Quantcast
Channel: g sengo
Viewing all 12428 articles
Browse latest View live

JAMBO FOOD PRODUCT CO. LTD MWEKEZAJI MKUBWA SEKTA YA VIWANDA ALIYEAMUA KUJIKITA MKOANI SHINYANGA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amejipambanua kuwa na Sera ya Serikali ya Viwanda, Jeh kwa wawekezaji wa ndani, sera hii inawashika mkono kwa kasi gani na kuwavusha? Uchumi wa Viwanda ukiimarika, Uchumi wan chi utakuwa kwa kasi na matokeo yake yataonekana hasa kwenye kuongeza wigo wa soko la ajira. Jeh kuna usawa kati ya udhibiti bidhaa za nje ili kulinda viwanda vyetu vya ndani? Kwa majibu ya maswali haya na mengineyo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products Company Limited, Bwana Salum Hamis anafunguka zaidi…… KUHUSU KIWANDA Kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited kinachojihusisha na uzalishaji wa vinywaji baridi ikiwemo soda, juisi na maji kimejichukulia umaarufu wa bidhaa zake bora ambazo zinapendwa na watu wa rika zote kutokana na uhalisia wake. Kiwanda hicho ambacho kilizinduliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, mnamo Januari 13, mwaka 2017, hadi sasa kimekuwa moja wa viwanda vya uzalishaji bidhaa bora za viwango vya kimataifa toka hapa nchini, vywenye radha murua kukufanya ujisikie fresh kabisa muda wote, kuupa mwili nguvu na mzuka zaidi, afya bora na kukuburudisha. Jambo wanazalisha na kusambaza vinywaji aina mbalimbali kwa jumla na rejareja. Vinywaji kama, Jambo Malta Lemon, Jambo Apple, Jambo Embe, Jambo Energy, Jambo Malta Pineapple, Jambo Lemon, Jambo Vito, Jambo Orange, Jambo Drinking Water na nyingine kibaooooo! Kiwanda cha Jambo kipo Shinyanga Mjini. Simu: +255622666692 au +255622666680 Email: info@jambogrouptz.net. Website: https://jambogroup.co.tz

DC MASASI ASEMA ATAKAYEPIGA KAMPENI KABLA YA WAKATI KUKIONA.

$
0
0


Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara, Selamani Mzee amepiga marufuku kwa kiongozi yeyote wa siasa wilayani humo kufanya kampeni za kisiasa kabla ya wakati kufika kwa ajili ya kuelekea katika uchaguzi mkuu wa 2020 badala yake wasubiri muda ufike ndipo wafanye hivyo.


Aidha, Mkuu huyo wa wilaya amewapa rungu viongozi wa Serikali za mitaa wilayani humo kutofumbia macho vitendo vya baadhi ya wanasiasa wilayani  ambao watajitokeza na kupinga agizo hilo na kwamba vyombo husika vya sheria vitafanya kazi yake.

Mzee alitoa agizo hilo jana wilayani Masasi  wakati alipokuwa akizungumza na wananchi pamoja na viongozi wa serikali ya mtaa wapiwapi-A mara baada ya mkuu huyo wa wilaya kujitokeza katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.

Alisema katika kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 wa raisi, wabunge na madiwani wapo baadhi ya wanasiasa wilayani Masasi wameanza kufanya kampeni kwenye maeneo yao wakati wakifahamu muda wa kufanya hivyo bado haujafika.

Alisema wenyeviti, watendaji na wajumbe wa serikali za mitaa wilayani Masasi katika kutekeleza majukumu yao wasisite kutimiza wajibu wao kwa kudhibiti vitendo vya aina hiyo kwa baadhi ya wanasiasa ambao wameanza kujitokea kwenye maeneo mitaa yao na kufanya kampen za kisiasa za uchaguzi kabla ya wakati kufika.

Mzee alisema viongozi wa serikali za mitaa kwenye maeneo yao washirikiane kwa nguvu moja kuhakikisha wanasiasa hao wanawadhibiti kisha wanawachisha tabia hiyo na badala yake wanatakiwa kusubiri muda ufike ndipo wafanye kampeni hizo kupitia taratibu husika ikiwemo za vyama vyao.

Alisema kitendo cha kufanya kampeni kabla ya muda muhafaka kufika ni kujiondolea sifa stahiki ya kugombea pindi muda wa kufanya hivyo utakapokuwa tayari umefika.

Mzee alisema kufanya hivyo ni kuvunja taratibu husika za uchaguzi na kwamba vyombo husika vitawachukulia hatua stahiki za kisheria.

Aidha, Mkuu wa wilaya huyo, ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi wa wilaya ya Masasi kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo la uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura kwa ajili ya kurekebisha taarifa zao kama zinauhitaji wa kufanya hivyo.

Kwa upande wake Msimamizi wa kituo hicho cha Mtaa wa Wapiwapi-A , Kulwa Mchelezo alisema zoezi hilo limeanza jana Januari 12 na hamasa ya watu kujitokeza kujiandikisha ni kubwa.

Alisema tangu zoezi hilo limeanza jumla ya watu 65 wamejitokeza huku zaidi ya wananchi 30 wakiwa ni wapya ambao umri wao kwa sasa unaruhusu kupiga kura.


Zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ni kwa ajili ya wale wanaotaka kurekebisha taarifa zao kwa sababu mbalimbali ikiwemo kupotelewa kadi zao, kuharibika na wale ambao kwa sasa wamefikisha umri wa kupiga kura na wanahitaji vitambulisho hivyo ili kuweza kupiga kura.

