari kuona wazazi wanawaozesha ama kuwaajiri kwenye shughuli za migodi na biashara ndogondogo watoto ambao wanaumri wa kwenda shule na wamefaulu mtihani wa darasa la saba.
Ameendelea kusema anafuatilia taarifa ya walimu ambao wameonekana kuwa ni kikwaza kwa kuchangisha fedha na kwamba endapo wakibaini hatua kali zitachukuliwa na kwamba amesikia kuna baadhi ya shule walimu wameendelea kuwatoza fedha wanafunzi kinyume na sheria.
katika mtihani wa darasa la saba mwaka jana wanafunzi 32,110 walifaulu na kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu lakini hadi kufikia tarehe 18 janaury mwaka huu wameripoti wanafunzi 17,202 sawa na asilimia 54 .
Kwa mujibu wa Takwimu zilizotolewa na idara ya elimu mkoa inaonyesha wilaya ya Bukombe walichaguliwa wanafunzi 3,985 na hadi sasa wameripoti 1,620 sawa na asilimia 41,Chato walichaguliwa 6,449 walioripoti ni 3,691 sawa na asilimia 57,Geita mji walichaguliwa 4,286 walioripoti ni 2,751,sawa na asilimia 64 huku Mbogwe waliochaguliwa ni 3,029 walioripoti ni 1,924 sawa na asilimia 64.
Halmashauri ya Geita vijijini wanafunzi 11,760 walichaguliwa kujiunga kidato cha kwanza lakini hadi sasa wameripoti wanafunzi 5,872 ambayo ni sawa na asilimia 50,wilaya ya Nyanghwale 2,601 walioripoti ni 1,344 sawa na asilimia 52
↧
ZANA ZA UVUVI HARAMU ZA MAMILIONI ZATEKETEZWA GEITA
Baadhi ya wananchi wakishuhudia zoezi la uteketezaji wa zana haramu za uvuvi kwenye Kijiji cha Nkome Wilayani Geita . |
Wananchi wa Kata ya Nkome wakiwa kwenye mkutano ambao ulikuwa na lengo la kuelezea hali ya uvuvi haramu ilivyo kwenye kata ya Nkome na namna ambavyo oparesheni imeweza kufanyika kwenye maeneo hayo. |
Kiongozi wa kikosi maalumu kinachoendesha oparesheni ya kupambana na uvuvi haramu ziwa victoria Gabriel Mageni akielezea namna ambavyo wameweza kuendesha zoezi hilo ndani ya siku kumi na mbili. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akisisita kwa wale ambao ni watumishi na viongozi kuacha kuendelea na tabia ya kushirikiana na wavuvi haramu . Na,Joel Maduka,Geita. |
Serikali Mkoani Geita Imeteketeza zana haramu zenye thamani ya shilingi milioni therathini na tatu zikiwemo Nyavu za makila zilizounganishwa 2,393,makokolo ya sangara 32,timba 142 makokoro ya dagaa 7 na dududu 11.
Hatua hiyo imetokana na oparesheni ya Kitaifa ya kupambana na uvuvi haramu ambayo inaendelea kwenye maeneo ya ziwa viktoria ikiwa na lengo la kuondoa uvuvi huo ndani ya ziwa hilo pamoja na kuondoa mitandao ya wafanyabiashara wa zana haramu za kuvulia ,biashara ya samaki wachanga na utoroshaji wa samaki na mazao ya yake,kwenda nje ya nchi kinyume cha sheria.
Zoezi hili la uteketezaji zana hizo limefanyika kwenye Kata ya Nkome ,ambapo kiongozi wa oparesheni hiyo Gabriel Mageni ,amemweleza mkuu wa mkoa huo kwamba kuna baadhi ya wafanyakazi wa hifadhi ya Rubondo wamekuwa wakihusika na uvuvi haramu kwa kuwaruhusu wavuvi kuingia kwenye hifadhi na wengine kuficha zana zao ndani ya hifadhi na kwamba wamekuwa wakilipwa fedha wafanyakazi hao maarufu kwa jina la "KIFUNDA"
Kufuatia malalamiko hayo mtandao huu umetafuta kwa njia ya simu afisa mahusiano wa TANAPA Pascal Shelutete alisema kuwa wao kama watu ambao wanamamlaka ya hifadhi za taifa na kwamba kwa mujibu wa kanuni na taratibu za sheria askari wao hawapaswi kushiriki kwenye vitendo vya ujangili na kwamba taratibu za kiuchunguzi zikifanyika na wakabaini kuna watumishi wanajihusisha na vitendo hivyo hatua za kisheria na za kinidhamu zitachukuliwa na hawawezi kuwakingia kifua.
