Quantcast
Channel: g sengo
Viewing all 12422 articles
Browse latest View live

ALLIANCE YAISULUBU PAMBA 2 0

$
0
0

Timu ya Alliance Fc ya jijini hapa imeendelea kujiweka mahala pazuri kutinga Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao, baada ya kuwafunga "TP lindanda Wanakawekamo'  Pamba Fc pia ya Mwanza, mabao mawili kwa nunge, katika mchezo wa Ligi Soka Daraja la Kwanza Tanzania Bara, uliopigwa ijumaa ya tarehe 26 mwezi January kwenye dimba la Nyamagana.

ETHIOPIA KUWAACHIA HURU MAELFU YA WAFUNGWA WA UPINZANI.

$
0
0
Ethiopia kuwaachia huru maelfu ya wafungwa wa upinzaniSerikali ya Ethiopia imetangaza kuwa itawaachia huru wafungwa waliotiwa nguvuni kufuatia machafuko ya mwaka 2015 na 2016 yaliyotokea katika eneo la Oromia.

Msemaji wa serikali ya Ethiopia, Addisu Arega Kitessa amesema kuwa wafungwa 2,345 wamesamehewa na wataachiwa huru siku chache zijazo.
Habari hiyo ya kusamehewa maelfu ya wafungwa nchini Ethiopia imetangazwa wiki moja baada ya kuachiwa huru kinara wa upinzani wa watu wa kabila la Oromo, Merera Gudina na wenzake 22 ambao makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema walikuwa wafungwa wa kisiasa. 

Watetezi wa haki za binadamu wanasema kuwa karibu wafungwa elfu mbili wa kisiasa wangali wanashikiliwa katika jela za Ethiopia.  
Kabla ya hapo Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn alikuwa ametangaza kuwa serikali yake itawaachia huru wafungwa wa kisiasa ili kujenga maridhiano ya kitaifa na kupanua demokrasia nchini humo.





Hailemariam Desalegn

Gudina alikamatwa mwaka 2016, baada ya kukosoa rekodi mbaya ya haki za binadamu ya serikali ya Addis Ababa na hali ya kisiasa nchini Ethiopia.
Askari usalama wa serikali ya Ethiopia wamekamata makumi ya maelfu ya watu na kuua waandamanaji zaidi ya 900 tangu yalipoanza maandamano ya watu wa Oromo waliokuwa wakipinga unyakuzi wa ardhi zao, ukandamizaji wa kisiasa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na vyombo vya dola. 

UZINDUZI KAMPENI ZA CCM UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE KINONDONI ZAWAVUTIA WENGI.

$
0
0
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba (kushoto), akimnadi kwa wananchi mgombea ubunge Jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo viwanja vya Biafra, Dar es Salaam leo. 
Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia akiwasalimia wananchi mara baada kutambulishwa na kuitwa jukwaani kumwaga sera zake za kuomba kura wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo kwenye viwanja vya Biafra, Dar es Salaam leo. 
Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia akizungumza mambo mbalimbali mbele ya Wanachama wa chama hicho na Wananchi kwa ujumla mara baada kutambulishwa na kuitwa jukwaani kumwaga sera zake za kuomba kura wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo kwenye viwanja vya Biafra, Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kimara Chadema, Ngudu Pascal Manota akiwasalimia wananchi wa Kinondoni jioni ya leo alipokuwa akitambulishwa kwao na kurudisha kadi ya chama hicho na kujiunga na CCM,pichani kati ni Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa kampeni za chama cha CCM, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba na kulia kwake ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,Stephen Wasira
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kimara Chadema, Ngudu Pascal Manota akirudisha kadi ya chama hicho na kujiunga na CCM,Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa kampeni za chama cha CCM, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba akiitazama kadi hiyo kwa makini
Aliyekuwa mjumbe wa bodi ya wadhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Muslim Hassaanal ambaye hivi karibuni alihamia CCM,akimwombea kura za ushindi Mgombea Ubunge wa jimbo la Kinondoni ,Maulid Mtulia wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo kwenye viwanja vya Biafra, Dar es Salaam leo. 
Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa kampeni za chama cha CCM, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba akizungumza mbele ya umati wa watu waliofika kuhudhuria uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo kwenye viwanja vya Biafra, jijini Dar es Salaam leo. 
Baadhi ya wananchi na wafuasi wa chama cha CCM wakishangilia wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo,katika viwanja vya Biafra Kinondoni jioni ya leo.
Baadhi ya wananchi na wafuasi wa chama cha CCM wakisikiliza kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la uzinduzi wa kampeni Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo la Kinondoni,mapema leo jijini Dar.PICHA NA MICHUZI JR.

MKAZI WA JIJI LA MWANZA AJISHINDIA MILIONI 40 ZA TATUMZUKA

$
0
0
 Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ilemela,Khadija Nyembo akimkabidhi mfano wa hundi  mkazi wa Buswelu,Ilemela,jijini Mwanza, Gibson Gratian Erasms,aliyejishindia kitita cha shilingi milioni 40 kwenye mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka uliofanyika jumapili iliyopita (Jackpot ya Jumapili).
 Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ilemela,Khadija Nyembo akiwa katika picha ya pamoja na Mkazi wa Buswelu,Ilemela,jijini Mwanza, Gibson Gratian Erasms,aliyejishindia kitita cha shilingi milioni 40 kwenye mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka uliofanyika jumapili iliyopita (Jackpot ya Jumapili),sambamba na baadhi ya viongozi wa Ofisi ya Wilaya na pamoja na ndugu wa mshindi huyo.