JAMBO FOOD PRODUCT CO LTD WAINGIZA BIDHAA 3 SOKONI KWA MPIGO

$
0
0

Jambo Apple Crush Soda, Jambo Ubuyu na Jambo Ukwaju ni bidhaa tatu zilizoingizwa sokoni hivi karibuni na Kiwanda cha kutengeneza vinywaji baridi cha Jambo Food Products chanya maskani yake mjini Shinyanga nchini Tanzania. Hamis Salum ni mmoja kati ya Wakurugenzi waandamizi wa kiwanda hicho akiwa ameambatana na Meneja wa Masoko wa Kampuni hiyo hapa wanakupa taarifa zaidi. KUHUSU KIWANDA Kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited kinachojihusisha na uzalishaji wa vinywaji baridi ikiwemo soda, juisi na maji kimejichukulia umaarufu wa bidhaa zake bora ambazo zinapendwa na watu wa rika zote kutokana na uhalisia wake. Kiwanda hicho ambacho kilizinduliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, mnamo Januari 13, mwaka 2017, hadi sasa kimekuwa moja wa viwanda vya uzalishaji bidhaa bora za viwango vya kimataifa toka hapa nchini, vywenye radha murua kukufanya ujisikie fresh kabisa muda wote, kuupa mwili nguvu na mzuka zaidi, afya bora na kukuburudisha. Jambo wanazalisha na kusambaza vinywaji aina mbalimbali kwa jumla na rejareja. Vinywaji kama, Jambo Malta Lemon, Jambo Apple, Jambo Embe, Jambo Energy, Jambo Malta Pineapple, Jambo Lemon, Jambo Vito, Jambo Orange, Jambo Drinking Water na nyingine kibaooooo! Kiwanda cha Jambo kipo Shinyanga Mjini. Simu: +255622666692 au +255622666680 Email: info@jambogrouptz.net. Website: https://jambogroup.co.tz

NAMBA ZA UTAMBULISHO NIDA MILIONI 6.8 HAZIJATUMIKA KUSAJILI LAINI ZA SIMU.

$
0
0

Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA inaendelea na zoezi la usajiri na utambuzi wa watu, uzalishaji wa namba za utambulisho wa Taifa na vitambulisho na ugawaji wake kwa wananchi zinazotumika kusajili laini za simu kwa alama za vidole na huduma nyingine zinazohitaji utambulisho.

NIDA imezalisha idadi kubwa ya namba za utambulisho wa Taifa kati ya hizo, namba za utambulisho wa Taifa 6,806,096 hazijatumika kusajili laini za simu kwa alama za vidole.



A

B

MONGELLA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA NIDA MWANZA AKUTANA NA OMBI KWENDA KWA MHE RAIS.

$
0
0

Wakati Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA ikiendelea na zoezi la usajiri na utambuzi wa raia, nao kupata namba zinazotumika kusajili laini zao za simu kwa alama ya vidole ili kuepuka kuzimiwa mawasiliano, nazo siku za ukomo wa zoezi hilo zikiwa zinatosha hata kuhesabika kwa vidole vya kiganja kimoja, kasi ya uzalishaji wa namba za utambulisho wa Taifa na vitambulisho sanjari na ugawaji wake kwa wananchi umeendelea kuathiri shughuli za ujasiliamali na uzalishaji kwa baadhi yao.

Alhamisi ya tarehe 16 Januari 2020 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella anafanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Mamlaka hizo mkoani hapa ambapo anakutana na misururu ya wananchi wakiwa wamesongamana kwenye mistari kulivaa lango kuu la ofisi hizo kwaajili ya kupatiwa huduma.


KABLA YA MCHEZO WA ALLIANCE NA SIMBA NABII MASHIMO AMETABIRI HAYA

$
0
0


Mchungaji maarufu mtandaoni maarufu kwa Mchungaji Mashimo asubuhi ya leo majira ya saa 3 na dakika 30 amezungumza na Jembe Fm kupitia kipindi cha kila Jumapili cha muziki wa Injili na habari zake kijulikanacho kama JEMBE GOSPEL, akizungumza juu ya tabiri zake za mara kwa mara ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikijikita katika soka la hapa nchini akitabiri michezo mbalimbali inayopigwa viwanja tofauti tofauti.

Mara baada ya mahojiano na kipindi hicho kinachoongozwa na Adolph Nzwalla feat Albert G. Sengo, hiki ndicho alichozungumza Mashimo.

CHADEMA WAVURUGANA SHINYANGA ...KATIBU MWENEZI CHADEMA ATUMBULIWA KUZUIA MKUTANO WA CHADEMA POLISI..MWENYEWE AKAZA

$
0
0
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi CHADEMA mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi akiwataarifu wanachama wa Chadema juu ya mkutano wao kuzuiwa kufanyika baada ya Katibu Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Shinyanga Mjini,Charles Shigino kuandika barua jeshi la polisi kuwa kuna taarifa za uvunjivu wa amani kwenye mkutano wa Chadema. 

CHANZO:- Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Baraza la Uongozi la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Shinyanga limemsimamisha nafasi zote za uongozi Katibu Mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga Mjini, Charles Shigino kutokana na kwenda kinyume cha Katiba ya Chama, Kanuni na Maadili ya Viongozi wa Chama kwa kuzuia mkutano mkuu wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga Mjini kwa kuandika barua Jeshi la Polisi akidai kuna dalili za uvunjifu wa amani endapo mkutano ungefanyika.

Akizungumza na Vyombo vya Habari leo Jumanne Januari 21,2020 katika ofisi za CHADEMA wilaya ya Shinyanga Mjini,Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi CHADEMA mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi amesema Baraza la Uongozi CHADEMA limechukua hatua hiyo baada ya kukutana katika kikao cha dharura cha kamati tendaji na kubaini kuwa Shigino amekiuka katiba ya chama na kanuni na taratibu za uongozi.

“Baraza limemsimamisha nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama,Ndugu Charles Shigino ambaye alikuwa Katibu Mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga na Mjumbe wa mkutano mkuu kata ya Ngokolo. Atabaki kuwa mwanachama na tunamuandikia barua ajieleze ndani ya siku 14 kwa nini asifukuzwe uongozi”,amesema Ntobi.

“Tulikuwa na mkutano mkuu wanachama wa Jimbo la Shinyanga Mjini leo katika ukumbi wa Ibanza Hoteli,tumeshangaa kupata taarifa kuwa Jeshi la polisi kupitia kwa mkuu wa polisi wilaya ya Shinyanga kuwa mkutano wetu umezuiwa kufanyika kutokana na barua iliyoandikwa na Shigino aliyeomba polisi wazuie mkutano kwamba kuna hatari na uvunjifu wa amani”,ameeleza Ntobi.

Amesema kutokana na hali hiyo viongozi wa CHADEMA walifika katika kituo cha polisi wilaya ya Shinyanga na kukutana na mkuu wa polisi wilaya (OCD) ambaye aliwaeleza kuwa wamezuia mkutano huo kutokana na barua ya mwenzao na ndipo Kamati tendaji ya Chadema ilipokaa katika kikao cha dharura na baraza la uongozi kuchukua uamuzi wa kumchukulia hatua Shigino.