Aidha Mageni aliongeza kuwa katika operesheni hiyo ambayo ina siku kumi na mbili baadhi ya mambo ambayo wameyabaini ni pamoja na baadhi ya viongozi wa vijiji na maofisa wanaosimamia maeneo ya uvuvi kuwapa hifadhi raia wa kigeni wanaojishughulisha na shughuli za uvuvi wakiwa hawana kibali na kusababisha serikali kukosa mapato.
Mkuu wa Mkoa huo,Mhandisi Robert Luhumbi,amewataadhalisha watendaji ambao wanashirikiana na wavuvi haramu na kwamba endapo kuna mtu hakibainika na kitendo hicho serikali itahakikisha inamchukulia hatua na kwamba kupitia oparesheni hiyo hatabakia hata mtu mmoja ambaye anajihusisha na shughuli hizo.
Nyawalwa Wange ni moja kati ya watu ambao wanajishughulisha na kazi ya uvuvi alisema agizo la Mkuu wa Mkoa ni la kuungwa mkono kutokana na kwamba uvuvi haramu umeendelea kuharibu kwa kiasi kikubwa samaki ambao wapo ndani ya ziwa viktoria na kwamba serikali iendelee kuwabaini wale wote ambao wanaendelea kufanya shughuli za uvuvi kinyume na sheria.
Katika oparesheni hiyo jumla ya fedha ambazo zimekusanywa ni zaidi ya milion, 111 fedha zinazotokana na faini ,malipo ya mrahaba pamoja na mauzo ya samaki.
↧
↧
MHE BITEKO AKIAGIZA KIWANDA CHA DANGOTE KUWEKA MKATABA WA UNUNUZI WA JASI KWA WACHIMBAJI WADOGO
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akitazama eneo la uzalishaji wa saruji katika kiwanda cha Dangote wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani Mtwara, Leo 19 Januari 2018. Picha Zote na Mathias CanalNaibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Kushoto) akitoa maelekezo kwa Meneja uzalishaji wa kiwanda cha Dangote Ndg Hemendra G. Raithatha alipotembelea kiwanda hicho wakati wa ziara ya kikazi Mkoani Mtwara, Leo 19 Januari 2018.Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja uzalishaji wa kiwanda cha Dangote Ndg Hemendra G. Raithatha kuhusu uzalishaji Wa saruji kiwandani hapo wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani Mtwara, Leo 19 Januari 2018.
Kikao cha kazi kikiendelea
Na Mathias Canal, Mtwara
Uongozi wa Kiwanda cha uzalishaji wa saruji cha (DANGOTE CEMENT LTD) Mkoani Mtwara umeagizwa kuandaa mikataba ya ununuzi wa jasi (Gypsum) na wachimbaji wadogo ili kuboresha Biashara ya wachimbaji hao sambamba na faida kwa kiwanda hicho kuliko ilivyo sasa ambapo kiwanda kinanunua Madini kutoka kwa wachimbaji wadogo bila kuwepo makubaliano maalumu yanayofanana kwa wote.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ametoa agizo hilo leo 19 Januari 2018 wakati akizungumza na uongozi wa kiwanda cha Dangote muda mfupi baada ya kutembelea kiwanda hicho akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mtwara.
Mhe Biteko alisema kuwa rasmi mikataba hiyo inapaswa kukamilika katika kipindi cha Siku 14 (Wiki mbili) kuanzia Leo 19 Januari 2018 hadi 2 Februari 2018 na kuwasilishwa kwenye ofisi ya madini kanda ambayo itawaita wadau wote kujadiliana vipengele vya mikataba hiyo ambayo itawafanya wachimbaji kuwa na bei ya pamoja na kutoa wajibu na haki kwa pande zote mbili.