MANSOOR ATINGA JIMBONI KWAKE.

$
0
0

TAREHE 29.01.2018

NA ZEPHANIA MANDIA WA G.SENGO TV

MHE.Shanif Mansoor Mbunge wa Jimbo la Kwimba, leo amemtembelea Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Mtemi Msafiri wakati akiwa katika ziara zake jimboni humo  na kufanya kikao kukutana na kamati ya ulinzi na usalama.

 Mwenyekiti wa kikao hicho cha ndani ambaye ni mkuu wa wilaya husika Mhe. Mtemi Msafiri ataja moja ya malengo ya kuketi kwao katika meza moja ni kujadili namna ya kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa jimbo la Kwimba na kuzitolea maazimio, pamoja na kuhakiki utekelezaji wa maazimio yaliyopita.


Mbunge wa Jimbo la Kwimba Shanif Mansoor.
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mtemi Msafiri akisalimiana na mzee wa Jimbo.
Mbunge wa Jimbo la Kwimba Shanif Mansoor akisalimiana na mmoja wa wazee wilayani humo.
Makaribisho yakifanyika ndani ya ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mtemi Msafiri kabla ykutia saini kitabu cha wageni. .
Mbunge wa Jimbo la Kwimba Shanif Mansoor akitia saini katika kitabu cha wageni ndani ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Kwimba Mtemi Msafiri akiongoza kikao cha Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya yake akiwemo mbunge wa Jimbo hilo Shanif Mansoor aliyeketi kuia kwa Mkuu wa wilaya.
Shanif Mansoor Mbunge katika picha ya pamoja na kamati.
Shanif Mansoor Mbunge katika picha ya pamoja na kamati.

MPINA AAGIZA VIWANDA VYA SAMAKI KANDA YA ZIWA VICTORIA KUANZA KAZI IFIKAPO JULAI MWAKA HUU.

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina(mwenye miwani ) akishirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Vincent  Anney na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Bi Anarozy Nyamubi kuteketeza nyavu haramu zilizokamatwa na kikosi kazi  maalum alichokiunda hivi karibuni katika wilaya ya Musoma kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi, Emanueli Bulayi akishuhudia tukio hilo leo.(Na John Mapepele)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Joelson Mpina akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Anarozy Nyamubi baada ya kuteketeza nyavu haramu katika Wilaya ya Butiama leo. (Na John Mapepele)
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Vincent  Anney akimwaga mafuta kwenye nyavu haramu ili kuzichoma moto katika kijiji cha Bwai Kumusoma wilayani Musoma leo. (Na John Mapepele)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Bwai Kumusoma wilayani Musoma leo ambapo alishiriki zoezi la kuchoma nyavu haramu zilizokamatwa na kikosi kazi  cha kudhibiti uvuvi haramu Kanda ya Ziwa Victoria  alichokiunda hivi karibuni, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Vincent  Anney akisoma majina ya  Wavuvi Haramu (Na John Mapepele)

Asisitiza operesheni ya kutokomeza uvuvi haramu kanda ziwa ni  ya kudumu
Na John Mapepele, Mara
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameagiza viwanda vinne vya kuchakata samaki na mazao yake vilivyofungwa  katika  Mikoa ya Mwanza na Mara kuanza kazi mara moja ifikapo Julai Mosi mwaka huu, ambapo amewataka wamiliki kupeleka mipango kazi ya namna ya kuvifufua  kabla ya  kufikia mwezi Machi mwaka  wizarani kwake.

 Alivitaja viwanda hivyo kuwa ni Tan Perch Limited na Supreme Perch Limited vilivyopo Mwanza na  Mara Fish Packers Limited na Prime Catch Limited  katika mkoa wa Mara.

Waziri Mpina alizungumza hayo jana wakati alipokuwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Mara na Mwanza kukagua operesheni maalum ya kutokomeza uvuvi haramu kanda ya Ziwa Victoria inayofanywa na kikosi kazi maalum alichokiunda hivi karibuni.

“Mimi kama Waziri mwenye dhamana ya Sekta ya Uvuvi nchini niliyepa kulinda raslimali za uvuvi nitahakikisha kwamba  ulinzi wa raslimali hizi ni wa kudumu, na usio na mwisho hadi uvuvi haramu utakapoisha  hapa nchini” alisisitiza Mpina
Waziri Mpina alipata fursa ya kuzungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mara na Kamati ya Ulinzi ya Mkoa huo, wananchi katika maeneo tofauti na hatimaye kushiriki katika zoezi la kuchoma nyavu haramu ambapo hadi sasa zaidi ya nyavu zenye thamani ya shilingi bilioni nne zimechomwa moto katika zoezi linaloendelea la kudhibiti uvuvi haramu mkoani Mara.

