↧
"SIO MIMI NILIESEMA CCM IMEOZA" Ridhiwan Kikwete akanusha
↧
WAWILI WAFARIKI DUNIA, WANNE WAJERUHIWA AJALI YA MABASI SENGEREMA.
↧
↧
WANAFUNZI SABA WAFANYA MTIHANI NA KUFAULU KUPANDISHWA MADARAJA YA MKANDA MWEUSI WA GOJU Ryu KARATE.
Sensei Rumadha Fundi akiwafanyisha mazoezi wanafunzi saba hao kabla ya kuanza kufanya mtihani wao wa kupanda daraja katika Dojo la Hekalu la Kujilinda lililomo katika ukumbi wa Shule ya Msingi ya Zanaki jijini Dar es salaam Jumatatu usiku Januari 22, 2018
Viongozi wakuu wa Dojo la Hekalu la Kujilinda lililomo katika ukumbi wa Shule ya Msingi ya Zanaki jijini Dar es salaam wakishuhudia wanafunzi saba wakifanya mazoezi kabla ya mtihani Jumatatu usiku Januari 22, 2018. Kutoka kulia ni Sensei Wilfred Malekia, Sensei Mohamed Murudker na Sensei Rashid Almasi
Sensei Rumadha Fundi akiendelea kuwafanyisha mazoezi wanafunzi saba hao kabla ya kuanza kufanya mtihani wao wa kupanda daraja katika Dojo la Hekalu la Kujilinda lililomo katika ukumbi wa Shule ya Msingi ya Zanaki jijini Dar es salaam Jumatatu usiku Januari 22, 2018
Sensei Rumadha Fundi akiendelea kuwafanyisha mazoezi kwa vitendowanafunzi saba hao kabla ya kuanza kufanya mtihani wao wa kupanda daraja katika Dojo la Hekalu la Kujilinda lililomo katika ukumbi wa Shule ya Msingi ya Zanaki jijini Dar es salaam Jumatatu usiku Januari 22, 2018
Sensei Rumadha Fundi akitoa mwongozo akiwa na uongozi wa dojo kabla ya mtihani wa kupanda daraja wa wanafunzi saba katika Dojo la Hekalu la Kujilinda lililomo katika ukumbi wa Shule ya Msingi ya Zanaki jijini Dar es salaam Jumatatu usiku Januari 22, 2018
Kutoka kushoto Ma-Senpai Abdulmajid Khan wa Hekalu la Kujilinda pamoja na Shaaban Yusuf na Galant Swai ambao wanatoka katika tawi la Hekalu la Kujilinda lililopo mjini Dodoma kwa jina la Miyagi dojo wakifuatiwa na ma-Senpai Yusuf Kimvuli wa Kaizen dojo na Senpai Seif Soud wa Hekalu la Kujilinda.
Wanafunzi watatu waliofaulu na kupanda daraja la kwanza (1st Dan) ama "Shodan" kutoka mkanda wa kahawia ni kutoka kushoto ma-Senpai Abdulmajid Khan wa Hekalu la Kujilinda pamoja na Shaaban Yusuf na Galant Swai ambao wanatoka katika tawi la Hekalu la Kujilinda lililopo mjini Dodoma kwa jina la Miyagi dojo.
Na Sultani Kipingo wa Globu ya Jamii
Wanafunzi waandamizi saba wa shule za Karate (dojo) mtindo wa Okinawa Goju Ryu za Kaizen na Hekalu la Kujilinda za jijini Dar es salaam na Dodoma wamefanya mitihani na kufaulu kupandishwa madaraja ya mkanda mweusi chini ya Sensei Rumadha Fundi (BOFYA HAPA KUMJUA) usiku wa Jumatatu Januari 22, 2018.
Wanafunzi hao kutoka Kaizen dojo iliyopo Shule ya Sekondari ya Jamhuri na dojo dada ya Hekalu la Kujilinda iliyopo katika shule ya msingi ya Zanaki ni pamoja na ma-Senpai Yusuf Kimvuli, Abdulwahud Aghfoul, Bilali Mtenga na Seif Soud ambao wamepanda kutoka mkanda mweusi daraja la kwanza (1st Dan) kwenda la daraja la pili (2nd Dan) lijulikanalo kama "Nidan".
Wakati ma-Senpai Kimvuli, Maghfoul na Mtenga wanatoka dojo la Kaizen, Senpai Seif Soud anatoka Hekalu la Kujilinda.
Wanafunzi wengine watatu waliofaulu na kupanda daraja la kwanza (1st Dan) ama "Shodan" kutoka mkanda wa kahawia ni ma-Senpai Abdulmajid Khan wa Hekalu la Kujilinda pamoja na Shaaban Yusuf na Galant Swai ambao wanatoka katika tawi la Hekalu la Kujilinda lililopo mjini Dodoma kwa jina la Miyagi dojo.
Hii ni mara ya kwanza kwa Sensei Rumadha Fundi mwenye Dan 4,“Yondan” na mwenye uzoefu mkubwa wa mafunzo ya Goju Ryu chini ya walimu wakuu wengi maarufu toka Okinawa, Japan, kuwafanyia mitihani na kuwapandisha madaraja wanafunzi wa Tanzania.
Sensei Rumadha, ambaye alianza mafunzo ya Okinawa Goju Ryu miaka 38 iliyopita katika Hekalu la Kujilinda la Zanaki amesema anajisikia furaha na fahari kutimiza hilo jukumu lake kwa mara ya kwanza, na kwamba hajutii kufunga safari hii kutoka Houston, Marekani, anakoishi na kuja kuwasaidia ndugu zake.
Na hilo liliwezakana baada ya mwaka jana huko nchini Poland Sensei Rumadha kufanya na kufaulu vizuri mitihani wake wa kupanda ngazi toka Dan ya tatu "Sandan" kwenda ngazi ya nne "Yondan" chini ya waamuzi (masters) toka Okinawa wakiongozwa na Sensei Yoshihiro Kancho Miyazato, ambaye ni Master au mwalimu mkuu wa Okinawa Goju Ryu Jundokan So Honbu Karate-Do huko Okinawa.
