Mwanalyaku mabingwa wa Balimi Ngoma Mwanza.
Fainali za Mkoa wa Mwanza zilifanyika katika Uwanja wa Polisi Mabatini na fainali za Kanda za mashindano ya Balimi Ngoma zinatarajiwa kufanyika August 16,2014 jijini Mwanza kwa kushilikisha vikundi viwili viwili kutoka Tabora, Shinyanga, Bukoba, Musoma na Wenyeji wa mashindano Mwanza.
Na Mwandishi Wetu.
FAINALI za mashindano ya Ngoma za Asili ngazi ya mikoa zijulikanazo kama “Balimi Ngoma Festival 2014” Mkoani Mwanza kikundi cha Mwanalyaku cha chenye makazi Magu kimefanikiwa kuwa mabingwa wa Mkoa wa Mwanza na kuzawadiwa fedha taslimu Shingi 600,00/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa Kagera katika fainali za Kanda zinazotarajiwa kufanyika Augusti 16,2014 Mkoani Mwanza.
Nafasi ya pili ya mashindano hayo ilichukuliwa na Kikundi cha Bujora cha Magu pia ambacho kilizawadiwa fedha taslimu Shilingi 500,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa katika fainali za Kanda.
Nafasi ya tatu ilichukuliwa na kikundi cha Utandawazi cha Ukerewe ambacho kilizawadiwa fedha taslimu Shilingi 400,000/= na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha Wadonho cha Sengerema ambacho kilizawadiwa fedha taslimu shilingi 300,000/=.
Nafasi ya tano ilichukuliwa na kikundi cha Mwanza Sanaa na nafasi ya sita ilikwenda kwa kikundi cha Ngoma Buhongwa ambavyo vilizawadiwa fedha taslimu Shilingi 150,000/= kila kikundi.
Jumla yaVikundi 6, vilijitokeza kushiriki fainali hizo za Mkoa wa Mwanza ngazi ya Mkoa kwa Mwaka 2014.
Akizungumza na kwanya kati tofauti Meneja matukio wa Kanda ya Ziwa, Erick Mwayela alisema Sababu msinigi ya kuwepo kwa Mashindano ya Balimi Ngoma za Asili ni kuenzi na kulinda utamaduni wa Kitanzania.
Mwayela aliongeza pia kuwa wao Kampuni ya Bia nchini ni sehemu yao ya kurudisha fadhila kwa watumiaji wa Kinywaji cha Balimi Extra Lager pamoja na vinywaji vyote vya Kampuni ya Bia Tanzania(TBL).