Kamanda anayeongoza kikosi cha kupambana na kudhibiti uvuvi haramu na utoroshaji wa mazao ya uvuvi Kanda ya Mara, Bakari Lulela alimweleza Waziri Mpina kuwa operesheni hiyo imefanyika katika Wilaya za Musoma, Butiama, Rorya na Bunda na kufanikiwa kukamata na kuteketeza zana haramu zenye thamani ya sh. bilioni 3.2 huku wavuvi na wafanyabiashara wa samaki na mazao yake waliokiuka sheria ya uvuvi wakitozwa faini ya sh. milioni 189.

Waziri Mpina aliziagiza mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua Maafisa Uvuvi wa  Kijiji cha Bwai Kumsoma waliotuhumiwa kushirikiana na wavuvi haramu kuondolewa mara moja katika kijiji hicho ili kupisha uchunguzi na ikithibitika wachukuliwe hatua kali kwa mujibu wa sheria.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dk. Vincent Anney amesema kwamba hayuko tayari kuona Wilaya yake inaendelea kuishi na watumishi wanaojihusisha na uvuvi haramu  na kwamba sheria kali zitachukuliwa dhidi yao ikiwa ni pamoja na kuwaondoa katika wilaya hiyo.

Aidha Waziri Mpina ameiagiza Wizara yake kuandaa bei elekezi ya kununua samaki itakayowezesha kuondokana na tabia ya wenye viwanda kushusha hovyo bei pindi samaki wanapoongezeka na hivyo kuwadhulumu wavuvi kupata malipo stahili yanayotokana na kazi yao.

Waziri Mpina alisema Ziwa Victoria ni hazina na raslimali kubwa kwa Tanzania ambapo inaaminika kuwa  ni la kwanza kwa ukubwa katika bara la Afrika kwa kuwa na eneo la 68,000Km2  na la pili duniani.

Alisema  pamoja  na umuhimu wa ziwa hili katika kukuza uchumi na kuboresha maisha ya watanzania bado linakabiliwa na shughuli za uvuvi haramu uliokithiri ambapo tafiti zinaonyesha kwamba kama hakutakuwa na jitihada za haraka za kutokomeza uvuvi haramu, ziwa hilo hali halitakuwa  na raslimali za uvuvi ikiwa ni pamoja na samaki katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Alitaja uvuvi haramu unaofanywa kuwa  ni pamoja na kuvua katika maeneo yasiyoruhusiwa, kutumia valiyombo visivyosajiliwa, kuvua bila leseni,kutumia sumu, kutumia nyavu za utali na kuvua samaki wachanga ama wazazi wasioruhusiwa.
Uvuvi haramu mwingini nikuvua kwa kokoro na  nyavu zenye macho madogo chini ya kiwango kinachokubalika kisheria, katuli, kumbakumba na gizagiza ambapo alisema Serikali imedhamilia kutokomeza  uvuvi huo haramu.

Aidha alisema operesheni hiyo katika kanda ya Ziwa Victoria dhidi  ya uvuvi  haramu ni ya kudumu na inafanyika kwa kuzingatia Sheria ya Uvuvi Na.22 yaMwaka 2003 na Kanuni 58(1) ya Uvuvi ya Mwaka 2009 na Sheria ya Mazingira Na 20 ya Mwaka 2004 kifungu Na(1), 65(1)a pia Sheria ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Na 29 ya Mwaka 1994 ili kudhibiti uvuvi haramu ulioshamiri kiasi cha kutoweka kwa raslimali ya samaki katika ziwa hilo kwa faida ya vizazi vya sasa na baadaye.

Waziri Mpina alisema Tanzania inamiliki 51% ya Ziwa hili ikifuatiwa na Uganda 43% na nchi ya Kenya inamiliki 6%. Ziwa hili ni moja ya maziwa yanayozalisha samaki kwa wingi duniani kwa makadirio ya takribani tani 1,000,000 kwa mwaka  ambapo asilimia 60 ya uzalishaji wa samaki wake unatoka Tanzania hivyo juhudi za pamoja za kutokomeza uvuvi haramu zinahitajika.

RAIA WA NIGERIA ANASWA BONGO AKIWA NA MADAWA YA KULEVYA.

$
0
0
Dar es Salaam. Polisi Kikosi cha Viwanja vya Ndege jijini Dar es Salaam linamshikilia raia wa Nigeria akituhumiwa kupatikana na dawa za kulevya aina ya Cocaine.

Christian Ugbechi (26), anadaiwa kukamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa kwa Julius Nyerere (JNIA) akiwa na pipi 59 zenye uzito wa zaidi gramu 800.

Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, Matanga Mbushi amesema leo Jumatatu Januari 29,2018 kuwa mtuhumiwa anaishi na kufanya kazi nchini Ufaransa.

Amesema alikuwa akisafirisha dawa hizo za kulevya kwenda nchini Ufaransa.

"Tumemkamata mtuhumiwa akiwa na pipi 59, kati ya hizo 56 alizificha kwenye soksi na tatu amezitoa leo kwa njia ya haja kubwa. Yupo chini ya uangalizi maalumu,” amesema Mbushi.