Tokea hapo Sensei Rumadha amekuwa na mamlaka ya kuwasaidia wanafunzi wake wa Tanzania na kuwafanyia mitihani na kuwapa wanafunzi "Dan" hadi ngazi ya pili " Nidan" sababu katika Goju Ryu Karate kuanzia Dan ya 3 na kuendelea hutolewa na Master Miyazato pekee.
"Hawa waliofaulu na kupanda daraja la pili hivi sasa wana mamlaka ya kufungua shule zao chini ya uangalizi wangu na wakiendelea kufanya vyema nitatoa idhini ya wao kuwa waalimu ("Sensei") wanaotambulika Okinawa baada ya muda si mrefu ujao" amesema Sensei Rumadha.
Hakusita kutoa shukran zake nyingi kwa mlezi wake wa mafunzo tokea utotoni, "Sensei Magoma Nyamuko Sarya akisema chini ya uongozi wake kitengo cha watoto kilichoitwa "Bomani Brigade" kilichobuniwa na mwanzilishi wa Okinawa Goju Ryu nchini Tanzania mwaka 1973, hayati Sensei Nantambu Camara Bomani.
Alitoa shukurani za pekee kwa viongozi wa sasa wa Hekalu la Kujilinda - Sensei Mohamed Murudker, Sensei Wilfred Melkia, Sensei Geofrey Sawayael “Shoo” na Sensei Rashid Almasi ambao amesema moyo wao wa kuendeleza Goju Ryu bila kutetereka pale Zanaki ni wa kusifika, na kwamba anawapongeza sana.
Sensei Rumadha pia ameeleza kuwa kabahatika mwaka huu kualikwa kuiwakilisha Tanzania ambayo pamoja na na Angola ni nchi pekee za Afrika zilizoalikwa kuhudhuria maadhimisho ya miaka 65 tangu kuanzishwa kwa chama cha "Jundokan" na Master Eiichi Miyazato Sensei huko Naha City, Okinawa, mwezi wa Novemba 1918.
Chama hicho kwa sasa kinaongozwa na mwanawe Yoshihiro Kancho Miyazato, ambaye pia ni Mwenyekiti mkuu dunia wa chama hicho na mwanae Master Eiichi Miyazato, ambaye amewafanyia mitihani ya mkanda mweusi zaidi ya walimu 15 toka ngazi ya pili" Nidan" hadi ngazi ya saba "Nandan".
Kwa mujibu wa Sensei Rumadha, ngazi hizo zote kwa utamaduni wa mtindo wa Okinawa Goju Ryu Karate huchukua miaka mingi sana kupandishwa ngazi tofauti na mitindo mingine.
↧
RC MASENZA AZIPIGA JEKI SHULE TANO MKOANI IRINGA
Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua moja ya shule ya sekondari ambayo inajengwa kwa nguvu za wananchi na serikali kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu mkoani Iringa
Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua moja ya shule ya sekondari na akiuliza kitu kuhusu ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyanzwa
Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua moja ya shule ya sekondari akielekea kukagua vyoo vya shule ya sekondari ya Nyanzwa
Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua vyoo vya shule ya Nyanzwa
Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua vyoo katika sekondari ya Ibumu
Na Fredy Mgunda,Kilolo
Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua moja ya shule ya sekondari na akiuliza kitu kuhusu ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyanzwa
Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua moja ya shule ya sekondari akielekea kukagua vyoo vya shule ya sekondari ya Nyanzwa
Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua vyoo vya shule ya Nyanzwa
Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua vyoo katika sekondari ya Ibumu
Na hili ni moja ya jengo ambalo linajengwa kwa ajili ya maabara za shule ya sekondari ya Ibumu
MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ametoa jumla ya shilingi milioni nne (4,000,000) kwa ajili ya kuchochea manendeleo ya ujenzi majengo kwenye shule nne za sekondari ikiwa na lengo la kuhakikisha kuwa wanafunzi wa shule hizo wanasoma bila kuwa na usumbufu wowote ule.
Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa shule mpya za sekondari zilizopo tarafa ya Mazombe mkuu wa mkoa Amina Masenza alisema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr John Pombe Magufuli imejipanga kuhakikisha wanafunzi wanasoma bila kulipia kitu mchango wowote ule utakaochangishwa na walimu.
“Mimi nimetumwa na Rais kusisimamia ila ya chama cha mapinduzi kuhakikisha inatendewa haki katika kuleta maendeleo hivyo ni lazima nihakikishe wanafunzi wanakwenda shule na sio vinginevyo maana bila wanafunzi kwenda shule Rais hawezi kunielewa nitakuwa sijatimiza malengo ya kutoa elimu bila malipo” alisema Masenza
Masenza alisema kuwa atachangia shilingi milioni moja kwa kila shule za sekondari za tarafa hiyo ambazo zipo kwenye ujenzi na shule hizo ni Ibumu na Nyanzwa ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma na kuwapunguzia umbali wa kutoka eneo moja kwenda eneo jingine kuifuata shule.
“Naombeni tuzikamilishe shule hizi kwa wakati ili kuwapunguzia umbali wa kusoma watoto wetu haiwezekani wanafunzi hadi kuikuta shule moja ni umbali wa zaidi ya kilometa kumi na tatu ,jamani hawa ni watoto zetu na maisha yao yanategemea elimu hivyo ni lazima tuwekeze kwenye elimu” alisema Masenza
Masenza aliwataka viongozi wa vijiji kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliofulu na kuchaguliwa kuingia kidato cha kwanza wapelekwe shule kwa wakati na wazazi wote ambao hawajawapeleke shule watoto wao wachukuliwe hatua kwa kuwa Rais hataki kuskia kuwa mtoto hajaenda shule.