“Shigino amekiuka maadili ya uongozi,amefanya utovu wa nidhamu,amekisaliti chama na kupanga njama ya kuhujumu chama na kutoheshimu ngazi za juu za uongozi katika chama. Shigino amekuwa na tabia ya kupinga maamuzi ya viongozi wenzake katika chama”,amesema Ntobi.
"
"Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA ya Mwaka 2006, Toleo la 2016. Ibara ya 7.5.4 (h) Baraza la Uongozi Mkoa, ndio Mamlaka ya nidhamu na uwajibishaji wa Viongozi wa Jimbo/Wilaya. (Ibara ya 6.3.6(iv).Kwa maana hiyo, Baraza la Uongozi limechukua hatua za kinidhamu dhidi yake, kwa kuzingatia Ibara ya 6.3.6.(d).

Hivyo, kuanzia leo, tarehe 21.01.2020, Chama kinatoa taarifa kwa umma na Wanachama kuwa Charles Shigino, amesimamishwa  ukatibu mwenezi wa Jimbo la Shinyanga Mjini mpaka hapo itavyoamuliwa vinginevyo",amefafanua.

Ntobi amebainisha kuwa mkutano huo mkuu wa wanachama ulilenga kujadili masuala mbalimbali ya kujenga CHADEMA ikiwemo kuwapa wanachama muhtasari wa mambo yaliyojiri katika Mkutano mkuu wa CHADEMA taifa uliofanyika hivi karibuni na kujadili waraka wa Katibu mkuu wa CHADEMA.

Naye Katibu wa Baraza la Uongozi CHADEMA mkoa wa Shinyanga, Zacharia Obad amesema Shigino anayo nafasi ya kujitetea ndani ya siku 14 na kukata rufaa baada ya siku 30 kuhusu maamuzi yaliyochukuliwa na Baraza la Uongozi CHADEMA mkoa.

Aidha amesema CHADEMA haitasita kuwachukulia hatua wale wote wanaokwenda kinyume na maadili na katiba ya CHADEMA.

Hata hivyo Shigino akizungumza na Malunde 1 blog amesema kitendo cha kuweka zuio la mkutano wa wilaya ya Shinyanga Mjini kutokana na kwamba viongozi wa Baraza la Uongozi CHADEMA mkoa wa Shinyanga wamekiuka katiba ya Chadema kwa kuitisha mkutano mkuu wa wilaya ambao hawastahili kuuitisha na kuhudhuria labda kama watakuwa wamepewa mualiko wa wageni waalikwa tu.

Shigino amesema kutokana kutoelewana kwake na viongozi wa baraza la uongozi Chadema mkoa wa Shinyanga kuhusu mkutano huo ndiyo kumemfanya aweke zuio kwa kutumia jeshi la polisi kwani hali isingekuwa shwari ndani ya mkutano huo.

“Ni kweli nimeweka zuio la mkutano wa Chadema kuzuia viongozi hawa waliokanyaga katiba ya CHADEMA. Mkutano wao ulikuwa Batili,Wametumia katiba gani hawa viongozi wa mkoa ambao ni viongozi wa baraza la uongozi wa mkoa na vikao vya mashauriano tu kuitisha mkutano wa wilaya halafu wao ndiyo wakawe wageni rasmi na wasemaji kwenye Mkutano mkuu wa wilaya. Kwenye mkutano huo pia waliita waliokuwa wagombea uenyekiti serikali za mitaa kuhudhuria mkutano..Sasa hapa wametumia katiba gani?,amehoji Shigino.

“Bado sijapata barua ya kusimamishwa uongozi. Lakini hawa Viongozi wa baraza la uongozi Chadema mkoa siyo wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya, Wamepata wapi haya mamlaka ?.Nitaripoti kwa viongozi wa Kanda ya Serengeti kilichotokea. Nataka nijue nani anatakiwa kutumbuliwa kati yangu na wao ambao wamekanyaga katiba?”,amesema.

Hata hivyo Shigino amesema yeye bado ni mwanachama wa CHADEMA na atabaki kuwa CHADEMA na ataendelea kuwa katibu Mwenezi Wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga Mjini na hapendi kuona Chama kinaharibiwa na watu wachache vimelea wanaotengeneza fitna ambao wanashiriki kuleta vurugu ndani ya chama.

Shigino alihamia CHADEMA mwaka 2015 akitokea CCM akiwa Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini na Januari 15,2019 alichaguliwa kuwa Katibu Mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga Mjini.
PICHA ZAIDI.
Hapa ni nje ya ofisi za Chadema wilaya ya Shinyanga Mjini,Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi CHADEMA mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi akiwataarifu wanachama wa Chadema juu ya mkutano wao kuzuiwa kufanyika baada ya Katibu Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Shinyanga Mjini,Charles Shigino kuandika barua jeshi la polisi kuwa kuna taarifa za uvunjivu wa amani kwenye mkutano wa Chadema uliotakiwa kufanyika leo Januari 21,2020 katika ukumbi wa Ibanza Hoteli Mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi CHADEMA mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi akitoa taarifa kwa wanachama wa Chadema kuhusu hatua iliyochukuliwa na Baraza la Uongozi Chadema mkoa kumsimamisha nafasi zote za uongozi Charles Shigino.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi CHADEMA mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi akitoa taarifa kwa wanachama wa Chadema kuhusu hatua iliyochukuliwa na Baraza la Uongozi Chadema mkoa kumsimamisha nafasi zote za uongozi Charles Shigino.
Wanachama wa Chadema wakimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi CHADEMA mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi CHADEMA mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi akisoma katiba ya Chadema na vifungu alivyokiuka Shigino.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi CHADEMA mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi akizungumza na waandishi wa habari ndani ya Ofisi ya CHADEMA Shinyanga Mjini leo Januari 21,2020 na kuwapa taarifa ya kumsimamisha nafasi zote za uongozi Katibu Mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga Mjini, Charles Shigino.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi CHADEMA mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi akizungumza na waandishi wa habari ndani ya Ofisi ya CHADEMA Shinyanga Mjini leo Januari 21,2020 na kuwapa taarifa ya kumsimamisha nafasi zote za uongozi Katibu Mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga Mjini, Charles Shigino.Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema mkoa wa Shinyanga Winfrida Mwenula. Wa kwanza kulia ni  Mwenyekiti wa  Madiwani wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga ,William Shayo akifuatiwa na Katibu wa Baraza la Uongozi CHADEMA mkoa wa Shinyanga,Zacharia Obad.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi CHADEMA mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi akionesha barua ya Charles Shigino kuzuia mkutano wa wanachama wa CHADEMA.
Katibu wa Baraza la Uongozi CHADEMA mkoa wa Shinyanga,Zacharia Obad akielezea zaidi kuhusu maamuzi waliyochukua dhidi ya Charles Shigino.
Katibu wa Baraza la Uongozi CHADEMA mkoa wa Shinyanga,Zacharia Obad akielezea zaidi kuhusu maamuzi waliyochukua dhidi ya Charles Shigino.
Katibu Mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga Mjini, Charles Shigino naye akizungumza na waandishi wa habari dhidi ya maamuzi ya Baraza la Uongozi la CHADEMA mkoa wa Shinyanga kumsimamisha nafasi ya Katibu Mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga Mjini ambapo amesema maamuzi hayo ni batili na ataendelea na nafasi hiyo na kubaki kuwa mwanachama mwadilifu wa Chadema. 
Katibu Mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga Mjini, Charles Shigino naye akizungumza na waandishi wa habari dhidi ya maamuzi ya Baraza la Uongozi la CHADEMA mkoa wa Shinyanga kumsimamisha nafasi ya Katibu Mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga Mjini ambapo amesema maamuzi hayo ni batili na ataendelea na nafasi hiyo na kubaki kuwa mwanachama mwadilifu wa Chadema.