KUTOKA TANGA BASI LATEKETEA KWA MOTO.

$
0
0

Basi la kampuni ya Tahmeed ambalo linafanya safari zake kutoka Dar es Salaam kwenda Mombasa Nairobi limeteketea moto katika kijiji cha Matumbi mkoani Tanga leo.


Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Benedict Wakulyamba amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ya moto na kusema kuwa hakuna abiria ambaye amepata madhara na moto huo ulioteketeza basi hilo.

"Ni kweli basi hilo limewaka moto leo, ila hakuna abiria aliyejeruhiwa wala kupata madhara yoyote kwa kuwa dereva alipoona dalili za moto alipaki gari pembeni na abiri ambao walikuwepo kwenye basi hilo kama 15 hivi wote waliweza kushuka mapema kabla ya moto kushika gari zima" alisema Wakulymba

VIDEO:- DR. SLAA KWA MARA YA KWANZA USO KWA USO IKULU NA JPM

$
0
0
Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi mteule, Dk Willibrod Slaa, Ikulu Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Januari 29, mwaka 2018 na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa imesema Dk Slaa amemshukuru Rais kwa kumteua kuwa Balozi na kuahidi kuwa yupo tayari kutekeleza majukumu atakayopangiwa kwa kutanguliza maslahi ya Taifa.

Imeeleza kuwa Dk Slaa ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa uongozi bora na kutekeleza mambo makubwa ikiwemo miradi ya ujenzi wa reli ya kisasa, ujenzi wa daraja la juu katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela, mradi wa uzalishaji umeme katika maporomoko ya mto rufiji na mapambano dhidi ya rushwa.


“Kwa kweli naona faraja, ninafurahi Serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza hatua kwa hatua karibu yote tuliyokuwa tunayapigania kwa miaka takribani 20 ya huko nyuma, mimi Dk Slaa nilikuwa napiga kelele kwa sababu nilikuwa naona kuna upungufu,” imesema taarifa hiyo ikimnukuu Dk Slaa.

Kwa upande wake, Rais Magufuli amempongeza daktari huyo kwa moyo wake wa kizalendo na amesema aliamua kumteua kuwa Balozi kwa kuwa anatambua ataweza kupigania maslahi ya Tanzania popote atakapopangiwa kuiwakilisha.

“Dk Slaa alinijulisha kuwa anakuja na akaomba akija angependa kuja kuniona na nikampangia leo, tumezungumza mambo mengi na ameniahidi kuwa atakwenda kufanya kazi yake vizuri kwenye nchi atakayokwenda kuwa Balozi,” amesema Rais Magufuli na kuongeza,

“Mheshimiwa Dk Slaa ni mtu safi, anazungumza kutoka moyoni na anaipenda Tanzania na mimi kutokana na moyo wake wa kuchukia ufisadi na kuchukia wizi nikaamua kumteua kuwa Balozi.”

Wakati huohuo, Rais Magufuli ameagana na maofisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambao wamestaafu baada ya kutimiza umri.

Walioagana na Rais ni Luteni Jenerali James Mwakibolwa aliyekuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ na Meja Jenerali Michael Isamuhyo aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Wengine ni Brigedia Jenerali Aron Lukyaa, Brigedia Jenerali Willima Kivuyo, Brigedia Jenerali Elizaphani Marembo na Kanali Peter Samegi.

KESI ZA MAHAKAMA NCHINI SASA KUENDESHWA KWA NJIA YA MTANDAO WA SIMU NA KOMPYUTA.

$
0
0


  Katika maadhimisho ya wiki ya sheria nchini, wadau wa sheria na mahakama mkoa wa Mwanza wamesema ukuaji wa teknolojia na kuanzishwa kwa mfumo wa Tehama, kutasaidia uharakishwaji wa kusikiliza mashauri ambayo yamekuwa yakilundikana kutokana na mfumo wa usikilizwaji wake wa kianalojia unaotumika sasa.


WAJASILIAMALI WATAKIWA KUJENGA UCHUMI WA TANZANIA

$
0
0
Mkurugenzi wa Uendeshaji  wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bathow Mmuni ambaye alikuwa mgeni rasmi akifunga mfunzo ya wajasiliamali yaliyoendeshwa na Sido mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Mkurugenzi wa Sido Dar es Salaam, MacDonald Maganga. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mkurugenzi wa Uendeshaji  wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bathow Mmuni akiwa ameshika chaki iliyotengenezwa na wajasiliamali waliokuwa waliopata mafunzo ya Sido-Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Uendeshaji  wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bathow Mmuni akionyeshwa nguo ya batiki iliyotengenezwa na wajasiliamali waliokuwa waliopata mafunzo ya Sido-Dar es Salaam. Pemnei kushoto ni
Mkurugenzi wa Uendeshaji  wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bathow Mmuni akionyeswa mafuta na sabuni walizotengeneza wajasiliamali waliopata mafunzo ya Sido-Dar es Salaam.  Pembeni ni Mkurugenzi wa Sido Dar es Salaam, MacDonald Maganga.