“Jamani Rais ameagiza kuwa wanafunzi wote wanatakiwa kuwa shule hata kama hawana sare za shule sasa huyo mzazi gani ambaye hatakiwa kuwa peleka shule naombeni kabla sijawakulia hatua nyinyi viongozi basi hakikisheni wanafunzi wote waliofaulu wanakwenda shule” alisema Masenza
Lakini mkuu wa mkoa alifanya ziara kwenye shule ya sekondari Kihesa manispaa ya Iringa na akatoa kiasi cha shilingi laki tano (500,000),shule ya sekondari Ilambilole shilingi milioni moja(1,000,000) na shule ya msingi Matembo nako alitoa kiasi cha shilingi laki tano (500,000) pesa zote hizo ni kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa majengo ya shule.
Aidha Masenza alisema kuwa sasa imefika mwisho kwa watoto wa mkoa wa Iringa kuwa soko la wafanyakazi wa kazi za ndani wakati wanauwezo wa kuwa viongozi hapo baadae.
“Nasema tena haiwezekani kila mfanyakazi ukifika daresalaam utasikia katoka Iringa sasa sitaki kusika swala hilo na wazazi wanaofanya hivyo nitawachulia hatua za kisheria serikali ya awamu ya tano inataka kuwa na wasomi wengi ili kuasaidia maendeleo ya nchi”alisema Masenza
Sipia Kinyowa ni kaimu mtendaji wa kata ya Nyanzwa, Amidu Kilamba diwani wa kata ya Nyanzwa,Hemerd Wiliamu diwani wa kata ya Ibumu na Justine Mgina mtendaji wa kata ya Ibumu ni baadhi ya viongozi waliompungeza mkuu wa mkoa kwa ziara aliyoifanya ya kimaendeleo na kimkatikati kuhakikisha wanafunzi wote wanatakiwa kufika shule na kusoma bila kubuguziwa na mtu yeyeto.
“Leo tumefarijiaka sana kuona mkuu wetu kaja na mikakati hasa ya kusaidia kukuza maendeleo kwenye sekta ya elimu hivyo hatuna budi kumuunda mkono kuhakikisha kuwa mambo aliyoyaongea tunayafanyia kzi ili kuhikisha wanafunzi wanasoma” walisema vingozi
↧
TIGO KANDA YA ZIWA YAMWAGA PESA KWA MAWAKALA WAKE WASHINDI.
Hatimaye Tigo Kanda ya Ziwa Victoria hii leo wamekabidhi zawadi kwa Mawakala washindi wawili katika shindano waliloshindanishwa kupitia utoaji huduma.
Mshindi wa kwanza kajinyakulia kitita cha shilingi milioni 2, huku mshindi wa pili akiondoka na kitita cha shilingi milioni 1, sherehe ya makabidhiano imefanyika ndani ya moja ya kumbi za Gold Crest Hotel jijini Mwanza na kuhudhuriwa na wafanyakazi na mawakala wa Tigo.
↧
↧
KAMATI YA BUNGE YA ARDHI,MALIASILI NA MAZINGIRA YAVUTIWA NA UBUNIFU WA SHUGHULI ZA KITALII HIFADHI YA TAIFA YA ZIWA MANYARA.
![]() |
Meneja Ujirani Mwema wa Tanapa,Hemed Mbugi akitembea juu ya daraja linalo ‘bembea’ ambalo ni moja kivutio kwa watalii wa nje na ndani. |
![]() |
Mbunge wa jimbo la Mtama mkoa wa Lindi akifurahia daraja linalo ‘bembea’ ambalo ni moja kivutio kwa watalii wa nje ya nchi na ndani. |
![]() |
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Kemilembe Lwota akitembea juu ya daraja hilo. |
![]() |
Meneja Mawasiliano wa Tanapa,Pascal Shelutete naye hakua nyuma kutembea juu ya daraja hilo ambalo limeongeza shughuli za utalii kwenye hifadhi hiyo. |
![]() |
Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Mazingira wakiwa juu ya daraja maalumu lililojengwa kuwawezesha watalii kuwaona wanyama aina ya Viboko na aina mbalimbali za ndege. |
![]() |
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Japhet Hasunga akifurahia mandhari ya daraja linalomwezesha mtalii kuona vizuri eneo la Ziwa Manyara. |
↧
MAKONDA AZINDUA JENGO LA UPASUAJI DAR.
↧
WATANO WANUSURIKA KUUNGUA NA MOTO.
↧
MWALIMU AKAMATWA KWA KUTUMIA LUGHA YA MATUSI KWENYE MTANDAO.
↧
↧
RC MASENZA: WATENDAJI ACHENI SIASA KAZINI FANYENI KAZI ZA KIMAENDELEO KWA WANANCHI
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina masenza akiongea na maafisa watendaji wa wilaya ya kilolo kwa lengo la kuhimiza ufanyaji kazi wao kwa kutatua changamoto za wananchi na hatimaye wapate maendeleo
pichani ni baadhi ya maafisa watendaji wa vijiji,kata na tarafa waliohudhuria kikao hicho cha mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza
Na Fredy Mgunda, Iringa.
MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza amewataka watendaji wote wa serikali kuacha kufanya kazi kwa mihemuko ya kisiasa kwa kuwa linarudisha maendeleo nyuma.
Onyo hilo limetolewa wakati wa kikao na maafisa watendaji wa wilaya ya Kilolo,Masenza alisema kuwa imebuka tabia ya viongozi wa serikali kujihusisha na siasa wakati wa utendaji wao wa kazi hivyo kuanzia saizi zitaki kusikia siasa wakati wa kazi.
“Haiwezekani kila siku mnafanya siasa tu huko vijijini badala ya kutengeneza mpango kazi wa kimaendeleo ambao utakuwa na faida kwa taifa na wananchi wote hivyo kuanzia leo sitaki kusikia tena hiyo tabia” alisema Masenza
Masenza alisema serikali ya awamu ya tano inataka watu wafanye kazi hivyo wakati siasa hakuna tena kama kuna viongozi wanataka siasa wasubili wakati ukifika watafanya hizo siasa.