Alisema kuwa katika mkataba huo ni lazima kuwepo kipengele cha kuwalipa ndani ya siku 30 wachimbaji Mara baada ya kiwanda kukusanya bidhaa zao jambo ambalo litaibua ufanisi na tija katika ukuzaji wa Biashara zao na kuaminika katika jamii.
Mhe Biteko alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli inataka wawekezaji wafanye kazi kwa amani pasina kusumbuliwa huku kwa upande wa wananchi wakisalia kunufaika na uwepo wa wawekezaji hao.
Alisema kuwa moja ya ajenda muhimu kwa serikali ni pamoja na kufanikisha ukuaji wa wachimbaji wadogo kufikia kuwa wachimbaji wa kati na hatimaye kuwa wachimbaji wakubwa hivyo ni lazima kuimarisha soko la ndani kwani wachimbaji wadogo hawawezi kukua kama soko la ndani halitaboreshwa.
Awali wachimbaji wa Jasi, walitoa kilio chao kwa Naibu Waziri huyo kuwa kiwanda cha Dangote hakinunui Madini yao na hata kikinunua malipo huchukua muda mrefu sana hadi miezi minne na kwamba kiwanda kinawagawa wachimbaji hao na kununua bei tofautitofauti kwa bidhaa moja jambo ambalo linawafanya wachimbaji wa Jasi kuambulia hasara.
Aidha, Naibu Waziri wa Madini Mhe Biteko amewataka watanzania wote wanaofanya kazi kwenye migodi na kwingineko kuwa waaminifu mahali pa kazi kwani kumekuwa na malalamiko ya wizi hususani migodini jambo ambalo linapunguza imani kwa wawekezaji.
↧
MKURUGENZI WA NGO YA MWANZA NA WENZAKE 9 WANASWA NA TAKUKURU KWA UTAPELI.
↧
TANZIA: BIBI LULU AKIDA SILVESTER AFARIKI DUNIA, MSIBA UKO SINZA MKABALA NA KITUO CHA SIMU 2000 DAR ES SALAAM
Maandalizi ya mazishi yanafanyika nyumbani kwa marehemu Sinza mkabala na kituo cha daladala Simu 2000.
Mwili utaagwa Jumatano Januari 24, 2018 kuanzia saa 8 mchana Kanisani KKKT Usharika wa Sinza -Kumekucha.
Mwili wa marehemu utasafirishwa siku ya Alhamisi tarehe 25/01/2018 kuelekea Kijiji cha Nronga-Machame, wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro.
↧
BILIONI 3 ZILIZOTOLEWA NA SERIKALI MKOANI GEITA ZINATARAJIWA KUBORESHA MIUNDOMBINU KATIKA VITUO SABA VYA AFYA
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akishiriki kuchimba msingi kwenye kituo cha afya cha Masumbwe Wilayani Mbongwe. |
Wananchi wakishiriki kwenye ujenzi wa msingi kwenye kituo cha afya cha Masumbwe Wilayani Mbongwe. |
Mkuu wa Wilaya ya Mbongwe ,Mathar Mkupasi akizungumza na wananchi ambao walikuwa wamejitokeza kuunga mkono jitihada za serikali za ujenzi wa jengo la kupasulia kwenye kituo cha afya cha Masumbwe. |
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM,Wilayani Mbongwe Johari Juma akisisitiza wanachama wa chama hicho kuwa mstari wa mbele kushiriki katika shughuli za maendeleo. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita ,Mhandisi Robert Luhumbi akisisitiza namna serikali ilivyojipanga kupunguza changamoto ya huduma za afya Mkoani humo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mbongwe. |
Na,Joel Maduka,Geita.
Jumla ya Sh Bilioni 3 zilizotolewa na serikali Mkoani Geita zinatarajiwa kuboresha miundombinu katika Vituo saba vya afya .
Mganga mkuu wa Mkoa wa Geita Dr Japhet Simeo alisema lengo kuu la hizo fedha ni kuboresha miundo mbinu kwa maana ya chumba cha upasuaji kujenga wodi ya watoto,wakina mama ,maabara na chumba cha kuhifadhia maiti na kwamba wanatarajia kuona fedha hizo zinafanyika kuboresha mandhari ya kituo kwa maana ya bustani na majengo ambayo yamechakaa.