LIVE:- SHEREHE ZA MWAKA MPYA 2020 KWA MABALOZI ( DIPLOMATIC SHERRY PATY ) . IKULU DSM

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ashiriki Sherehe za Mwaka Mpya 2020 na chakula cha jioni kwa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini (Diplomatic Sherry Party ) Katika ukumbi wa kikwete Ikulu Jijini Dar es salaam.

#LIVE: HAFLA YA KUKABIDHI NYUMBA ZA MAAFISA NA ASKARI WA MAGEREZA . UKONGA DSM

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ashiriki hafla ya Kukabidhi nyumba za Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza Ukonga Jijini Dar es salaam.

Breaking News: WAZIRI WA MAMBO YA NDANI KANGI LUGOLA AJIUZURU.

$
0
0


Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekubali ombi la kujiuzulu kwenye nafasi yake ya Uwaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola kutokana na sababu mbalimbali.

Rais Magufuli amesema hayo wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa nyumba 12 za Askari Magereza kwenye Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam, ambapo ameeleza kulikuwa na mkataba ambao ni wa ajabu.


''Mhe. Kangi Lugola nilitegemea barua yake ya kujiuzulu leo angetakiwa asiwepo hapa, Watu wamesaini mradi wa hovyo ambao hata Bunge haujui ni mambo ya hovyo watu walikuwa wanalipwa sitting allowance ya dola mia 800, Kangi Lugola pamoja na mwili wake ni Mwanafunzi wangu nimemfundisha Sengerema Secondary lakini kwa hili hapana, Commissioner Thobias Andengenye kwa hili pia Hapana''.

ATC KUWAPELEKA CHINA WACHIMBAJI WADOGO

$
0
0

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo Nchini, John Bina amewasilisha ombi kwa Balozi wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki, akimwomba balozi kuzungumza na wawekezaji toka taifa hilo kuona jinsi gani wanaweza kusaidia wachimbaji nchini katika uwezeshaji wa vifaa na vitendea kazi vya uchimbaji wa madini, teknolojia na suala la mitaji.

Akizungumza katika MKUTANO WA FURSA ZA UWEKEZAJI WA TEKNOLOJIA MITAJI NA MASOKO YA MADINI NCHINI UNAOFANYIKA ROCK CITY MWANZA na kuhudhuriwa na wachimbaji wadogo na viongozi wa sekta hiyo toka mikoa yote nchini, Bina amesema kutokana na shirikisho lake kuwa na rasilimali watu ya kutosha anaimani ushirikiano ukijengwa kati yao na Ubalozi wanauwezo wa kukopesheka kwa kupatiwa mkopo wa vifaa na nyenzo za kisasa za uchimbaji ili wanachama wake waweze kukodisha na kupitia kipato kitakachopatikana kulipa deni la mkopo.

Aidha Rais huyo amewasihi wachimbaji hao kutojihusisha na suala la utoroshaji madini, akisema serikali tayari imekwisha weka mfumo rafiki kwao kufanya biashara bila hofu ya kukimbilia njia za panya kuhofia tozo zisizoeleweka.

Pia Rais huyo wa Shirikisho ameiomba Serikali kutoa ufafanuzi juu ya taratibu za kuuza bidhaa nje ya nchi na zuio lake kwa kufafanua ni madini gani yanaruhusiwa kusafirishwa na madini gani hasiyoruhusiwa.


Bunge lanusa ufisadi wa bilioni 15 Machinjio ya Dodoma, laagiza vigogo NARCO, NICOL wakamatwe

$
0
0

Na Mwandishi Wetu,Dodoma 

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji imeagiza kukamatwa na kushtakiwa  Watendaji wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), Watendaji Wakuu wa Wizara ya Mifugo pamoja na Viongozi wa Kampuni ya Taifa ya uwekezaji (NICOL) kufuatia kashfa ya uchotwaji wa Shilingi bilioni 15 kwenye Biashara ya Uendeshaji wa Machinjio ya Dodoma katika kipindi cha miaka 11 iliyopita.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mahmoud Mgimwa alisema watendaji wa Kampuni ya Ranchi ya Taifa (NARCO) na Watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi waliohudumu katika  kipindi cha kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2015 ambapo walishirikiana kwa pamoja na Kampuni ya NICOL kuwaibia watanzania fedha hizo jambo ambalo Bunge 11 kamwe haliwezi kubariki wizi huo mkubwa wa fedha za watanzania.

Akizungumza kwenye ziara ya kamati hiyo kutembelea machinjio ya Dodoma ambayo kwa sasa inaendeshwa Serikali baada ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina kuvunja mkataba huo mbovu baina ya NARCO na NICOL  uliooingiizia hasara Serikali kwa kipindi cha miaka 11 huku wahusika waliohusika na kashfa hiyo wakiwa bado hawajachukuliwa hatua yoyote.