“Jamani rais wetu ameshasema kuwa huu sio wakati wa porojo za kisiasa huko makazini hivyo mnapaswa kufanya kazi na sio kupiga siasa fanyeni kazi kwa nguvu zote kuhakikisha mnatatua kero za wananchi katika maeneo yenu husika” alisema Masenza
Masenza alisema kama kuna mtendaji wa serikali anataka kufanya kazi za kisiasa basi hana budi kuachia nafasi yake ya kazi ili akaendelee kufanya kazi ya siasa na nafasi yake itajazwa na viongozi ambao wapo tayari kufanya kazi na serikali ya awamu ya tano.
Aidha Masenza aliwaagiza wakurugenzi wote mkoani Iringa kuwachukulia hatua za kisheria mara moja viongozi wa serikali watakuwa wanajishughulisha na maswala ya kisiasa la sivyo wao ndio watachukuliwa hatua kwa kufuata miongozo ya kiserikali inavyoagiza.
“ wakurugenzi mnawajua sana hawa watendaji hivyo ni lazima muwadhibiti kufanya siasa wakati wa kazi na mnatakiwa kuwa wakali pindi mtakapogundua kuwa wanafanya siasa makazini” alisema Masenza
Naye katibu tawala wa mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu alisema kuwa ameshatoa walaka unaonyesha majukumu ya watendaji wa serikali hivyo hategemee kuona kiongozi wa serikali akifanya siasa kazini.
“Jamani nimetuma na kuwa walaka wa majukumu yenu hivyo sitegemie mnakiuka la sivyo nitaanza kuwa sughulikia kiongozi mmoja mmoja ili nikomeshe tatizo la siasa makazini” alisema Ayubu
Ayubu aliwataka makatibu wa wilaya kufanya kazi kwa kufuata miongozo ya serikali la sivyo serikali haitafikia malengo ya kuleta maendeleo kwa wananchi kama ambavyo wamejipangia hivyo inapaswa kila mmoja anafanye majukumu yake kikamilifu ili kutimiza malengo ya serikali.
“Rais wa awamu ya tano DR John Pombe Magufuli hataki tufanye kazi kimazoea kama ambavyo ili kuwa awali saizi ni kazi tu hivyo ni lazima kufanya hivyo” alisema Ayubu
↧
DC MJEMA, AKAGUA UKARABATI MAJENGO SHULE ZA JANGWANI NA AZANIA, LEO. WALIMU NA WANAFUNZI WAMSHUKURU RAIS DK. MAGUFULI, WASEMA AKIAHIDI ANATEKELEZA
Mkuu wa wilaya ya Ilala Sopphia Mjema akipozi kwenye kitanda alipotembelea Shule ya sekonari ya Jangwani, kukagua maendeleo ya ukarabati wa majengo unaogharamiwa na serikali kwa maelekezo ya Rais Dk. John Maguduli katika shule hiyo na shule ya Azania, jijini Dar es Salaam, leo. DC Mjema alitumia kitanda hicho wakati akisoma katika shule hiyo miaka zaidi ya 30 iliyopita.
Mkuu wa shule ya Jangwani Geradine Mwaisenga akimpokea DC Mjema kuka alipowasili kwenye shule hiyo.
Mkuu wa Shule ya Jangwani Geradine Mwaisenga akieleza taarifa ya hali ya ukarabati wa majengo ya shule hiyo ulipofikia sasa ambapo amesema umekamilika kwa kiasi cha asilimia 90. Kulia ni Katibu Tawala wa Ilala Edward Mpogolo na katikati DC Mjema
Ofisa wa Wakala wa majengo akimpatia maelezo DC Mjema kuhusu mradi huo wa ukarabati wa vyoo kwenye majengo ya shule ya jangwani. Kulia ni Edward Mpogolo
Moja ya vyoo vilivyokarabatiwa kwenye shule hiyo ya Jangwani.
DC Mjema (kushoto) akizunguma alipokuwa akikagua chumba cha darasa kilichokarabatiwa
Mwalimu wa somo la fizikia wa kidato cha nne Felix Sameli akifundisha darasani muda mfupi kabla ya DC Mjema kuingia katika darasa la kidato hicho.
DC Mjema (kulia) akisalimiana na wanafunzinwa Kidato cha Nne katika shule ya sekondari ya Jangwani akiwa katika ziara hiyo ya kukagua maendeleo ya ukaranbati wa majengo
DC Mjengwa akiwa na mwanafunzi wa kidato hicho sabrina Saidi ambaye alikuta anakaa kwenye dawati alilokuwa akitumia wakati wakisoma katika shule ya Jangwani zaidi ya miaka 30 iliyopita.
DC Mjema akiwaonya wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari ya Jangwani kutojiingiza katika mambo ya utukutu ikiwemo kupata mimba wakiwa bado masomoni na badala yake wazingatie masomo kwa bidii.
DC Mjema akiongozwa na Mkuu wa shule hiyo kukagua mabweni ya wasichana yaliyokarabatiwa.
DC Mjema akihoji jambo alipokagua vyoo ambavyo ukarabati wake unaendelea katika shule hiyo.
"Hivi hii milango metengenezwa kwa mbao aina gani?" DC Mjema akahoji alipokagua ukarabati wa vyoo katika shule hiyo.
DC Mjema akijaribu kuhakikisha kama maji yanatoka kwenye bafu alipokagua ukarabati wa vyoo kwenye eneo la wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule hiyo ya Jangwani.
DC Mjema akionyeshwa sehemu ya wanafunzi kulia chakula ambayo bado ukarabati wake haujakamilika katika shule hiyo ya Jangwani.
baadhi ya wanafunzi wenye uhitaji maalum wakiwa darasani katika shule hiyo ya Jangwani.
DC Mjengwa na msafara wake wakitoka baada ya kufanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali katika shule hiyo ya Jangwani.