Mjasiliamali Suleiman Nassoro Mohamed ambaye ni Katibu wa BAKWATA akisoma risala wakati wa hafla ya kuhitimu mafunzo.
Baadhi ya wajasiliamali wakipatiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo.
Wajasiliamali wakiwa katika picha ya pamoja. --- Wajasiliamaji watakiwa kuendelea kutengeneza bidhaa zenye ubora ili kuweza kujenga uchumi wa Tanzania. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji NSSF, Bathow Mmuni wakati akifunga mfunzo ya Sido yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam ambapo aliwataka wajasiliamali kuendelea kuwa wabunifu kwa kutenegeza bidhaa zenye ubora. "Nawaomba wajasiliamali mtengeneze bidhaa zenye ubora na nzuri zitakazowavutia wateja ili mtakapoziuza zitachangia pato la taifa kukua zaidi," alisema Mmuni. Aliongeza kuwa kwa sasa NSSF wamejipanga kurudi kuanza kuwasaidia wajasiliamali ili kukuza kipato chao ili waweze kuendeleza uchumi wa viwanda. Kwa upande wa Mkurugenzi wa Sido- Dar es Salaam, MacDonald Maganga aliwaomba wajasiliamali wote walipo mtaani kuchangamkia mafunzo ya Sido ili yaweze kuwaongezea ujuzi na kuzifanya bidhaa zao zikawa na thamani zaidi. "Wajasiliamali jitokezeni kokote pale mlipo mchangamkie mafunzo tunayoyatoa maana yamekuwa yakiwajenga zaidi kwa kuongeza ubora wa bidhaa mnazozitengeneza, ukiangalia katika kundi lenu hili kuwa watu wameshaanza kutengeneza bidhaa ila wamekuja kujiongezea ujuzi zaidi jambo ambao ni jema zaidi maana unapopata cheti cha Sido kitakusaidia kuweza kupenya katika soko," alisema Maganga.

LIVE: KUAPISHWA KWA ODINGA BAADHI YA VITUO VYA HABARI VYAZIMWA NA SERIKALI KWA MUDA USIOJULIKANA.

$
0
0

LIVE COVERAGE: NASA's 'Swearing In'

SERIKALI YATANGAZA MWAROBAINI WA FAO LA KUJITOA.

$
0
0
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Walemavu, Antony Mavunde aelezea mbadala wa fao la kujitoa linaloliliwa na baadhi wa wanachama wa mifuko ya jamii. Mavunde ameyasema hayo wakati serikali ikipanga kuwasilisha bungeni Muswada wa Sheri ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa mwaka 2017 unaotalajiwa kujadiliwa na kupitishwa katika mkutano wa kumi unaoanza Januari 30, mwaka huu.J

JINSI YA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME NA KUONDOA UCHUNGU KWA ALOVERA

$
0
0

Alovera inapoliwa mara kwa mara na uchungu wake huweza sababisha madhara katika figo, hivyo bas! unapochanganya mseto kama ulioona kwenye video husaidia kupunguza makali ya uchungu. dawa hiyo inaweza kutibu magonjwa mengi ikiwemo nguvu za kiume, jaribu uone matokeo yake.

GLOBAL FUND YATOA TRIONI MOJA KWA TANZANIA KUSAIDIA UKIMWI, TB NA MALARIA

$
0
0

 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Makamu wa Rais (Sera na Uratibu), Profesa Faustine Kamuzora (kulia), na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamisi Shaaban, wakisaini hati za makabidhiano ya sh. trioni moja zilizotolewa na Shirika la Global Fund kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kusaidia mapambano ya Ukimwi, TB na Malaria katika hafla iliyofanyika Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam leo. Wengine waliosimama katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  na viongozi wengine kutoka Global Fund.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk. Mpoki Ulisubisya, akizungumza katika hafla hiyo.

Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania, Frederic Clavier, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mnufaika wa Global Fund, Joan akielezea jinsi alivyo nufaika na shirika hilo.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wanaishi na VVU-Ukimwi, Mwinuka Juastine, akizungumza.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamisi Shaaban (kulia), akimkabidhi hati ya makabidhiano Mwakilishi wa Global Fund Tanzania, Linden Morrison.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Makamu wa Rais (Sera na Uratibu), Profesa Faustine Kamuzora, akizungumza.
Taswira ya ukumbi wa mkutano katika uzinduzi huo.


Na Dotto Mwaibale

SHIRIKA la Kimataifa la Global Fund limetoa shilingi trioni moja kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya mapambano ya magonjwa ya ukimwi, malaria na kifua kikuu kwa mwaka 2018-2020. 

Akizungumza katika hafla ya kutiliana saini makabidhiano ya fedha hizo baina ya mfuko huo na serikali Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema fedha hizo ni muhimu sana kwa nchi yetu.

Alisema fedha hizo zitaelekezwa katika kupambana na magonjwa hayo ambapo kwa ugonjwa wa ukimwi zimetolewa sh.bilioni 769, TB sh. bilioni 67 wakati malaria sh.bilioni 320.

Alisema fedha hizo zitatumika kikamilifu kwa lengo lililokusudiwa na zitasimamiwa  na Ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Afya na Mashirika Yasiyo ya kiserikali.