Mgimwa alielezwa kushangazwa na usimamizi mbovu, ubadhirifu na ukiukwaji mkubwa wa mkataba uendeshaji wa machinjio hiyo na kuelezea kusikitishwa kwake na watendaji  waliopewa dhamana kusimamia mali hiyo kwa niaba ya watanzania kushirikiana kufanya hujuma hiyo.

Mgimwa alihoji iweje tangu mwaka 2008 ufisadi huo umefanyika bila wahusika kuchukulia hatua wakiwemo waliokuwa watendaji wa NARCO, NICOL na Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kuagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwatafuta na kuwafikisha kwenye vyombo vya Sheria.

Pia Kamati hiyo imepongeza uamuzi wa Serikali ya kuvunja mkataba wa mauzo ya mali za machinjio ya Dodoma baina ya Serikali na Kampuni ya NICOL na kuirejesha machinjio hiyo chini ya umiliki wa Serikali na kuitaka kufanya haraka kurejesha masoko ya nyama katika nchi za Falme za Kiarabu yaliyopotea kutokana na usimamizi mbovu wa waendeshaji hao wa zamani.

Pia Kamati imeitaka Serikali kuhakikisha fedha zote kiasi cha jumla ya shilingi 9,712,127,660 ambazo Serikali ilimeibiwa katika biashara ya machinjio zinalipwa haraka pamoja mbia NICOL kulipa madeni yote inayodaiwa Kampuni ya Ubia TMCL kiasi cha shilingi 5,248,084,000.

Mbali na Kamati hiyo kupongeza uamuzi wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) ambaye ni mbia katika Kampuni ya Ubia TMCL kujiondoa kwenye ubia wa Kampuni ya TMCL bado viongozi waliohusika na ufisadi huo waweze kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria.

Mbunge wa Moshi Vijijini, Antony Komu alisema uamuzi uliofanywa na Waziri Mpina katika kubaini kasoro hizo na kuchukua hatua unapaswa kuendelezwa kwa Serikali kutengeneza mfumo endelevu wa kubaini udhaifu na kuchukua hatua kwani ni jambo la kusikitisha kuona  ufisadi mkubwa kiasi hicho umefanyika bila ya wahusika kuchukuliwa hatua.

Komu alitaka hatua kama hizo ziwe endelevu ili kunusuru mali za nchi badala ya kumuachia kiongozi  mmoja tu ambaye ni Waziri Mpina kusimamia mambo kama hayo.

Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina aliihakikishia Kamati hiyo kuwa Serikali iko kwenye hatua ya mwisho ya kuifanyia ukarabati mkubwa machinjio hiyo na kurejesha upya masoko ya nyama nje ya nchi ikiwemo nchi za Famle ya Kiarabu na Comoro.

Pia ameihakikishia kamati hiyo kuwa wote waliohusika na wizi na ubadhirifu hawatapona kwani Serikali inajua kuwa mbali na fedha hizo zilizoibwa za watanzania bado hata mishahara ya wafanyakazi wa kampuni hiyo nayo ilifanyiwa ufisadi na kuleta usumbufu mkubwa watumishi.

Waziri Mpina alisema kwa muda mrefu Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekuwa ikichukua hatua mbalimbali katika kurekebisha kasoro za uendeshaji wa Machinjio ya Dodoma kama sharti muhimu katika Mkataba wa Mauzo ya Mali kwenye Ibara ya 4.1.3.1 na kwa kuwa jitihada za kuinusuru Machinjio hiyo zimefanyika kwa muda mrefu bila ya mafanikio yoyote.

Hivyo Serikali ilijiridhisha kwamba Mbia (NICOL) amekiuka vipengele muhimu vya Mkataba katika Ibara ya 7, 13, 6, 9 na 102; Pia NICOL imekuwa ikifanya biashara na mali za Kampuni bila ya kuwekeza na bila ya kutoa gawio kwa Serikali kwa kipindi chote cha miaka 11 alichokabidhiwa Kiwanda hicho;

Waziri Mpina amesema tangu machinjio hiyo ibinafsishwe Serikali imeendelea kupata hasara na mali nyingi za Kampuni kama mitambo, majengo, magari na rasilimali nyingine zimechakaa na hakuna ukarabati wowote uliofanyika;

Pia nchi yetu imepoteza ajira, fedha za kigeni, biashara na masoko ya mazao ya mifugo baada ya Kiwanda kufungiwa kuuza mazao ya mifugo katika nchi za Jumuiya ya Kiarabu (UAE).

Aidha, Kampuni 10 zilisimama kusafirisha na kufanya biashara ya nyama baada ya Kiwanda kufungiwa ambapo kwa mwezi mauzo ya nyama nje ya nchi katika Machinjio yalikuwa yamefikia tani 192 sawa na mbuzi 24,000 kwa mwezi. Pia, kiwango cha uchinjaji wa ng’ombe kushuka kutoka wastani wa ng’ombe 120 hadi 50 kwa siku;

Hata hivyo hasara na madeni ya Kiwanda cha TMCL yanaendelea kukua kila uchao huku Mbia (NICOL) akishindwa kurekebisha kasoro zilizobainika katika vipindi tofauti hata baada ya kupewa notisi ya muda wa siku 30 na hata Mbia mwenzake (NARCO) kumpa notisi ya siku 180, pia, ziara za Viongozi katika Machinjio akiwemo Waziri wa Mifugo na Uvuvi.

MAREKANI YAMUOMBOLEZA BINGWA WA MPIRA WA KIKAPU KOBE BRYANT.

$
0
0

Nyota wa mpira wa kikapu nchini Marekani Kobe Bryant na binti yake Gianna ni miongoni mwa watu tisa waliofariki katika ajali ya helikopta iliyotokea mji wa Calabasas, California.
Bryant amefariki akiwa na miaka 41, alikuwa anasafiri na ndege binafsi aina ya helikopta ambayo ilianguka na kuwaka moto.
Mkuu wa polisi wa Los Angeles anasema kuwa hakuna yeyote aliyenusurika katika ajali hiyo.
Ripoti za awali zilisema kuwa kulikuwa na watu watano ndani ya ndege.
Bryant, ambaye ni bingwa wa Ligi ya Kikapu NBA mara tano alikuwa anatambuliwa duniani katika historia ya kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi wa kikapu.