DC Mjengwa na msafara wake wakitoka baada ya kufanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali katika shule hiyo ya Jangwani.
DC Mjema kabla ya kuondoka akakagua ukarabati wa chumba cha maabara katika shule hiyo
"Sasa chumba kama hiki cha maabara kinatakiwa kuwa na umeme muda wote" akasema DC Mjema.
Ofisa wa wakala wa Majengo akitoa maelezo ya mwisho kabla ya kuondoka DC Mjema kwenye shule hiyo ya Jangwani.
DC Mjema akizungumza na waandishi wa habari alichoshuhudia na maoni yake baada ya kukagua ukarabati wa majengo kwenye shule hiyo ya Jangwani. " Nimerishwa sana na ukarabati uliofanyika, Walimu, wafanyakazi wa kawaida na wanafunzi hakikisheni mnaitunza miundo mbinu hii ilivyokarabatiwa na kuwa mizuri. namshukuru na kumpongeza Rais Dk. Magufuli kwa uamuzi wake wa kuielekeza serikali kukarabati shule hizi" Alisema DC Mjengwa.
DC Mjengwa akizungumza na wanafunzi aliowakuta wakijisomea kwenye viwanja vya shule ya Jangwani wakati akienda shule ya Azania kuendelea na ukaguzi wa ukarabati wa majengo pia katika shule hiyo.
DC Mjema akizungumza na wanafunzi katika shule ya Azania.
DC Mjema akiongozwa na Mkuu wa Shue ya Azania Erasto Gwimile (kushoto), kwenda kukagua maeneo mbalimbali ya majengo yaliyofanyiwa ukarabati katika shule hiyo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo (katikati) akiinama wakati wakienda kukagua ukarabati katika moja ya madarasa ya shule hiyo ya Azania.
DC Mjema akikagua vyoo vilivyokarabatiwa kwenye shue hiyo ya Azania.
DC Mjema akizungumza wakati akikagua mabweni katika shule hiyi=o ya Azania. Alishauri kuwekwa milango ya dharula kuwezesha wanafunzi kutoka kwa urahisi wakati wa majanga kama ya moto, badala ya kutegemea kutoka katka milango yenye vizuizi vingi kama mageti.
DC Mjema akimpa pole mwanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya Azania Enock Michael ambaye alimkuta amelala bwenini kutokana na kuwa na homa.
Mkuu wa shule ya Azania akitoa maelezo kuhusu ukarabati wa moja ya vyumba vya madarasa.
DC Mjema na msafara wake wakiendelea na ukaguzi
DC Mjema akiwa katika chumba cha darasa kwa ajili ya kuzungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Azania. Kulia ni Edward Mpologo na kushoto ni Mkuu wa shule hiyo Erasto Gwamile.
DC Mjema akizungumza nao
Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi wa Azania Goodlove Kapufi akizungumzia ukarabati wa majengo ya shule yao. " kwa niaba ya wenzangu tunamshukuru sana Rais Dk Magufuli kwa kuelekeza ukarabati huu ufanyike, tunasema asante sana," alisema. Makamu huyo wa Rais.
Katibu Tawala wa Ilala akimsalimia Makamu huyo wa Rais wa Serikali ya Wafnafunzi wa shule ya Azabia
Mkuu wa Shule ya Azania Erasto Gwimile akisoma taarifa ya hali ya ukarabati wa majengo ya shule, alisema ukarabati ulichelewa kukamilika kwa wakati hivyo kusababisha shule kuhelewa kufunguliwa.
DAS wa Ilala Mpogolo akiwa na Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Azania.
Mkuu wa Shule ya Azania akimshukuru DC Mjema kwa kutembelea shule yao
DC Mjema akizungumza na baadhi ya wanafunzi za shule ya zanaki wakati ameketi nao kwenye dawati
DC Mjema akiagana na Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Azania
DC Mjema akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi katika msafara wake na baadhi ya viongozi wa shule hiyo ya Azania kabla ya kuondoka mwishoni mwa ziara yake.
DC Mjema akiagana na Mkuu wa Shue ya Azania Erasto Gwamile baada ya ziara yake ya kukagua ukarabati wa majengo katika shule hiyo leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
↧
JEMBEKA NA KILIMO.
VIJANA 6 wilayani #igunga wanaolima kwa kikundi huku wakicheza ngoma, wanapiga mzigo balaa.
Baada ya mahojiano na #KAZINANGOMA niliwauliza, "kundi lenu linaitwaje....!!?" Wakasema ingawa wako kipindi kirefu katika kilimo wakilima mashamba ya wananchi kwa malipo ambayo kwayo wametengeneza ajira, lakini bado kundi lao hawajalipa jina....... Nikawaambia "Hamuwezi kwenda hivi hivi bila ya kuwa na jina la kundi watu watawatambuaje..!" Na ndipo wakanipa fursa niwachagulie jina.
Bila ajizi nikawabatiza kwa MAJI YA MOTO kundi lao nikalipa jina JEMBEKA NA KILIMO (ikiwa na maana 'fanya kilimo kama burudani ingawa inatupa pesa'.
Wao wanafurahia sana kazi hii, kuanzia saa moja asubuhi hadi saa tisa wanauwezo wa kulima hekari 4, na kwa kila hekari moja gharama ya kulima au kupalilia ni shilingi elfu 15,000/= top... Haina mjadala. .
Hivyo wana uhakika wa kutoka na Tsh 45,000/= kwa siku. .
Jeh huoni kuwa hii itahamasisha vijana wengi kuwekeza kwenye ajira za kilimo kuliko kubanana na ajira za maofisini?..........
CC:- @jembenijembe @paulmakonda @eddievied @gijegije @mansourjumanne @deejaykflip @prince_nzwalla @johnjackson_jj @djmike_beatz @chrissthedj @djscopion @deejay_jacko @mustafakinkulah @johangasa4 @harith_jaha
↧
LUKUVI AJA NA MAAMUZI HAYA JIJINI MWANZA
WANANCHI wanaomiliki nyumba 664 katika mitaa ya Kigoto na Kabuhoro katika Kata ya Kirumba Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza wametakiwa kuwa na subira wakati serikali ikitafuta ufumbuzi wa mgogoro uliopo kati yao na Jeshi la Polisi.