Simeo alizitaja wilaya ambazo zimepatiwa fedha hizo ni wilaya 5 ikiwemo halmashauri ya wilaya ya Geita ambayo imepewa kiasi cha sh ,Milioni 500 kwenye kituo cha afya cha Nzera na kwamba hadi sasa wameshajenga majengo manne ambayo yamekaribia kukamilika , Mbogwe milioni 800 ambazo zimegawa kwenye vituo viwili vya afya, Bukombe milioni 400 kwaajili ya kituo cha afya cha uyovu , Chato wamepatiwa fedha kwaajili ya vituo viwili ambvyo ni Bwanga Milioni 500 na Karumwa milioni 400 na Wilaya ya Nyang’hale milioni 400 kwaajili ya kituo cha afya cha Nyang’hale.
Juma Mabura ni moja kati ya wananchi wa Wilaya ya Mbongwe ambapo ameelezea kuwa kumekuwape na changamoto kubwa ya upungufu wa majengo na kwamba kukamilika kwa baadhi ya majengo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma ya afya.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Luhumbi amesema kuwa majengo yaliyo kwenye hatua ya renta na maboma yakikamilika watakuwa kwenye asilimia 55 kwa maana ya zahanati 262 na kwamba nyingine wameanza ujenzi .
Aidha amesisitiza kuwa lengo la serikali ni kuondoa kero ya kimiundombinu kwenye sekta ya afya ili kuwawezesha watanzania kupata huduma bora za afya.
↧
↧
MBUNGE MGIMWA NIPO TAYARI KUNYIMWA KURA KATIKA UCHAGUZI WA MWAKA 2020
Mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamuod Mgimwa aikiongea na baadhi ya walimu wa shule za sekondari na shule za msingi jinsi gani ya kutatua kero zilipo shuleni ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi![]()

Mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamuod Mgimwa akiwakabidhi zawadi ya mbuzi kwa walimu wa shule za msingi waliofanya vizuri katika moja ya kata iliyopo jimboni kwake.
Na Fredy Mgunda, Iringa
Wananchi wa jimbo la Mufindi kaskazini wametakiwa kuwapeleka watoto wao shule kwa lazima kwa kuwa elimu inatolewa bure na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Mafuli kwa lengo la kuhakikisha kila mwanafunzi wote waweze kupata elimu na kuondoa ujinga na kuleta maendeleo kwa taifa.
Hayo yamesemwa na mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamuod Mgimwa alipokuwa kwenye ziara ya kukagua miundombinu ya shule zilizopo katika jimbo hilo ili kuweza kuzitatua changamoto zilizopo katika maendeo hayo.
Akiwa bado yupo kwenye ziara hiyo mbunge huyo aligundua kuwa wazazi wengi wamekuwa kikwanzo cha kuwapeleka shule watoto wa hivyo akawataka viongozi wote wa serikali za vijiji kuwa chukulia hatua wazazi ambao hawatawapekeka shule watoto wao.
Mgimwa alisema kuwa yupo tayari kunyimwa kura na wananchi ambao atawachukulia hatua za kisheria kwa kutowapeleka shule watoto wao kwa ajili ya faida ya maisha yao.
“Nasema kweli nitakubali kuachia ngazi ya kuwa mbunge kwa kunyimwa kura za wananchi wasiopenda maendeleo ya watoto wao,hadi sasa shule zimefungua lakini wazazi hawawapeleki shule watoto nitahakikisha wanachukuliwa hatua za kisheria” alisema Mgimwa
AidhaMgimwa alisema kuwa sasa imefika mwisho kwa watoto wa jimbo la Mufindi Kaskazini kuwa soko la wafanyakazi wa kazi za ndani wakati wanauwezo wa kuwa viongozi hapo baadae.
“Nasema tena haiwezekani kila mfanyakazi ukifika daresalaam utasikia katoka Iringa jimbo la Mufindi Kaskazini sasa sitaki kusika swala hilo na wazazi wanaofanya hivyo nitawachulia hatua za kisheria serikali ya awamu ya tano inataka kuwa na wasomi wengi ili kuasaidia maendeleo ya nchi”alisema Mgimwa
Mgimwa alisema kuwa wazazi wa jimbo la Mufindi la Mufinda watafungwa kwa kuwapeleka watoto wao kufanya kazi za ndani pindi wamalizapo shule ya msingi au sekondari kufanya hivyo kunadumaza maendeleo yao.