Mashabiki wamekusanyika katika eneo lililotokea ajali
Salamu za rambirambi kutoka kwa watu maarufu na wachezaji wenzake nyota huyo zimekuwa zikimiminika kuonyesha mshtuko wa kifo cha nyota huyo wa mpira wa vikapu.
Viwanja vyote vya mpira wa vikapu nchini Marekani vilitenga muda wa kuwa kimya kwa heshima ya mchezaji huyo.
Bryant atakumbukwa katika tuzo za Grammy ambazo zilikuwa zikitolewa katika uwanja wa LA Lakers, eneo ambalo alikuwa akichezea kipindi chote.
"Tumechanganyikiwa na tuna uzuni sana kwa sasa," alisema mtangazaji wa Grammys Alicia Keys.
"Kwa sababu mapema leo katika mji wa Los Angeles, Marekani na duniani kwa ujumla tumepoteza shujaa.

Kobe Bryant alikuwa bingwa wa NBA mara tano na mshindi wa Oscar
Tumesikitishwa sana kwa kumpoteza Kobe Bryant, ndio maana leo tumesimama katika nyumba aliyoijenga."
NBA ilitoa tamko linalosema kuwa ,imesikitishwa sana na ajali iliyosababisha kifo cha Kobe Bryant na binti yake, Gianna" mwenye umri wa miaka 13.
"Kwa misimu 20 , Kobe alituonyesha kile ambacho kinawezekana kwa mtu ambaye ana kipaji na nia ya ushindi," alisema.

Ajali ilitokeaje?

Afisa wa polisi Alex Villanueva alisema kuwa helkopta inaonyesha uwa na watu tisa wakati inaanguka, na kuondoa idadi ya watu watano ambao walitajwa hapo awali na maofisa.
Katika taarifa iliyotolewa na mji wa Calabasas zilisema kuwa wamepokea taarifa hiyo kwa maskitiko makubwa sana.
"Ndege hiyo ilianguka nje kidogo ya mji wa Las Virgenes majira ya asubuhi wa saa za Marekani . Hakuna aliyenusurika, aliongeza.
Gavin Masak, alikuwa anaishi karibu na eneo tukio hilo lilipotokea, alikiambia kituo cha CBS News kuwa helkopta ilianguka.
"Haukuwa kama mlipuko lakini tulisikia kama bomu limelipuka kwa sauti kubwa. Lakini ilisikika kama sauti ya ndege au helkopta, ilisikika sauti kubwa sana, niliingaia ndani na kwenda kumtaarifu baba yangu na kumwambia kilichotokea. Hivyo nilivyotoka nikaona moshi mweusi ukitokea mlimani, ulikuwa mweusi au kama kijivu", alisema.

Shahidi mwingine alisema kuwa alisikia injini ikiwa inashida hata kabla ndege haijafika chini.
Polisi wa LA wameonyesha picha za tukio la ajali hiyo zikionyesha gari la zima moto na moshi ukivuka kutoka milimani.

Presentational white space

Bodi ya taifa ya usafiri imeitambua ndege iliyoanguka kuwa ni Sikorsky S-76B na imesema kuwa itatuma kikosi chake kuchunguza chanzo cha ajali hiyo.

Bryant alikuwa nani?

Bryant alicheza mpira wa kikapu kwa 20-katika viwanja vya Los Angeles Lakers. Aliacha kucheza mpira huo Aprili 2016.
Mafanikio yake ni pamoja na kuwa mchezaji bingwa wa NBA kwa mwaka 2008, mara mbili aliibuka kuwa bora zaidi ya wengine.
Vilevile alikuwa mfungaji bora wa NBA pamoja na bingwa mara mbili wa mashindano ya Olympiki.
Aliwahi kupata pointi 81 dhidi ya wachezaji wa Toronto Raptors mwaka 2006, katika historia ya michezo ya NBA.
Bryant alishinda tuzo za Oscar kama mchezaji wa filamu fupi mwaka 2018 filamu hilo ilikuwa 'Dear Basketball', filamu ya dakika tano iliyoangazia barua moja ya
Aliwahi kupata pointi 81 dhidi ya wachezaji wa Toronto Raptors mwaka 2006, katika historia ya michezo ya NBA.
Bryant alishinda tuzo za Oscar kama mchezaji wa filamu fupi mwaka 2018 filamu hilo ilikuwa 'Dear Basketball', filamu ya dakika tano iliyoangazia barua moja ya michezo aliyoandika mwaka 2015.
Bryant na mke wake, Vanessa, walikuwa na watoto wengine wakike watatu ambao ni Natalia, Bianca na Capri.

Presentational white space

Bryant alishutumiwa kwa kesi ya unyanyasaji wa kingono mwaka 2003, na binti mwenye umri wa miaka 19-aliyekuwa akifanya kazi katika mgahawa wa Coloradot. Alikanusha madai hayo, na kusema kuwa walikuwa na mahusiano ya kimapenzi ya kukubaliana.
Kesi hiyo ilifutwa baada ya mtu aliyemshtaki kukataa kutoa ushahidi mahakamani.
Ingawa baadae aliomba radhi kwa kitendo kile na kusema sababu ilikuwa msichana aliyekuwa naye hakuwa na mtazamo sawa na wake wakati walipokuwa kwenye mahusiano yao.

Watu wanasemaje kuhusu kifo cha nyota huyo?

Salamu nyingi za rambirambi zimemiminika katika mitandao ya kijamii kufatiwa taarifa ya ajali hiyo.
Shaquille O'Neal,ambaye alicheza na Bryant huko Lakers kati ya mwaka 1996 na 2004,alisema kuwa hana neno la kusema kwa sababu ya maumivu ambayo anayo.
"Ninakupenda na utakumbukwa," aliandika katika mtandao wa Instagram wakiwa katika picha ya pamoja na jezi zao za Lakers.
Deron Williams, alikuwa mshindi wa medali ya dhahabu ya Olympiki akiwa na Bryant, aliishiwa maneno. alimuelezeaBryant kuwa mchezaji bingwa aliyewahi kucheza naye.
Mchezaji wa mpira wa vikapu wa zamani Tony Parker alisema kusikitishwa kwa kifo hicho.
"Hii ni habari ya kuhuzunisha sana", alisema rais wa Marekani Donald Trump.
Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama alimuelezea Bryant kuwa bingwa na aliyeonesha umahiri katika kipaji chake.
Usain Bolt ambaye ana medali nane za dhahabu za olimpiki alisema kuwa haamini taarifa hizi.
Mwanamuziki Kanye West aliandika katika mtandao wa twitter kuwa Bryant aliishi maisha ambayo yaliwavutia wengi.
Mariah Carey naye alisema alivyoshtushwa na taarifa hizi.