Pia wamezuiwa kujenga nyumba nyingine mpya kwenye maeneo ya mitaa yao na badala yake wawe walinzi na kuonya watakaothubutu kujenga hawatalipwa fidia ambapo awali walitakiwa kuondoka na kupisha eneo hilo baada ya kuandikiwa ilani ya siku saba na jeshi la polisi.
Akizungumza na wananchi hao Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alisema serikali imesikia kilio chao na hivyo amekuja chunguza mgogoro huo ili ifanye uamuzi wa kuutatua.
Amesema serikali inataka kufahamu mahitaji ya wananchi na polisi na kuonya wananchi wanaoishi kwenye maeneo hayo wasithubutu kujenga (kuongeza) majengo mengine zaidi ya yaliyopo sasa na watakaokaidi hawatalipwa fidia.
“Nimekuja kuangalia mgogoro huu na kuchungumza jambo hili ili serikali ifanye uamuzi. Msidhani nina majibu, majibu yatatolewa ndani ya mwaka mmoja lakini msituhubutu kuongeza nyumba zingine zaidi, kuweni walinzi wa maeneo haya na tunataka muwe maeneo mzuri ili tuwarasimishie,”alisema Lukuvi.
Waziri huyo wa ardhi alisisitiza baada ya uchunguzi atamshauri vizuri Rais John Magufuli namna ya kumaliza mgogoro huo baina ya wananchi na taasisi hiyo ya serikali.
Lukuvi alieleza eneo la Kigoto ambalo Polisi inadai inataka kujenga Chuo cha Polisi wanamaji, nyumba za askari, gati la boti na meli za doria zinaweza kujengwa popote lakini eneo hilo lazima lipangwe upya hata kama matumizi yakibadilishwa kwa kuwa haiwezekani watu waishi kwenye nyumba za hoovyo hovyo.
“Miaka 70 hadi leo kwa nini ujenzi haukuzuiwa,hakuna viongozi hapa na kama mngewashirikisha wangewasaidia kuzuia.Je, upembuzi yakinifu ulifanyika kwenye eneo mnalotaka kujenga mdomo huo wa gati la boti za polisi?
Aidha akizungumza kwa niaba ya wenzao ,Ferdinand Mtundubalo alimweleza Waziri kuwa hawana tatizo na ujenzi wa gati la boti za polisi isipokuwa warasimishiwe makazi yao ili waondokanane na mgogoro huo.
Katika hatua nyingine Waziri Lukuvi aliwataka wataalamu wa wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela waainishe eneo la Uwanja wa Ndege wa Mwanza na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikosi cha Ihale ili kila mmoja alinde eneo lake.
Pia alishauri eneo la Nyamwilolelwa litakalobaki baada ya kutengwa la uwanja wa ndege na JWTZ lipimwe wapewe wananchi wa eneo wapatao 1,961 na kuhusu barabara ya Mwanza –Igombe uamuzi wa Rais Magufuli ubaki ulivyo na uheshimiwe.
Pia wamezuiwa kujenga nyumba nyingine mpya kwenye maeneo ya mitaa yao na badala yake wawe walinzi na kuonya watakaothubutu kujenga hawatalipwa fidia ambapo awali walitakiwa kuondoka na kupisha eneo hilo baada ya kuandikiwa ilani ya siku saba na jeshi la polisi.
Akizungumza na wananchi hao Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alisema serikali imesikia kilio chao na hivyo amekuja chunguza mgogoro huo ili ifanye uamuzi wa kuutatua.
Amesema serikali inataka kufahamu mahitaji ya wananchi na polisi na kuonya wananchi wanaoishi kwenye maeneo hayo wasithubutu kujenga (kuongeza) majengo mengine zaidi ya yaliyopo sasa na watakaokaidi hawatalipwa fidia.
“Nimekuja kuangalia mgogoro huu na kuchungumza jambo hili ili serikali ifanye uamuzi. Msidhani nina majibu, majibu yatatolewa ndani ya mwaka mmoja lakini msituhubutu kuongeza nyumba zingine zaidi, kuweni walinzi wa maeneo haya na tunataka muwe maeneo mzuri ili tuwarasimishie,”alisema Lukuvi.
Waziri huyo wa ardhi alisisitiza baada ya uchunguzi atamshauri vizuri Rais John Magufuli namna ya kumaliza mgogoro huo baina ya wananchi na taasisi hiyo ya serikali.
Lukuvi alieleza eneo la Kigoto ambalo Polisi inadai inataka kujenga Chuo cha Polisi wanamaji, nyumba za askari, gati la boti na meli za doria zinaweza kujengwa popote lakini eneo hilo lazima lipangwe upya hata kama matumizi yakibadilishwa kwa kuwa haiwezekani watu waishi kwenye nyumba za hoovyo hovyo.
“Miaka 70 hadi leo kwa nini ujenzi haukuzuiwa,hakuna viongozi hapa na kama mngewashirikisha wangewasaidia kuzuia.Je, upembuzi yakinifu ulifanyika kwenye eneo mnalotaka kujenga mdomo huo wa gati la boti za polisi?
Aidha akizungumza kwa niaba ya wenzao ,Ferdinand Mtundubalo alimweleza Waziri kuwa hawana tatizo na ujenzi wa gati la boti za polisi isipokuwa warasimishiwe makazi yao ili waondokanane na mgogoro huo.
Katika hatua nyingine Waziri Lukuvi aliwataka wataalamu wa wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela waainishe eneo la Uwanja wa Ndege wa Mwanza na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikosi cha Ihale ili kila mmoja alinde eneo lake.