“Haiwezekani mwanafunzi amefaulu halafu mzazi anampeleka kufanya kazi za ndani siwezi kukubali hata kidogo maana nimegundugua wazazi wengi hawapendi watoto wao waendelee kusoma badala yake wanataka wakafanye kazi za ndani narudia kusema mtoto akifaulu asipopelekwa shule nitamchulia hatua za kisheria huyo mzazi” alisema Mgimwa
Mgimwa aliwataka wanafunzi wakike kuacha kufanya ngono wakiwa na umri mdogo ili kupunguza mimba za utotoni na kupoteza dira ya maisha wakiwa watoto wadogo na kufanya hivyo kutawapelekea kufungwa jela kwa kuwa sheria itachukua mkondo wake.
“Acheni kufanya tendo la ndoa mkiwa na umri mdogo ili baadae mjenge maisha yetu viongozi wengine wa wanawake wanavyofanya kazi serikalini na kwenye mashirika mbalimbali ya nje ya nchi na ndani ya nchi”alisema Mgimwa
“Acheni kufanya tendo la ndoa mkiwa na umri mdogo ili baadae mjenge maisha yetu viongozi wengine wa wanawake wanavyofanya kazi serikalini na kwenye mashirika mbalimbali ya nje ya nchi na ndani ya nchi”alisema Mgimwa
Mgimwa aliwapongeza walimu wa shule za msingi za jimbo la Mufindi Kaskazini kwa kuendelea kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa na kuendelea kuitangaza vizuri jimbo hilo kupitia elimu.
“Kwa kweli nisiwe mnafiki nichukue fursa hii kuwapongeza walimu kwa kufanya vizuri maana kila mwaka elimu inazidi kukua katika jimbo la Mufindi Kaskazi na kuendelea kuitangaza kitaifa” alisema Mgimwa
nao baadhi ya walimu wakuu wa shule zilizopo jimbo la Mufindi Kazskazini walisema kuwa wazazi wengi wamekuwa kikwazo cha maendeleo ya wanafunzi kwa kuwakatisha tamaa juu ya umuhimu wa elimu.
“Hapa katika kata hii ya Kibengu wazazi wengi hawapendi watoto wao kwenda kusoma kwa kuwa watakuwa wanapunguza nguvu kazi zao mashambani ndio maana hawawapatii mahitaji muhimu ya kuwasaidia wanafunzi kusoma kwa uhuru” alisema walimu
Walimu walimuomba mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini kutafuta wataalam wa saikolojia kuja kuwapa elimu wazazi ili kukuza taaluma kwa wanafunzi wa kata hiyo.
“Ukiangalia hali ya ufaulu wa shule hizi ni mzuri lakini kutokana na wazazi kutokujua umuhimu wa elimu wamekuwa hawawapeleki watoto wao sekondari wakifaulu mitihani ya shule ya msingi hivyo inapelekea upungufu wa wanafunzi katika shule ya sekondari ya Ilogombe” alisema Walimu.
Mfikwa alisema kuwa wamekuwa wakiitisha mikutano ya mara kwa mara lakini bado tatizo kubwa hivyo jitihada zinahitajika kukomesha tabia hiyo kwa kuwa bila hivyo watoto wa kata hiyo wataendelea kuwa wafanyakazi za ndani tu
Zakayo Kilyenyi ni diwani wa kata ya Kibengu alikiri kuwa wazazi wengi wa kata hiyo hawana elimu juu ya umuhimu wa kujua dhamani ya elimu katika maendeleo ya familia zao na taifa kwa ujumla.
“Kweli kabisa wazazi wa kata ya Kibengu wamekuwa wakiwaambia watoto wasifanye mitihani vizuri ili wasifaulu kwa kuwa wakifaulu watakuwa na gharama kubwa ya kuwasomesha hivyo wakifeli wataenda kuwafanya kazi za ndani na ndio furaha kwa wazazi wa kata ya Kibengu” alisema Kilyenyi
Kilyenyi alisema kuwa uongozi wa kata ya Kibengu utaendelea kutoa elimu kwa wazazi hao ili kurudisha morali ya kuendelea kuwapa mahitaji muhimu yanayohitajika shuleni kwa kwa lengo la kuboresha maisha ya watoto hao.