AJABU:- NDEGE YA IRAN YAANGUKA BARABARANI BAADA YA RUBANI KUKOSA MWELEKEO .

$
0
0

Ndege ya abiria ya Iran ilijipata katika barabara ya umma baada ya kuteleza katika barabara ya uwanja wa ndege ilipokuwa ikitua.
Abiria wawili kati ya 136 waliokuwa wakiabiri ndege hiyo walipata majeraha ya miguu kufuatia kisa hicho katika mji wa Mahshahr, kulingana na maafisa wa afya.
Ndege hiyo ya kampuni ya Caspian iliondoka mjini Tehran . Matairi yake hayakujitokeza kabisa wakati ilipotarajiwa kutua.
Picha za abiria waliokuwa wakitoka katika ndege hiyo zilichapishwa katika mitandao ya kijamii.
Runinga ya serikali ilinukuu maafisa wa usafiri wa angani wakisema kwamba rubani aliishusha ndege hiyo kuchelewa hivyobasi akakosa barabara ya ndege.
Ripota mmoja ambaye alikuwa ndani ya ndege hiyo alisema kwamba matairi ya nyuma ya ndege hiyo yaliharibika na kwamba ndege hiyo iliteleza bila matairi yake.

Presentational white space

Msemaji wa shirika la udhibiti wa safari za angani Reza Jafarzadeh aliambia chombo cha habari cha Isna news kwamba ndege hiyo iliteleza kutoka katika barabara yake siku ya Jumatatu alfajiri .
Aliongezea kwamba uchunguzi unaendelea.

HIVI NDIVYO WADAU WA MADINI NCHINI TANZANIA WANAVYOPAMBANA KUIKUZA SEKTA HIYO.

$
0
0


Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki ametanabaisha fursa za kibiashara zilizopo ndani ya sekta ya madini katika soko la nchini China, na kuwahimiza watanzania kuzichangamkia kwani uwakilishi wake upo tayari kuwahuwisha wafanyabiashara hao kwa kila hatua.


Balozi Kairuki amezibainisha fursa hizo mwishoni mwa wiki (Januari 24, 2020) jijini Mwanza wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa madini Tanzania uliolenga kujadili fursa za uwekezaji, teknolojia, mitaji na masoko ya madini huku akiwasihi wafanyabiashara wa madini Tanzania kujiandaa na safari ya kutembelea China mwezi ujao ili kusaka fursa mbalimbali katika sekta ya madini.

KATIKA PICHA:-

HAYA ndiyo yaliyojiri katika kikao cha wadau wa madini kilichofanyika jijini Mwanza Januari 24, 2020.











KITUO CHA KUKUZA BIASHARA ZA WAJASILIAMALI CHAZINDULIWA JIJINI MWANZA.

$
0
0

Tanzania kuelekea nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025 ni suala ambalo mgombea urais kupitia tiketi ya CCM katika uchaguzi mkuu uliofanyika 2015, Dk John Magufuli alikuwa akilihubiri kila alipokuwa akisimama katika mikutano ya hadhara.

Alieleza kwamba serikali atakayoiunda akipewa ridhaa hiyo amekusudia iwe ambayo itabadili maisha ya watanzania hususani wale wenye kipato cha chini, katika mwendelezo wa juhudi za kufanikisha adhma hiyo Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amezindua kituo cha kuendeleza ukuaji wa biashara za wajasiriamali kupitia shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) chini ya mradi wa SIDO TLED HUB, 

Mongella amefanya uzinduzi huo Januari 24, 2020 katika viunga vya ofisi za SIDO Nyakato jijini Mwanza na kubainisha kwamba serikali mkoani Mwanza iko tayari kutoa ardhi kwa ajili ya shughuli za viwanda vidogo.


 Mkurugenzi Mkuu SIDO, alisema Profesa Sylvester Mpanduji akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Meneja SIDO Mkoa Mwanza, Bakari Songwe akitoa salamu zake kwenye uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), Mariam Munanka akitoa salamu zake kwenye uzinduzi huo.
 Rais wa chama cha wafanyabiashara, viwanda na kilimo TCCIA, Paul Koyi akizungumza kwenye ufunguzi huo.
Mkurugenzi Mkazi Shirika la VSO, Dawn Hoyle akitoa salamu zake kwenye mkutano huo.
Mwakilishi Ubalozi wa Canada nchini Tanzania, Christopher Duguid akitoa salamu zake kwenye uzinduzi huo.
Mwakilishi shirika la Africa CUSO International, David Forest akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mwakilishi Mkazi Shirika la Africa CUSO International, Romanus Mtunge akitoa salamu zake kwenye uzinduzi huo.
 Wadau mbalimbali wakifuatilia uzinduzi huo.
 Wadau mbalimbali wakiwemo kutoka Kituo cha Biashara, Viwanda na Kilimo nchini (TCCIA) walikuwa sehemu ya waliojumuika kwenye hafla hiyo.
 Wadau kwa umakini na tafakari wakifuatilia hafla hiyo.

 Wadau kwa umakini na tafakari wakifuatilia hafla hiyo.
 Mkurugenzi wa kampuni ya Mwanza Quality Wines inayotengeneza mvinyo wa matunda (Power Banana), Leopord Lema (kulia) akitoa ufafanuzi kuhusiana na bidhaa hiyo baada ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto) kutembelea mabanda ya wajasiriamali mbalimbali waliohudhuria halfa hiyo.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto) akifurahia jambo baada ya kutembelea banda la kampuni inayotengeneza mvinyo kwa kutumia ndizi jijini hapa ijulikanayo kama  Mwanza Quality Wines.

Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto) akiwa banda la wajasiliamali akinamama.