Alisema katika masuala ya ukimwi zitatumika kwa ajili ya vipimo, dawa za kurefusha maisha na kufubaza virusi kwa wagonjwa wa ukimwi na katika ugonjwa wa malaria fedha hizo zitatumika kwa ajili ya vipimo na matibabu pamoja na kununua vyandarua.


"Kwa upande wa wagonjwa wa TB ni asilimia 40 tu ndio waliofika kwenye vituo vya afya na kuthibitika kuwa na maambukizi na wamepatiwa matibabu lakini tunataka hadi ifikapo mwaka 2020 tunataka asilimia 70 ya watanzania watakaogundulika kuwa na maambukizi wajulikane na wapatiwe matibabu" alisema Ummy.

Ummy aliongeza kuwa kati ya wagonjwa 100 wenye maambukizi ya TB wagonjwa 90 waliothibitika kuwa na maambukizi walitibiwa na kupona kabisa.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy amewataka Katibu Mkuu wa Wizara yake, Tamisemi na Ofisi ya Rais kuhakikisha wanazisimamia vizuri fedha hizo ili kupata matokeo mazuri waliyo yakusudia.

Mratibu wa Watu Wanaotumia Dawa za Kulevya Tanzania (TANPUD), Happy Assan alisema mradi huo utawasaidia sana na kuhakikisha hawataathirika ukizingatia kuwa fedha hizo zitawafikia walengwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wanaishi na VVU-Ukimwi, Mwinuka Juastine alisema mradi Global Fund imewasaidia waathirika 900,000 kwa kuwapa dawa za kupunguza makali ya ukimwi ARV na kufubaza virusi vya ugonjwa huo.

NI IGUNGA WILAYA YA MFANO KATIKA MAPINDUZI YA ZAO LA PAMBA MSIMU HUU WA KILIMO.

$
0
0


WAKULIMA KUPIGWA MSASA JUU YA UVUNAJI PAMBA.
Na Albert G. Sengo,Igunga
Mkuu wa wilaya ya Igunga John Mwaipopo amesema kuwa halmashauri yake kushirikiana na bodi ya Pamba nchini (TCB) mnamo mwezi Machi watatoa semina elekezi ya uvunaji wa zao la Pamba ili kupata stahiki katika ubora.

Mwaipopo ametanabaisha hayo mbele ya wandishi wa habari waliofanya ziara wilayani mwake kujioneo yanayojiri.

“Kumekuwa na changamoto kubwa sana nyakati za mavuno, kwa wakulima wa wilaya yangu kuchuma Pamba pamoja na mashina yake, kitendo ambacho hakikubaliki kwani huondoa sifa ya ubora wa zao hilo katika soko la dunia”

Ameongeza kuwa kupitia kampeni ya kuhamasisha kilimo cha Pamba waliyoifanya na mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Wandry imeweza kuongeza idadi ya wakulima wa zao hilo wanaotoka ndani na nje ya wilaya, kiasi kwamba hata wananchi wa mikoa ya mbali nao wamemiminika kukodisha mashamba na kufanya kilimo cha ‘Dhahabu nyeupe’.

“Sisi Igunga bado tuna ardhi kubwa sana wananchi wetu wanalima hapa lakini bado tunawakaribisha wananchi kutoka maeneo mengine, ninazo taarifa kuna wakulima hapa wametoka mpaka Dar es salaam na maeneo mengine wao wamekuja kwakuwa wameiona fursa na kuichangamkia”

“Kwa miaka miwili hii kumekuwa na mwanga mkubwa wa mafanikio na kuona wapi tunaelekea, mfano Mwaka jana tulipata kilogramu milioni kumi la laki saba na mwaka mmoja kabla yaani mwaka juzi tulipata kilogramu milioni 11 hiyo ni kwasababu mwaka jana kumekuwa na hali ya ukame unao shindana mwaka hadi  mwaka, sasa kwa hali ilivyo sasa nikimaanisha mvua za kutosha, hamasa ya wakulima wengi kujitokeza naiona Igunga ikipaa na kuishangaza nchi katika mavuno” Aliongeza Mwaipopo.

Kwa mujibu wa Mwaipopo mpaka sasa wilayani Igunga kuna kata 17 na vijiji 54 vinalima zao la Pamba.

Kwa upande wake mkaguzi mwandamizi wa zao la Pamba wilayani hapa George Kihimbi amesema kuwa uhamasishaji mkubwa uliofanywa kwa msimu wa kilimo 2017-2018, wamedhamiria kulima jumla ya hekari 110,000.

Katika hatua nyingine licha ya kuipongeza Serikali kwa kuwapatia mbegu na madawa kwa wakati pia ameiomba Serikali/Bodi ya Pamba, kupitia maafisa wake na mawakala kurejea tena kwenye maeneo hayo na kuwaongezea dawa kwani daadhi yao walikiuka masharti na kulazimika kuzigawa na kuzielekeza dawa za awali kwenye mahindi ili kuyanusuru na wadudu waharibifu waliolivamia zao hilo.