Pia alishauri eneo la Nyamwilolelwa litakalobaki baada ya kutengwa la uwanja wa ndege na JWTZ lipimwe wapewe wananchi wa eneo wapatao 1,961 na kuhusu barabara ya Mwanza –Igombe uamuzi wa Rais Magufuli ubaki ulivyo na uheshimiwe.
↧
↧
ZIMAMOTO NCHINI YAPATA TUZO YA UTENDAJI BORA YA MWAKA 2017
Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jesuald Ikonko (katikati) akiongea na Waandishi wa habari wa radio Times Fm wakati akitoa taarifa ya Mafanikio ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ya mwaka 2017, kabla ya kukabidhiwa Tuzo na Cheti cha heshima kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Times Fm, Bw. Rehure Nyaulawa (kushoto) kwa kutambua utendaji kazi wa Jeshi hilo, Matangazo hayo yalikuwa yakirushwa moja kwa moja toka Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema jana tarehe 26/01/2018.
Mkurugenzi Mkuu wa Times Fm, Bw. Rehure Nyaulawa (kushoto) akitoa pongezi na shukrani kwa Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jesuald Ikonko (katikati) wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo na cheti cha heshima kwa kutambua utendaji kazi wa jeshi hilo (kulia) ni Mkurugenzi wa vipindi Times Fm Bw. Amani Misana wakati wa Matangazo hayo yalikuwa yakirushwa moja kwa moja toka Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema jana tarehe 26/01/2018.
Mkurugenzi Mkuu wa Times Fm, Bw. Rehure Nyaulawa (kushoto) akimkabidhi Cheti cha heshima Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jesuald Ikonko (katikati) kwa kutambua utendaji kazi wa Jeshi hilo wakati wa Matangazo hayo yalikuwa yakirushwa moja kwa moja toka Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema jana tarehe 26/01/2018.
Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jesuald Ikonko akipokea Tuzo ya heshima toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Times Fm, Bw. Rehure Nyaulawa kutokana na utendaji kazi wa Jeshi hilo kwa jamii na Taifa kwa ujumla (kulia) ni Mkurugenzi wa vipindi Times Fm Bw. Amani Misana wakati wa Matangazo hayo yalikuwa yakirushwa moja kwa moja toka Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema jana tarehe 26/01/2018.
Picha ya Pamoja, Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jesuald Ikonko (wa nne kulia) akiwa na Viongozi Waandamizi wa Jeshi pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Times Fm, Bw. Rehure Nyaulawa (kulia kwake) na (kushoto kwake) ni Mkurugenzi wa vipindi Times Fm Bw. Amani Misana Matangazo hayo yalikuwa yakirushwa moja kwa moja toka Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam mapema jana tarehe 26/01/2018. (Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA - JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
↧
MWILI WA MAREHEMU LULU SYLVESTER MATTUNDA LEMA WAWASILI KIJIJINI NRONGA KWA MAZISHI
Marehemu Lulu Sylvester Mattunda Lema.(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Familia katika picha ya pamoja eneo la Korogwe Bararara ya Tanga
Waombolezaji wakiwa nyumbani hapo |
Sylvester Mattunda Lema (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na watoto wake mara baada ya kuwasili Nyumbani kwao katika Kitongoji cha Nkwelengya, Kijiji cha Nronga, Kata ya Machame Magharibi, Mkoa wa Kilimanjaro Wilaya ya Hai kwa taratibu za mazishi yatakayofanyika Leo Saa Nane Mchana, Januari 26, 2018 katika makaburi ya familia yaliyopo eneo hilo
Mwinjilisti wa Usharika wa Nronga, Donald Lema akizungumza jambo baada ya mwili wa marehemu, Lulu Sylvester Mattunda Lema ulipowasili katika Kitongoji cha Nkwelengya, Kijiji cha Nronga, Kata ya Machame Magharibi, Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro Januari 25, 2018 kwa taratibu za mazishi yanayofanyika leo Ijumaa Januari 26, 2018 saa Nane Mchana, katika makaburi ya familia yaliyopo eneo hilo, ambapo Lema alisema, "Katika mtihani huu ndugu yangu Sylvester,umeshinda katika ile ahadi uliyotamka ni kifo ndicho kitakacho tutenganisha mimi na wewe Lulu,hivyo ahadi hiyo umeitimiza.
"Profesa Lema pamoja na ndugu zako wote nachukua nafasi ya kuwapeni pole sana na Mungu akawatie nguvu, huyo aliyekufa maisha yake yamekwisha aliyebaki ndiye ameumia zaidi,wapo ndugu zetu waliokuwa Dar es Salaam ambao katika msiba huu walishughulika kufa kupona wahakikishe jambo hili limewezekana kama hivi lilivyowezekana.
Wapendwa niseme nivile tunauona msiba tukiusikia kwa mwingine, tumeona mwili umetufikia nyumbani,kutokana na msiba huu kuna watu wanashughulika kwa kujitolea kwa hali na mali, wapo wanaotoa matangazo wapo wanaofanya hili na lile kuhakikisha jambo linakwenda vizuri na wapo waliojitoa kwa hali na mali.
Na kwa wale waliotoka Dar es Sallam na kwa wale waliotoka ndani na nje ya nchi naomba
kuwashukuru sana kwaniaba ya ushirika wa Nronga kwa kufanya juhudi zote kuuleta mwili wa mpendwa hapa nyumba pia napenda kuwaambia mumtie moyo ndugu yenu pamoja na watoto na mumtegemee Mungu Kwa mioyo yenu yote, huu mwaka ni mwaka wa marejesho, atarejesha amani pasipo amani, atarejesha baraka pasipo baraka, atarejesha afya mahali afya imetoweka na huu mwaka nimzuri sana kwa anaemtegemea Mungu.