"Wote ni mashahidi kwamba kuna baadhi ya wajasiliamali kupitia mikopo wameuziwa nyumba zao, viwanja vyao hata mali zao walizokuwa nazo, wamesaidiwa kuanzisha mpango wa biashara unaouzika benki na kukopesheka lakini hawakusaidiwa mpango unaolingana na wazo la mwenye biahsra na muelekeo wa mfanyabiashara. Kituo hiki kitahakikisha wajasiliamali wanapata mikopo inayofanana na wao, kuwaelekeza maeneo yanayotakiwa sanjari na masoko yanavyohitaji"  alisema Mwakilishi Mkazi Shirika la Africa CUSO International, Romanus Mtunge akitoa salamu zake kwenye uzinduzi huo.

SERA YA USHIRIKA MSINGI WA MABADILIKO CHANYA YA SEKTA YA USHIRIKA

$
0
0


 Mkurugenzi mstaafu wa Rabo Foundation Netherlands Bw. Pierre Van Hedel akielezea namna Vyama vya Ushirika vinavyofanya kazi katika nchi ya Netherlands kwa lengo la kujifunza na kuongeza ujuzi katika maboresho ya Sera ya Ushirika ya Tanzania


 Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika wa Kifedha Bw. Josephat Kisamalala akieleza jambo wakati wa Warsha ya maboresho ya Sera ya Maendeleo ya Ushirika

 Mkurugenzi wa Mipango Ufuatiliaji na Tathmini wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Bw. Buji Bampebuye akifafanua jambo katika kikao cha Warsha ya kujadili maboresho ya Sera ya Ushirika (2002) kilichokuwa kikifanyika Mkoani Morogoro hivi karibuni
Mjumbe wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania (SCCULT) Bi. Anna Lupiano akieleza matarajio ya Vyama katika maboresho ya Sera ya Maendeleo ya Ushirika
 Mshauri wa Kibiashara wa Shirika la Kimataifa lisilo la Kiserikali AGRITERRA Bw. Raymond Lyimo akitoa mada kwa wajumbe wa Warsha ya maboresho ya Sera ya Maendeleo ya Ushirika
 Mshauri wa Kibiashara wa Shirika la Kimataifa lisilo la Kiserikali AGRITERRA Bw. Mikidadi Waziri akitoa mada wakati wa Warsha ya maboresho ya Sera ya Ushirika



Mkurugenzi wa Mipango Ufuatiliaji na Tathmini wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) Bw. Buji Bampembuye amesema wadau wote wa Ushirika wakitekeleza majukumu yao ya Kiushirika kupitia dira na mwelekeo wa Sera ya Ushirika, ni dhahiri kwamba Sekta ya Ushirika itakuwa na mabadiliko chanya na yenye tija kwa wananchi. 

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Warsha ya kujadili maboresho ya Sera ya Ushirika (2002) iliyoanza Jumanne 28 Januari, 2020 hadi 29 Januari 2020, Mkoani Morogoro. 

“Ushirika ni moja ya nyenzo muhimu inayoweza kutumika nchini katika kuondoa umaskini na kuondokana na uchumi tegemezi. Hivyo, kwa kuimarisha Sera ya Ushirika tunajiwekea misingi imara ya kuendeleza Ushirika nchini,” alisema Bw. Bampebuye 

Bw. Bambebuye amesema Tanzania tunaweza kujifunza mambo mengi mazuri kutoka kwenye nchi zilizofanikiwa katika Sekta ya Ushirika pia tunaweza kutumia tafiti zetu zilizowahi kufanyika na kuingiza yatakayoongeza chachu ya ukuaji wa Sekta ya Ushirika na kupata Sera itakayokuwa ikijibu Changamoto za wakulima na Wanaushirika kwa ujumla. 

Mshauri wa Kibiashara wa Shirika la Kimataifa lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Ushirika nchini liitwalo AGRITERRA Bw. Mikidadi Waziri akitoa mada katika Warsha hiyo ameeleza kuwa Shirika hilo kama mdau wa Ushirika limekuwa likifanya kazi katika kuongeza msukumo wa Maendeleo katika Sekta ya Ushirika kupitia mafunzo kwa Vyama vya Ushirika ya Utawala Bora, Usimamizi wa Fedha na uhamasishaji. 

Bw. Mikidadi alisema kuwa baadhi ya Changamoto zilizopo katika Sekta ya Ushirika ni pamoja na ushiriki mdogo wa vijana na wanawake hususan katika ngazi za uongozi za Vyama vya Ushirika. Hivyo, akashauri haya ni mambo ya msingi ya kuzingatiwa katika maboresho ya Sera ili kuhakikisha kuwa Sekta inakuwa endelevu na inatoa fursa za kiuchumi kwa makundi yote ya jamii zetu. 

Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania (SCCULT) Bi. Anna Lupiano amesema uboreshaji wa Sera ya Ushirika unatoa matazamio ya kupata utendaji na utekelezaji wa majukumu utakaoenda kujibu changamoto mbalimbali za Sekta ya Ushirika. 

Bi. Lupiano ametoa wito kwa Viongozi na Watendaji wa Vyama vya Ushirika kufuata na kutekeleza matakwa ya Sera mpya itakapokuwa tayari katika hatua za utekelezaji ili kuboresha na kuhakikisha uendelevu wa Vyama vya Ushirika. 

UJIO WA MV ILEMELA SASA WAMPA USINGIZI MBUNGE ANGELINA MABULA.

$
0
0

Ni dhahiri kuwa changamoto ya usafiri kwa wananchi wa eneo kati ya Kayenze na kisiwa cha Bezi wilayani Ilemela mkoani Mwanza sasa inakwenda kuwa historia mara baada ya kuanza majaribio ya usafiri na usafirishaji jumanne ya tarehe 28 Januari 2020.

Akizungumza mbele ya mamia ya wananchi Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt. Angeline Mabula amekiri kuwa "Kweli ukitaka maendeleo wahitaji kuwa na ndoto kubwa" kwani wakati wa ahadi za uchaguzi 2015 moyo ulimsukuma kutamka ndoto yake hiyo kwa wakazi jimboni mwake lakini ilimnyima usingizi akiwaza na kuwazua nini kitatokea iwapo ahadi hiyo isinge kamilika.

Mabula amemwaga sifa nyingi kwa Rais wa Serikali ya awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akidai kuwa ndiye aliyempa kiburi na kujiamini kupitia historia ya utendaji wake.
Viewing all 12428 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>