“Mwaka huu tunategemea kuzalisha Tani laki 6 tofauti na Mwaka jana ambapo zilipatikana Tani laki 130,000 ambazo pia tuliona zimeongezeka tofauti na miaka iliyotangulia”  Alisema Kihimbi. 

Kwa mujibu wa Bodi ya Pamba nchini Tanzania jumla ya  hekari milioni 1.5 tayari zimeshalimwa pamba tofauti na msimu uliopita ambapo ni hekari laki 6na59 elfu ndizo zilizolimwa zao hilo. 

KUHUSU FURSA MBALIMBALI ZITAKAZOPATIKANA WILAYANI HUMO MARA BAADA YA ZAO HILO KUSHAMIRI NA IWAPO WAWEKEZAJI WATASIMIKA VIWANDA, FUATILIA SIMULIZI KUPITIA VIDEO HAPO JUU.

AKSANTE.

SUMAYE, SOSOPI WAMNADI MWALIMU LEO.

$
0
0


Mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema, Salum Mwalimu amewaomba wananchi wa Kinondoni kumchagua awahi mkutano wa Bunge la bajeti utakaoanza Aprili, mwaka huu ili awasilishe hoja za maendeleo.

Amesema hayo leo Jumanne Januari 30,2018 alipohutubia mkutano wa kampeni Magomeni Morocco wilayani Kinondoni.

“Msifanye makosa siku ya uchaguzi, waacheni hao wengine wapige kelele. Mkimchagua mbunge dhaifu mtaendelea kubaki dhaifu katika kipindi cha miaka mitano,” amesema Mwalimu.

Amesema yeye ni mfuatiliaji  wa masuala ya  fidia na atakapokuwa mbunge, wananchi wa Kinondoni hawatapata shida kwa kuwa anajua kunusa zilipo fedha kwa ajili ya maendeleo.

Mkutano huo pia ulihutubiwa na viongozi mbalimbali wa Chadema, akiwemo mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Pwani na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye; mwenyekiti wa Baraza la Vijana la chama hicho (Bavicha), Patrick ole Sosopi na mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea.

KUNDI KUBWA LA FISI LAVAMIA KIJIJI.

$
0
0


WANANCHI wa Kata ya Inyeze wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamelalamika kwa diwani wa kata hiyo kwa kuvamiwa na kundi kubwa la fisi  kijijini.

Hayo yamesemwa katika kikao cha baraza la madiwani na Diwani wa kata hiyo, Lucas Makulumo, ambaye alisema fisi hao wanaonekana muda wote wa mchana na usiku.

Diwani Makulumo alimtaka Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Abel Shija, aeleze halmashauri ina mpango gani juu ya wanyama hao waliovamia kata yake na kuhatarisha maisha ya wananchi wake.

Aidha diwani huyo alilieleza  baraza hilo kuwa matukio ya wanyama hao kuvamia maeneo ya kata yake yamekuwa ya kawaida, hali inayowatia  hofu wananchi wake, wakiwamo watoto wanakwenda shule. Akijibu malalamiko hayo, Mwenyekiti  Shija alisema alikubaliana na diwani huyo kuwa jambo hilo ni hatari na kuagiza hatua zichukuliwe mapema.

Alimuagiza mkurugenzi kuhakikisha anawatumia wataalamu wa  maliasili na wanyamapori kuhakikisha wanyama hao kuondolewa na kuhakikisha hawaleti madhara kwa wananchi.

MTULIA AZIDI KUTIKISA KINONDONI

$
0
0

Image may contain: one or more people, people on stage, crowd and outdoor

Mgombea Ubunge katika jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya CCM Maulid Said Mtulia akinadi sera zake jukwaani na kuomba kura kwa wapiga kura wa Kata ya Ndugumbi.


**********

*YALIYOSEMWA NA MGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA KINONDONI, MAULID SAID MTULIA KWENYE MKUTANO WA KAMPENI KATA YA NDUGUMBI JUMANNE JANUARI 30, 2018*

"Kama Mtulia angekuwa amenunuliwa asingepewa tena dhamana ya kugombea Ubunge " - Mtulia

"Ningekaaje kwenye chama ambacho Mwenyekiti na Katibu hawaelewani, nimejitoa ili niwe na uhuru wa kuwatumikia wana Kinondoni." - Mtulia

"Kile chama hamkusikia kimesimamisha wabunge 8, mlitaka nami nisimamishwe?" - Mtulia



"Mtulia nimejiuzulu ili kuwaokoa Wananchi wa jimbo la Kinondoni" - Mtulia


"Kuhama chama ili kujiunga na chama chenye maendeleo, huo ni usaliti?" - Mtulia

"Mtulia huyu ndio aliotoa hela yake mfukoni kujenga visima vya maji; Mtulia aliyefungua kesi mahakamani kuzuia bomoa bomoa; ndio Mtulia yule aliyeomba maghorofa ya Magomeni Watu waliojitokeza nyumba zao wakae bure" - Mtulia

"Mtulia mimi ni yule yule mkinichagua nitahakikisha naendelea kuwaletea maendeleo nikishirikiana na viongozi wenzangu na Rais wangu mpendwa Di. Magufuli " - Mtulia