“Zana potofu zimekuwa kikwazo kikubwa sana katika maendeleo ya wananchi wa kata ya Kibengu hivyo tukiondoa zana hiyo elimu itakuwa kwa wanafunzi wa kijiji hichi” alisema Kilyenyi
↧
FULL TIME: KAGERA SUGAR 0 vs 2 SIMBA SC, NDEMLA NA BOCCO WALIPA KISASI KAITABA LEO, SIMBA AREJEA KILELENI!
Simba imezidi kujichimbia kileleni baada ya kuichapa Kagera Sugar kwa mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba hii leo jioni.
Bao za Simba Sc leo hii zimefungwa kipindi cha pili baada ya kumaliza dakika 45 timu zote mbili zikiwa 0-0. Bao la kwanza limefungwa na Said Ndemla na bao la pili limefungwa na John Bocco baada ya mabeki wa Kagera Sugar kujichanganya.
Kipindi cha pili dakika ya 70 Said Ndemla aliipatia Simba goli la Kwanza na kufanya Simba kuongoza kwa bao 1-0. Wakati huo baaada ya bao hilo Shomari Kapombe aliingia kwa mara ya kwanza tangu asajiliwe Simba akichukua namba ya Gyan.
Kipindi hicho cha pili dakika ya 80 John Bocco aliipachikia Simba bao la pili Baada ya kazi nzuri ya Shomari Kapombe aliyeingia kipindi hicho cha pili na Simba kuwatandika bao la pili na Simba kuongoza bao 2-0' Hadi dakika 90 zinamalizika Simba 2-0 Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Ushindi huo unawarudisha Simba kileleni wakiwa na pointi 32.
Kiungo wa Simba Hamis Said Juma (Ndemla) akipeta baada ya kufunga bao la kwanza dhidi ya timu ya Kagera Sugar.
Beki wa Kagera Sugar Juma Nyosso akikimbiza mpira akiwa sambamba na mshambuliaji wa Kagera Sugar Emmanuel Okwi.
Kadi ya Njano ilitolewa kwa mchezaji wa Kagera Sugar Fakhi
Emmanuel Okwi akiwa Chini chaliii!!
Mshambuliaji wa Kagera Sugar akimwangalia Mwamuzi juu ya rafu aliyotendewa na Mchezaji wa Kagera Sukari.
Okwi akiwa chini
Mlinzi wa Kagera Sugar Asante Kwasi akijutia kukosa nafasi ya kufunga bao
John Bocco akiwa chini na mwezake wa Kagera Sugar baada ya patashika kutokea...kipindi cha pili.
Jukwaa kuu wakiutaza mchezo
Viongozi mbalimbali wakiwa jukwaa kuu wakiutaza mchezo Kagera sugar dhidi ya Timu ya Simba ya Jijini Dar es Salaam.

Hakuna kupita!! hapa!

Mchezaji wa Kagera Sugar alimdhibiti mchezaji wa Simba kupita hapa!
Kichuya akijiandaa kupiga kona.
Mavugo wakati huo akipiga jalamba
Patashika kwenye lango la Kagera Sugar kipindi cha pili
Juma Kaseja akimcheki John Bocco
John Bocco akimtoka Mohamed Fakhi wa kagera Sugar
Baada ya kumtoka aliachia pasi kwa Mdemla aliyemalizia nyavuni na kuwanyanyua mashabiki wa Simba kwenye Viti kwenye Uwanja wa Kaitaba.
Shangwe kwa Ndemla
Wakipongezana kwa bao
Raha kwa Mashabiki wa Simba
Wachezaji wa Kagera Sugar baada ya mchezo kumalizika wakiwa wamepoteza mchezo huo wa bao 2-0 mbele ya timu ya Simba SC ya jijini Dar es Salaam.