↧
KATIBU WA CCM KATA YA BUHALAHALA ATUHUMIWA KUTAFUNA KIASI CHA SH MILIONI 20
![]() |
Ofisi za kikundi cha wajasiliamali (KIWAGE) zilizopo mtaa wa Shilabela Mjini Geita zikiwa zimefungwa . |
![]() |
Mwenyekiti wa Mtaa wa Shilabela Bw,Elias Mtoni akielezea suala la vikundi ambavyo vimeonekana kuwa na dhana ya utapeli juu ya fedha za wajalisiamali . |
↧
MWANAUME ATUHUMIWA KUMUUA MKE NA MTOTO WAKE WILAYANI CHATO
![]() |
Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye eneo ambalo kumetokea tukio. |
![]() |
Jirani wa Familia ambapo kumetokea mauaji Bi,Mariam Shija akizungumza na waandishi wa habari kwa masikitiko juu ya tukio hilo. |
![]() |
Diwani wa Kata Minkoto , Bw Geroge Magezi akiwasisitiza wananchi kushiriana na jeshi la Polisi kwenye suala la ulinzi na usalama. |
↧
↧
LUKUVI AFUNGUKA KILE KITAKACHO WAKUTA WAMILIKI ARDHI WAKAIDI MKOANI MWANZA
Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi William Lukuvi ametangaza kiama kwa wamiliki ardhi ambao hawajalipa kodi ya pango la ardhi na kutoa muda hadi kufikia APRIL 30 mwaka huu kuhakikisha kuwa wanalipa kodi hiyo ambayo ipo kisheria na watakaoshindwa watafikishwa mahakamani ifikapo mwezi MAY mwaka huu.
↧
DKT. MWANJELWA AISHUKURU CHINA KWA KUONYESHA NIA YA KUISAIDIA TANZANIA KWENYE MAENDELEO YA TAFITI ZA KILIMO CHA MINAZI NA MIHOGO
Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akimweleza mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu namna ambavyo Kituo cha Utafiti Mikocheni kinavyochangia kwenye kuongeza tija na uzalishaji katika Sekta ya Kilimo kushoto kwa Dkt. Mwanjelwa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Dkt. Thomas Kashillilah
Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu katika moja ya maabara ya Kituo cha Utafiti Mikocheni
Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu wakimsikiliza Mkuu wa Idara ya Udhibiti wa Magonjwa ya Mimea Dkt. Deusdeth Mbanzibwa katika moja ya maabara ya Kituo cha Utafiti Mikocheni
Aina za mbegu mbalimbali za mihogo ambazo ni Sehemu ya matokeo ya tafiti zinazoendeshwa na Kituo cha Utafiti Mikocheni ambazo Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu walipata nafasi ya kujionea
Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu wakimsikiliza Mtafiti Mwandamizi wa Kituo cha Mikocheni Dkt Aloyce Kulaya ambaye amewaeleza faida za mbegu za mahindi ziligunduliwa Kituoni hapo kupitia Mradi wa WEMA
Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Dkt. Qu Dongyu wakimsikiliza Dkt. Christopher Materu Mkuu wa Idara ya Udhibiti wa Wadudu na Magonjwa kutoka Kituo cha Utafiti Mikocheni namna nzuri ya kudhiti magonjwa ya mimea kwa kutumia wadudu marafiki
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Dkt Mary Mwanjelwa ameishukuru Serikali ya China kwa kuonyesha nia ya kusaidia eneo la utafiti na maendeleo hususan kwenye kuendeleza zao la minazi na mihogo kupitia Kituo cha Utafiti wa Mazao cha Mikocheni JIJINI Dar es Salaam.
Dkt Mwanjelwa amemshukuru Serikali ya China kupitia Naibu Waziri wa Kilimo wa China Dkt Qu Dongyu mara baada ya kufanya ziara katika Kituo hicho mapema leo.
Katika Wasilisho lake kwa ugeni wa Waziri huyo wa Kilimo kutoka China, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Utafiti Mikocheni Dkt Fred Tairo amesema Kituo kimekuwa kikiendesha tafiti mbalimbali zenye lengo la kuzuia na kukabiliana na magonjwa hatari ya minazi na mihogo lakini kikwazo kikubwa kimekuwa teknolojia hafifu na uzoefu mdogo katika nyanja hiyo.
Mara baada ya wasilisho hilo Naibu Waziri wa Kilimo wa China ambaye anataaluma ya kilimo amesema Serikali ya China ipo tayari kuisaidia Tanzania kwenye maeneo ya utafiti wa kuzuia magonjwa ya mazao kwenye minazi na mihongo na kutoa wito kwa Watafiti wa Tanzania kuongeza juhudi katika kubunia teknolojia mbazo zitakuwa rahisi na rafiki kwa Wakulima wa Tanzania ili iwe rahisi kuziuza na baadae pato lake lisaidie Kituo hicho kujiendesha.
Dkt Qu Dongyu yupo nchini kwa ziara ya Kiserikali pamoja na Mwenyeji wake, Dkt Mary Mwanjelwa ambapo wote kwa pamoja wamepata nafasi ya kuitembelea maabara ya Kituo cha Utafiti Mikocheni na kujionea matokeo ya tafiti mbalimbali.
Akizungumzia kuhusu uwezeshaji wa Serikali ya China kwa Kituo cha Utafiti Mikocheni, Mtafiti Mwandamizi wa Kituo cha Mikocheni Dkt Aloyce Kulaya amesema kwa sehemu kubwa Kituo kimekuwa kikipata uwezeshaji kutoka Serikalini pamoja na Wabia wa Maendeleo kama Mfuko wa Bill and Belinda Gates Foundation na kuongeza kuwa uwezeshaji kama kutoka Serikali ya China utaongeza tija na uzalishaji katika mazao mengine si kwa minazi na mihogo tu.
Dkt Qu Dongyu anataraji kumaliza ziara yake ya Kiserikali hapo kesho kwa kukutana na Wawekezaji wa China waishio Tanzania na baadae atareje nyumbani siku hiyo ya Jumamosi.
↧
YAH:- SI KWELI KUWA TIMU YA TAIFA YA NGUMI INAISHI KWA CHAI NA CHAPATI.
↧