"Ninaomba tena ridhaa ili nihakikishe nawaletea maendeleo wana Kinondoni kutokana na kugombea kwenye chama chenye ilani ya uchaguzi iliyoshikan dola" - Mtulia

"Naomba dhamana ya kugombea ili nikashirikiane na wenzangu kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM 2015 - 2020" - Mtulia

"Kazi yangu mkinichagua ni kwenda kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM na si porojo wala usanii" - Mtulia

"Ukichagua Mtulia umechagua maendeleo; ukimchagua Mtulia umejenga daraja kati ya Wananchi na Serikali" - Mtulia
"Mtulia huyu ndio aliotoa hela yake mfukoni kujenga visima vya maji; Mtulia aliyefungua kesi mahakamani kuzuia bomoa bomoa; ndio Mtulia yule aliyeomba maghorofa ya Magomeni Watu waliojitokeza nyumba zao wakae bure" - Mtulia

"Mtulia mimi ni yule yule mkinichagua nitahakikisha naendelea kuwaletea maendeleo nikishirikiana na viongozi wenzangu na Rais wangu mpendwa Di. Magufuli " - Mtulia

"Ninaomba tena ridhaa ili nihakikishe nawaletea maendeleo wana Kinondoni kutokana na kugombea kwenye chama chenye ilani ya uchaguzi iliyoshikan dola" - Mtulia

"Naomba dhamana ya kugombea ili nikashirikiane na wenzangu kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM 2015 - 2020" - Mtulia

"Kazi yangu mkinichagua ni kwenda kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM na si porojo wala usanii" - Mtulia

"Ukichagua Mtulia umechagua maendeleo; ukimchagua Mtulia umejenga daraja kati ya Wananchi na Serikali" - Mtulia

MBUNGE KABATI ATOA MSAADA WA MIFUKO 25 YA SARUJI KATIKA KANISA LA FREE PENTECOST CHURCH OF TANZANIA

$
0
0
Mbunge wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akimkabidhi mchungaji wa kanisa hilo la Free Pentecost Church of Tanzania Francis Okero huku akiwa sambamba na katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa
 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa na viongozi mbalimbali  wa chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa pamoja na madiwani wa chama hicho.
Hili ndio kanisa la la Free Pentecost Church of Tanzania ambalo mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati amekabidhi mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.


Na Fredy Mgunda,Iringa.

MBUNGE wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati ametoa msaada wa mifuko ishirini na tano (25) katika kanisa la Free Pentecost Church of Tanzania lililopo kata ya Isakalilo kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa kanisa jipya ili kuendelea kutoa huduma bora ya neon la mungu.

Akizungumza wakati wa ibada iliyofanyika katika kanisani hilo Kabati alisema kuwa ni heri kujibembeleza kwa mwenye mungu kuliko kujipendekeza kwa binadamu mwenzako hivyo ni bora kuchangia shughuli za kihoro kuliko shughuli za kidunia.

“Mimi nimejitoa kuchangia shughuli zote zinazo muhusu mungu hivyo naomba mnishirikishe nami nitakuja bila kusita kwa kuwa ndio kazi yangu hata iliyonifanikisha mimi kuwa mbunge” alisema Kabati

Kabati alisema kuwa aliwaahidi kuwapa mifuko ishirini na tano ya saruji hivyo ametimiza ahadi hiyo kwa kuwapa mifuko ya saruji yote aliyoiadi hivyo amefanikiwa kutekeleza na kuwaomba wananchi wananchi wengine kuchangia maendeleo ya kanisani.

“Alikuja diwani hapa kwa niaba yangu na kuahidi mifuko hiyo ambayo ni sawa na tani moja hivyo nimeamua kutimiza kuwa lengo langu nikiahidi kitu lazima nitimize malengo yangu ya kuitoa ahadi hiyo” alisema Kabati

Aidha Kabati aliwata wananchi na viongozi mbalimbali kuendelea kuchangia shughuli za kimaendeleo kwa jamii na taasisi ambazo hazina uwezo wa kufikia mafanikio yanayotakiwa kwa ajili ya kutatua kero zinazorudisha nyuma maendeleo.

Kabati amesema kuwa wananchi na viongozi wanatakiwa kumtegemea mungu ili kuweza kufanikisha malengo wanayotarajia.

Katika hatua nyingine Kabati amewataka wazazi kuwapeleka shule watoto wao ili wakapate elimu ambayo ndiyo itakuwa dira ya maisha yao ya baadae.

Kwa uoande wake mchungaji wa kanisa hilo la Free Pentecost Church of Tanzania Francis Okero alisema kuwa walikuja viongozi wengi na kutoa ahadi nyingi lakini hakuna hata mmoja aliyetimiza ahadi yake zaidi ya mbunge Ritta Kabati.

"Nilialika wageni wengi wakala na kutoa ahadi nyingi kwa mbwembwe nyingi lakini kilichotokea hadi sana viongozi wote hakuna aliyetimiza malengo hayo hivyo nichukue furasa kushukuru" alisema Okero

Mchungaji Okero alimshukuru mbunge huyo kwa kutimiza ahadi yake ambayo itatusaidia katika ujenzi wa kanisa letu

Viewing all 12422 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>