↧
VIDEO:- HAWA HAPA 10 WALIONASWA NA TAKUKURU MWANZA KWA UTAPELI WA AJIRA
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Mwanza, inawashikilia watu 10 akiwemo Mkurugenzi mkuu wa shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na kusaidia mama na mtoto pamoja watu wanaioshi na virusi vya ukimwi, Andrea Mabagala kwa tuhuma za kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu kinyume cha sheria.
Mkuu wa Takukuru mkoani Mwanza, Ernest Makale, amewaambia waandishi wa habari kuwa watuhumiwa hao wamekuwa wakiwatapeli watu mbalimbali wakiwemo wahitimu wa vyuo vikuu kwa lengo la kuwapatia ajira kinyume cha sheria.
↧
NAIBU WAZIRI WA ELIMU ATAKA VIFAA VYENYE THAMANI YA SH 14 BILIONI VIFUNGWE HARAKA
![]() |
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,William Ole Nasha akitoa hotuba yake wakati wa mahafali ya tisa ya Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) |
![]() |
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,William Ole Nasha(wa pili kuli) akiwapongeza wanafunzi wahitimu waliofanya vizuri zaidi katika kozi walizosomea |
Arusha.Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,William Ole Nasha ameuagiza uongozi wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) uwe umefunga vifaa vya kisasa vyenye thamani ya Sh 14 bilioni ndani ya wiki nne badala ya siku 67 ili vianze kutumika mara moja.
Ametoa agizo hilo kwenye mahafali ya tisa ya wahitimu 465 wa fani mbalimbali za ufundi jijini hapa kuwa ukarabati na upanuzi wa karakana ufanyike ndani ya muda alioutoa ili vifaa hivyo vitumike kwa malengo yaliyokusudiwa.
"Nilipotembelea Chuo hiki Desemba 2,mwaka jana nilitoa maagizo mharakishe ujenzi na ukarabati wa miundombinu itakayotumika kufunga vifaa hivyo kutoka Austria,nafarijika kusikia kuwa utaanza mara moja kwani Wizara ilishatoa kibali cha kutumia watalaam wenu wa ndani na fedha mnayo,"alisema Ole Nasha
Alisema sekta ya elimu ya ufundi kwa mujibu wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2015 inatarajiwa kuleta maendeleo ya haraka ya rasilimali watu walioelimika na kupenda kujielimisha zaidi ili kulifanya taifa lipate maendeleo.
Ole Nasha aliongeza kuwa elimu ya ufundi ina mchango mkubwa katika kufikia uchumi wa kati unaotegemea viwanda na nchi zilizoendelea kama Japan na China zimefikia hapo zilipo kwa kutilia mkazo elimu ya ufundi.
"Katika Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo 2016/17 hadi 2020/21 tunalenga kuongeza idadi ya wahitimu wa Vyuo vya Ufundi Stadi(Veta) kutoka 150,000 hadi 700,000 na Vyuo vya Elimu ya Ufundi vinavyotoa elimu ya Kati kutoka 40,000 hadi 80,000,"alisema
Kuhusu idadi ya wasichana wanaosoma elimu ya ufundi kuwa ndogo alivitaka vyuo vyote vya ufundi nchini kuweka mikakati ya kuongeza udahili ikiwa ni pamoja na kutoa kipaumbele maalum kwa kwa wanafunzi wa kike wanaomba kujiunga.
Pia aliagiza Mamlaka ya Elimu nchini(TEA)kuharakisha upatikanaji wa fedha kiasi cha Sh 1.7 bilioni kilichotengwa kwaajili ya ujenzi wa hosteli za wasichana katika Chuo hicho ili kupunguza pengo katika wavulana na wasichana.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha ATC,Dk Masudi Senzia alisema wahitimu 465 wamemaliza katika ngazi za Astashahada ya awali,Astashahada ,Stashahada na Shahada huku wahitimu wa kike ni 101 sawa na silimia 21 na wahitimu wa kiume ni 364 sawa na asilimia 78.
Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com
↧
↧
KAMANDA WA POLISI AWEKA BAYANA CHANZO CHA ALIYEGONGWA NA NDEGE.
↧
KAIMU MKURUGENZI MKUU TAA ATEMBELEA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
↧
fastjet | Pata bei nafuu zaidi za nauli kati ya Dar es salaam na Mbeya |Kilimanjaro unaposafiri na fastjet kila siku
| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
↧